HOJA Kwamba Rais Samia hataki 'Jeshi' lake lichafuke? Kuna uwajibikaji tena hapo?

HOJA Kwamba Rais Samia hataki 'Jeshi' lake lichafuke? Kuna uwajibikaji tena hapo?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Akizungumza baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala aliowateua na kuwabadilishia vituo vya kazi Septemba 2, 2026, katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, Rais Samia Suluhu Hassan, alitaja moja ya sababu ya kuwateua kuwa ni kuwalinda na kuwapusha changamoto zilizokuwa zikiwanyemelea.

Rais Samia amewakumbusha viongozi hao kuwa wao ndio jeshi lake, "Nilisema kuwa wakuu wa mikoa nyie ndio jeshi langu. Sasa hakuna anayependa jeshi lake lichafuke.”

Rais Samia amebainisha kuwa uamuzi wa kuwabadilisha vituo vya kazi badala ya kuwaondoa umelenga kuwalinda na kuwaondosha katika matatizo na tuhuma mbalimbali alizokuwa akipokea kutoka katika maeneo yao ya awali.

Amesisitiza kuwa vituo vipya walivyopangiwa vinatoa fursa mpya ya kujirekebisha na kuacha tabia mbaya au kuingilia majukumu yasiyowahusu, ili wajikite kikamilifu katika kuwahudumia wananchi.

"Sasa kama ulikuwa unajijua unatabia mbaya au yoyote kule ulikotoka, kupya unakokwenda ni nafasi mpya kajirekebishe.”

Kauli hii maana yake Rais Samia anawalinda viongozi wabovu, wasiotumikia wananchi na wasio wawajibikaji. Badala ya kuwaondoa na kuweka wengine, yeye anawageuza hapa na pale. Ni kauli ya kusikitisha sana.
Inawezekana Mkuu wa mkoa analalamikiwa na wananchi, au ananyanyasa wananchi au anatumia tu vibaya madaraka yake, halafu anahamishiwa mkoa mwingine kuendeleza uovu wake.

Vinginevyo inawezekana Rais Samia alimaanisha kuna wakuu wa mikoa au makatibu tawala wanaojaribu kuhujumu utawala wake, hasa pale aliposema "kama ulipewa kazi wewe ni coordinator wa mambo fulani kaache u coordinator, tumikia watu."

Hata hivyo, bado Rais anapaswa kuwa mwajibishaji, sio kugeuza geuza viongozi, leo anawaweka hapa kesho kule.

Ni sawa na ile kauli aliyoitoa Machi 30, 2026 wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na ile ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), akitaka taasisi zilizofanya vibaya zitajwe ili zione aibu.

Soma pia: Kwa hiyo adhabu ya mafisadi ni kuwaaibisha?! Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Rais Samia

Kwanza ieleweke kwamba, utawala wa Rais Samia haujajiambanua kupambana na ufisadi, wizi, rushwa na ubadhirifu Serikalini. Hakuna wakati tumesikia viongozi Fulani wamewajibishwa kwa wizi, ufisadi au ubadhirufu, badala yake utasikia wamebadilishwa hapa, wamepelekwa pale, wamerudishwa huku, yaani serikali ya urejelezaji (recycling).

Sasa katika hotuba ya juzi Septemba 2, 2026, Rais Samia anawaita wateule wake kuwa ni jeshi lake ambalo halitaki kuchafuliwa. Pengine anamaanisha hilo ni jeshi la malaika wasiochafuka.

Tulitarajia Rais Samia atakuwa mkali kwa viongozi wasiowajibika mwa kuwaondoa kazini na kuweka wapya wanaoweza kuwajibika. Lakini mtu anaharibu hapa, unamhamishia mkoa mwingine halafu unamwambia akajirekebishe? Kwani hakuna viongozi wasafi serikalini au kwenye CCM?

Kauli hiyo haina tofautiani na ile aliyoitoa Januari 13, 2022 alipokuwa akizungumza na mawaziri na manaibu mawaziri jijini Dodoma, akisema “kila mbuzi hula urefu wa Kamba yake.”

"Mara moja nilisema kwenye baraza la mawaziri nikasema mimi najua kila mbuzi hula urefu wa kamba yake, jinsi kamba yako inavyokuruhusu ndivyo unavyokula lakini nikawaambia mbona mnakula sana? Mnavimbiwa! Si kweli kwamba hampati kwenye maeneo yenu, mnapata, lakini jipimie, jipimieni.”

Soma pia: Rais Samia: Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, lakini mbona mnakula sana mnavimbiwa? Jipimieni!

Kwa hiyo Rais Samia akawaambia mawaziri wajipimie? Kwamba kukitokea utekelezaji wa miradi huko wajipimie, lakini wasile sana. Hapo kuna uwajibikaji gani?

Matokeo yake sasa ndani ya Serikali kumejazana watendaji wasio na sifa, bali kazi yao ni kujipendekeza tu kwa rais ili waendelee kula na kujipimia wanavyotaka, lakini wananci wasio na fursa ya kujipimia wanaogelea kwenye umasikini.
 
Back
Top Bottom