Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,904
Uko Sahihi Mkubwa Aweda
Pengine tuna Tatizo la Kimsingi zaidi kuliko Mfumo wa Elimu. Hata kama tukiubadili Mfumo leo hatutapata mafanikio kwa kuwa hata kama tkiubadili mfumo na wahitimu wanaenda kufanya kazi katika mfumo uliocollapse ni lazima nia zao njema zitakuwa Transformed kuwa za Kifisadi. Ni vigumu kuwa mwadili wakati mfumo wetu wa kimamlaka unakusukuma upokee au kutoa Rushwa ili ufanikiwe.
Thats why nikasema thinking yetu ina matatizo lakini pia mfumo wetu wa kiutawala una Matatizo. Tanzania hii tunaishi kitumwa pasipo kujijua. Tunahitaji Kuibatiza nchi hii, tena ubatizo wa kuzamishwa katika maji izaliwe upya. Izaliwe upya katika kwa kubadili system ya Utawala, Kustructure upya kila kitu, sera za uchumi, afya, elimu, mahakama, ulinzi..kila kitu. Vitu vyote hivi vinategemeana na kila kimoja kinaathiri kingine. Iwapo tunahitaji mabadiliko ya kweli lazima tukae chini na kuisuka upya system ya nchi hii from zero. Ili kumwezesha daktari atibu kwa uhakika, engineer ajenge kwa moyo na akili thabiti, hakimu ahukumu kwa haki, polisi alinde usalama na haki mkulima alime kwa bidii, mfanyakazi afanye kazi kwa uhakika............. Kwa sababu hata tukibadili katika lakini mfumo wa utekelezaji wake ukawa ni huu huu wa sasa....Tunaendelea hivi hivi!
Ntulutumbi nimekupata,
Nakubaliana na wewe kuwa kila sehemu imeoza, serikali na sekta binafsi kote kunanuka rushwa na kuna kila aina ya matatizo. Kauli ya mbiu ya tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele ni aibu ya miaka 50.
Hoja yangu ni kuwa, kwa kuwa mahakama ni matatizo matupu, serikalini ( Ikulu, CAG, Takukuru, polisi nk) ni matatizo matupu, Bunge ndo usanii mtupu, tunahitaji kuanza mahali ktk kubadili au kubatiza ( as you said) nchi yetu. Hatuwezi kutangaza kwamba kuanzia tarehe 10/12/2011(mwaka wa 51 wa uhuru wetu) nchi yetu imebadilika. Hilo haliwezekani. Kwa kuwa mabadiliko (mabatizo ) haya tunayozungumzia siyo tukio la siku moja, ni mchakato wa zaidi ya miaka 5.
Kwa hiyo basi, kwa mapendekezo yangu, tunahitaji kuanza kwenye elimu. Hii ni kwa sababu elimu inafundishwa kwa watoto kuanzia miaka 3 au 5 chekechea hadi 21/25 - chuo kikuu ambao hawajachafuliwa nafsi zao kifisadi. Tukiwa na silabasi nzuri, siyo hii ya sasa ( silabasi inayozungumzia uzalendo, ubaya wa Rushwa, ubaya wa Uvivu, faida ya ufahamu mzuri wa ujasiriamali kukabiliana na umaskini), watoto ambao ni matunda ya mfumo huu mpya wa elimu, watakataa Rushwa, watakuwa wazalendo wakiwa mahakamani, serikalini, na Bungeni watatenda haki. Mashujaa wa kutaja orodha ya mafisadi bila woga kama Dr Slaa wataongezeka. Huu ndio utakuwa mwanzo mpya.
Hata hivyo, Serikali itakayosimamia mchakato huu wa kubadili nchi yetu lazima itangaze tarehe ya kuanza mchakato huo kama Nyerere alivyotangaza azimio la Arusha. Ijulikane tarehe x ( mf 10/12/2011) ni mwanzo wa kubadili nchi yetu kimfumo na kimaaadili japokuwa hatuwezi kusema itachukua muda gani. Vyombo vya habari vitangaze.
Pili, Lazima tukubaliane kuhusu mafisadi na wabadhirifu kabla hatujaanza mchakato huo. Kuna namna mbili. Kwanza ni kuwasamehe wote waliohusika kabla ya tarehe ya kubatiza nchi yetu ila warejeshe fedha zote walizoiba (Reconciliation).
Pili, ni kusema kwamba, wote waliofisadi nchi yetu huko nyuma tutawawajibisha kisheria kwa kuwapeleka ktk mahakama maalumu ya kubadili nchi yetu - ugumu wa hili la pili ni kuwa hakuna mbunge, mahakimu au viongozi wa serikali yetu watakaopona - kama wapo ni wachache sana. Majaji watakaosimamia mahakama hii ni wale wastaafu au walioopo wasiotiliwa shaka na majaji wenzao ktk utoaji wa hukumu - majaji wa namna hii wapo.
Tatu, hili litafanyika baada ya kupatikana kwa katiba mpya itakayokuwa imeondoa madhaifu yote yaliyojaa ktk katiba ya sasa inayompa rais madaraka makubwa sana - Rais mfalme. Na Rais atakayeongoza mabadiliko mabadiliko haya hawezi kuwa kikwete lazima awe mwingine ambaye hajahusishwa na kashfa ya aina yoyote - Rais mwenye Moral authority.
Thx