Kwangu mimi, Regia Mtema ndio mbunge/mwanasiasa mahiri mwanamke mwaka 2011...

Ni moja ya sifa ambazo Mungu alimpa sasa mimi nifanyaje?

Uzuri upo kwa mtazamaji, wewe utaona mzuri wengine watasema anahitaji kwenda gym.

Isitoshe, uzuri unahusiana vipi na umahiri wa mbunge? Kwani ubunge ni beauty contest?
 

Unapaswa kufatilia records za Regia na sio kudandia gari kwa mbele utasagwa mkuu,kwa hakika Regia ametumia muda wake mwingi kuimarisha chama kati ya wabunge wanawake wa CDM...tatizo umfahamu vyema na kwa hiyo unakuja na hoja za kupinga tu kienyeji bila kuwa na vigezo......
 
Uzuri upo kwa mtazamaji, wewe utaona mzuri wengine watasema anahitaji kwenda gym.

Isitoshe, uzuri unahusiana vipi na umahiri wa mbunge? Kwani ubunge ni beauty contest?

Narudia tena uzuri sio sifa ya kuwa mbunge,kwangu mimi ni sifa ya nje ya!!!! ila kwa hakika ni kati ya jembe la kike kwa sasa kwenye siasa za Bongo...fatilia habari zake.
 
Migomo ya vyuo, unaonyesha wewe ni insider wa Chadema, kwa vile lengo la muanzisha thread ni kumfagilia Mhe. Regia Mtema ambaye ni mbunge wa chama chako, hivyo ni kiongozi wako, wewe kama mwanachama mtiifu, hukupaswa kuyaleta hayo mambo yake ya ndani humu!. Maadam lengo la thread ni fagilia, wewe kama hufagilii unajinyamazia tuu maana mbunge wenu akifagiliwa chama chenu pia kinazidi kupaa!.
 

Wewe acha kutia aibu hapa,kwani haya ni mawazo ya CDM au ya kwangu? una uhakika CDM walimchagua kwasababu ya uzuri wake? Haya ni mawazo yangu binafsi na yasihusihwe na chama changu hata kidogo...kama una la kuchangia nenda kafanya kazi zingine...
 
Angetakiwa kuwa number ya pili kwenye
Ile list ya most influential woman in Tanzanian.

I like her ..
we need people with strong personality.
She has my vote . Keep up Regina. .....
 

Wewe acha kutia aibu hapa,kwani haya ni mawazo ya CDM au ya kwangu? una uhakika CDM walimchagua kwasababu ya uzuri wake? Haya ni mawazo yangu binafsi na yasihusihwe na chama changu hata kidogo...kama una la kuchangia nenda kafanya kazi zingine...

Angalia huyu hata hajui kwamba chama ni watu, na kama wanachama wenyewe ndio hawa sioni ajabu CCM inakuwa vigumu kuitoa. Huwezi kutoa uozo kwa kuonyesha wananchi uozo mwingine, tuonyesheni mna chama mbadala kweli.

Nimeuliza Regia kafanya nini cha maana kupewa umahiri sijapata kitu chochote concrete. Is this the best you guys can do?

Kubali kwamba kuweka uzuri kama moja ya sifa ya umahiri wa mbunge umechemsha.
 
Kakemea wageni waondoke morogoro warudi kwao!!

Hiyo si distinction, sanasana ni xenophobia na kutoelewa dynamics za globalization.

Umasikini wetu hauwezi kuletwa na wageni. Na hatutatui kitu kwa kufukuza wageni kama hatuwezi kufanya kazi wenyewe.Tunatafuta mchawi.

Kuweka kumbukumbu sawa

Alisema hivi bungeni 'wasio wazawa wa Morogoro waondoke' akirejelea Watanzania wa kawaida.

Siku ya pili, alifuta kauli yake hiyo bungeni na kuomba Hansad irekebishwe

Kwa hiyo hakuwa akizungumzia wageni kutoka nje ya nchi, alikuwa anazungumzia Watanzania wengine msiruhusiwe kumiliki ardhi Morogoro kama hamkuzaliwa huko.
 

Haya ni mawazo mgando.

Kama mtu ni mchemfu ni mchemfu tu, na akisifiwa sifiwa isivyotakiwa, kama mtu ana data za kutuonyesha vingine, anatakiwa kutupa tu, ili mradi ziwe za kweli.

Hizi habari za kulindana kichamachama si ndio tunazikataa CCM?

Sasa kwa nini zikubalike CHADEMA?

Kwa nini tunataka double standards?
 

Ahsante,

Sasa mtu mchemfu kama huyu anaropokaropoka tu na kulazimika kufuta kauli yake bungeni. Mtu ambaye hata haelewi kwamba kwa mujibu wa katiba ya Tanzania hakuna Mtanzania atakayekuwa mgeni nchini mwake (nimeona upumbavu huu hata Professor Mwandosya anaongea, ina more tioned down disguise, hii nchi hii), kwani nchi ni moja na mtu anaruhusiwa kwenda popote ilimradi asivunje sheria, mpuuzi kama huyu ndio mmemuona mbunge "mahiri".

I mean I am not against CHADEMA, najua pia nobody is perfect, lakini huyu mediocre aliyeshindwa ubunge na kwenda kuupata mezani, kisha akasema ubunge unamboa hata bila ya kumaliza mwaka, huyu mpuuzi aliyekuja kuitukana constituency yake hapa JF kwamba ni "wabeba box" ndiye mnamuona mtu mahiri?

Is this the best you can come up with?
 
:A S thumbs_down:
 
Mm nimependa anavyo vaa nguo za heshima nywele ajaweka dawa(natural) upo juu dada
 
Nimeambiwa mbunge mahiri, umahiri hauji bila kazi inayoonekana, ndio maana nikataka kujua sababu za umahiri huu ni zipi ili tujue umahiri unaendana na kazi yake au la.
Mkuu Kiranga, with due respect, the motive behind hii thread ni consolation kwa Mhe. Regia Mtema kufuatia ile thread nyingine ya Wanawake 10 wa shoka Tanzania, kwa vile kule Mhe. Regia hayupo na kwa mujibu wa muanzisha mada kwake Mhe. Regia ndiye angestahili kuwa number 1 na vigezo vyake ndio hivyo kaviweka pia vikijumuisha gender yake, visibility yake, body mophology na ability etc.

Kwa vile huu ndio mtazamo wake, na hizo ndizo sifa zake, lengo likiwa ni kufagilia, nashauri kwa vile tuko kwenye festival season ungeacha tuu hii fagilia iendelee bila wewe kuingiza neno lolote!.

Kitendo tuu cha mwanamke kujaza form kugombea jimbo kwa kuzingatia hali aliyonayo dada huyu ni ushujaa tosha wa kustahili pongezi kwa sababu huko Chadema kuna wanawake wengi wamebwetekea viti maalum tuu. This means she is a dare devil with a darring heart!.

Tukija michango yake bungeni, kwa Mhe. Regia japo sio outspoken lady lakini she speak, she ask, hata kama anachoongea ni cha kawaida tuu au maswali yake ni mepesi lakini aneongea, anachangia na anauliza tena mpaka kwenye maswali kwa PM. Kitendo hicho kwa fans wake ni ushujaa maana kuna wabunge wangapi wako kimya kabisa!.

Wajameni hebu waacheni fans wawasifu watu wao this is festival season!.
 
Precisely,

Huu ndio umahiri wenyewe?

Labda kwa kauli yake hii

"Makinda is a good Speaker ever. I admire her. Tatizo lenu ni mfumo dume unawasumbua. She is Democratic."
 
Labda kwa kauli yake hii

"Makinda is a good Speaker ever. I admire her. Tatizo lenu ni mfumo dume unawasumbua. She is Democratic."

Kwa msingi wa wanachama kama hawa safari yetu si fupi hata kidogo.
 

Sasa mbona kwenye thread ile Mkuu hukuja kusema watu wasiponde? Ukamuacha Pindi Chana afananishwe na Chakula cha Kihindi? Au kuna privileges maalum kwa watu maalum? Kama kule hakukuwa na haki ya festive season, lipi linalofanya hapa kuwe na haki hiyo?

Besides, mtu mwengine atakuuliza festive season kwa nani?



Hapa bila ya kujijua umeleta dharau kwake. Kuwa yeye ni dhaifu sana, na kwa kuwa amejaribu kugombea basi apongezwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…