Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,167
- 5,613
Nimeona wengi wakiwa desperate wakitaka kazi, lakini mabandiko mengi yamekaa kihuni sana. Ni vigumu kupata kazi kama tu first impression itakuwa ni mhuni fulani hivi. Kwa sababu kizazi cha xoxo kimekuwa na mtindo wa kudharau vitu vya msingi kwa pretext ya "Usi complicate maisha", nimeona niwasaidie vijana na wanetu hawa. Lakini pia uzi huu unaweza kuwa msaada kwa mtu yeyote mwingine ambaye anatafuta kazi na anataka kufanya mambo kwa weledi
Yafuatayo kwa ufupi sana ni mambo muhimu kukuongezea nafasi ya kupata kazi
1. Usitumie akaunti iliyokaa kihuni. Unakuta mtu ana akaunti ambayo imekaa kihuni kihuni tu. Jina la kihuni, au hata halieleweki. Avatar anavuta bangi, signature ina vitu kiba inappropriate. Yaani sahau kupata kazi serious hata kama ni mtaalam kiasi gani. Picha atakayopata potential employer, ni ile uliyoichora kwenye avatar yako. Hata kama ni jina fake basi tafuta jina zuri, lenye maana fulani nzuri tu, weka avatar ya mtu anayejiheshimu na andika signature yenye vitu vya msingi.
2. Shiriki kwenye mijadala ya fani yako. Ukiwa bubu wa kuandika unaficha kipawa chako. Jaribu kushiriki mijadala ya fani yako kwa level uliyo nayo. Huko utakutana na opportunity. Unaweza kuta unajadiliana na mtu anayetafuta mhasibu au mwalimu. Ukichangia vitu postive halafu akalikuta tangazo lako la kazi, ni rahisi kukufikiria kwa sababu tayari ana angalau experience ya kujadiliana nawe.
3. Jadiliana na watu kwa nidhamu na heshima. Kuna watu inapokuja wakati wa kutafuta au kubadili kazi inabidi atumie akaunti mpya. Hii ni kwa sababu keshatukana watu wote aliotofautiana nao. Maisha ni kutofautiana. Ila hata pale unapotofautiana na mtu andika kwa staha. Mkosoe mtu kwa staha, na ukitanguliza nidhamu mbele kama tai. Mwajiri yeyote atapenda kuajiri mtu ambaye mnaweza kutofautiana asilimia 100 bila kutukanana au kugombana.
4. Jifunze vitu vingi nje ya fani yako. Unaweza kuta umesoma sociology lakini mjadala uliopo ni wa uhasibu. Jifunze mawili matatu kuhusu hiyo fani. Hujui hayo machache yatakusaidia wapi. Lakini pia kuna soft skills ambazo zinahitajika na kila fani. Jifunze hizo na anzisha au shiriki mijadala inayozihusu
5. Andika kama mtu anayehitaji kazi. Ni aghalabu sana kukuta hapa JF mtu ameandika kama kweli anaomba kazi. Unpotafuta kazi hakikisha bandiko lako limejitosheleza kwa taarifa ambazo sio identifying. Sema wewe ni nani, umesoma nini, umemaliza lini, unajua kufanya nini na nini bila kusaidiwa na unajua nini ambacho utahitaji kufundishwa ili uvifanyie kazi. Andika taarifa za kutosha kiasi cha mtu asiyekuhitaji asiulize. Hii itakusogeza hatua moja mbele kupata ajira. Usiandike tu kama kuku anatafuta sindano ambayo hajui hata kama ipo. Andika ukiwa na makusudi.
6. Andika kwa usahihi. Ukiandika vibaya vibaya hakuna mtu atakuchukulia serious, hata kama unajua mpaka unaumwa! Andika vizur kwa ufasaha. Kama kazi unayoihitaji inatumia kiingereza sana, basi andika kwa lugha hiyo. Hakikisha unapitia ulichokiandika kabla ya kutuma. Hii itampa picha mwajiri kama afuatilie zaidi au apotezee. Kunandika Xaxa, gdnite au ujinga mwingine, ujue hakuna atakayechukulia bandiko lako serious.
7. Onyesha una malengo gani na hii kazi. Moja kati ya tatizo la Watanzania ni kuwa professional normads. Yaani ndani ya miaka 3 amebadili kazi 6. Hapo average ni miezi sita kwa kila kazi. Hakuna mwajiri anataka ujinga huo. Kama unataka kukaa muda mfupi, onyesha kwenye bandiko lako. Kama unataka kukaa muda mrefu weka wazi pia. Usiwe vague kwenye nini kampuni watarajie toka kwako
8. Kama unataka kujitolea weka wazi namna unayotaka kujitolea. Je unatarajia kujilipia nauli na chakula au unatarajia upewe? Lakini pia unapojitolea kampuni inakupa ujuzi na maarifa. weka wazi wao watapata nini toka kwako? Je watakufundisha then ukiisha kujua unasepa kwenye green pasture? Au unatarajia kufanya nini? Wengi hudhani kujitolea unaipa favor kampuni au biashara inayokupa nafasi. Kimsingi wewe unayejitolea ndio mfaidika namba moja. Kwa hiyo washawishi watapata nini, baada ya wao kuwekeza kwao
Mambo yako mengi na wengine wataongezea, ila usidharau haya mambo ni muhimu sana!