Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums

Kwanini Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) isianzishe campaign ya kuhamasisha wazazi kuanza kuwalipia watoto wao pesa kidogokidogo katika accounts maalum ya bodi wangali wakiwa bado wanasoma elimu ya msingi (Darasa la Kwanza)?

Jenga picha mtoto anasoma darasa la kwanza kwa miaka saba (7) kisha baada ya kuhitimu anajiunga na kidato cha kwanza mpaka cha nne kwa miaka minne (4) ambacho kwa sehemu kubwa hapa Tanzania ndicho kiwango cha elimu ambacho wanafunzi anaruhusiwa kujiunga na chuo cha ufundi kama amekosa fursa ya kuendelea na Advanced Level.

MATHEMATICAL BREAK DOWN
==========
Idadi ya miezi ndani ya mwaka: 12

Idadi ya miaka atakayosoma mwanafunzi kabla ya kujiunga na elimu ya juu/ufundi: 11

Kiwango cha chini cha uchangiaji kwa kila mwezi: 8,000/=

Makusanyo ya mwaka mzima kwa mwanafunzi mmoja - 12 x 8,000 = 96,000

Makusanyo ya miaka 11 kwa mwanafunzi mmoja - 12 x 11 x 8,000 = 1,056,000

Kutokana na takwimu niliyoipata humu humu jamiiforums: "Wanafunzi 947,221 wa darasa la saba kutoka shule 17,051 za Tanzania bara, wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kesho Jumatano na keshokutwa Alhamisi Septemba 12, 2019"

Just assume kwamba wanafunzi walioanza la kwanza ndio haohao waliomaliza darasa la saba na hakuna aliyekufa wala kuacha shule na idadi kamili ni 947,221.

Makadirio ya makusanyo ya mwezi kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza - 8,000 x 947,221 = 7,577,768,000

Makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza - 8,000 x 12 x 947,221 = 90,933,216,000

Kwa makusanyo kama haya kwa mwezi kwa wanafunzi wote takribani shilingi 90,933,216,000 bodi ya mikopo wanaweza kuwekeza hii pesa katika fixed deposits kwenye banks za kibiashara pamoja na kununua "government securities" na kupata returns kubwa na za maana tu kila baada ya miezi sita au mwaka.

Kama familia ina wanafunzi wawili mmoja akifa pesa zinahamia kwenye account ya mdogo/kaka yake.

Ndugu zangu, mimi sio mtaalam sana wa hesabu na uchumi lakini bila shaka idea yangu mtakuwa mmeielewa. Ninawakaribisha kwa michango zaidi pamoja na kukosolewa (Constructive Criticism)

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Rahisi mtu kumhamasisha kuweka akiba ya kifedha kwaajili ya afya yake (bima ya afya) sababu ya afya haiepukiki.


Ni ngumu mzazi kuweka akiba ya elimu ya juu kwa style hiyo uitakayo labda aiweke kwenye akaunti yake binafsi au amfungulie mtoto wake, mathalani mtoto asipofika elimu ya juu, basi fedha zaweza tumika kwaajili ya masuala mengine, kuliko kwenda kuitumbukiza kwenye akaunti ya bodi maana yake matumizi yake ni kwaajili ya elimu ya juu tu.
 
Kila chombo kinaundwa na sheria na kina majukumu yake mahususi. NSSF na PSSF wao wameweza sababu ni majukumu yao ya kimsingi ndani ya wigo wao, tena kuna mafao kwa wanufaika yanayogusa elimu.


HESLB wao sio jukumu lao, ni bodi ya mikopo yaani wao wanatoa tu funds kwaajili ya wanufaika kwa vigezo vyao, labda utaratibu ubadilishwe kuwezesha wazo lako.
Sawa utaratibu ubadilike kama wataona inafaa
 
Malalamiko yapo kila sehemu kwenye hizi taasisi haswa za serikali hata bodi ya mikopo inalalamikiwa mnooo.

Sasa je tunafanyaje?
Malalamiko yenye tija yafanyiwe kazi kwa manufaa mema ya taasisi husika na yale ya uzushi yawekwe kando
 
Nafikiri wapaswa fahamu mchango wa sekta binafsi ktk maendeleo ni mkubwa mnoo na hiyo serikali inatambua ushirikiano wa PPP ( Public and Private Partnership).

Taasisi binafsi zina shukrani kwa jamii, labda kama ni taasisi uchwara, ktk utendaji wake mathalani kampuni kitaalamu na kisheria zinapaswa kujitoa kwa jamii (corporate social Responsibility) sehemu ya faida yao wanairudisha kwa jamii achilia mbali kodi yao wanayochangia kwa serikali ambayo huleta maendeleo uyatakayo.

Uzoefu unaonyesha, huduma inayotolewa na serkali peke yake bila ushirikiano na sekta binafsi ina changamoto kubwaaa mifano ipo lukuki.
Mkuu, siwezi kuingia JF kuishauri taasisi binafsi. Huu ndio msimamo wangu.
 
Tatizo la huyo mzee baba ni kupenda mademu wa masaki na mbezi beach. Dada zetu wa uswahilini a.k.a kuku wa kienyeji hana time nao kabisa.
Sasa anapenda mademu wa kishua anazo pesa za kuhonga? Kama hauna hela mademu wazuri wote utaishia kuwaita shemeji.
 
Napata
Mkuu, siwezi kuingia JF kuishauri taasisi binafsi. Huu ndio msimamo wangu
Huu uzalendo wako unatusihi kila siku, ni kwa serikali ama kwa nchi?

Yaani unaipenda serikali ama waipenda nchi?

Kama waipenda nchi hutaona ugumu kutoa ushauri kwa sekta zote, lakini kama waipenda serikali utajikita kwa serikali tu.

Chaguo ni lako!
 
Napata

Huu uzalendo wako unatusihi kila siku, ni kwa serikali ama kwa nchi?

Yaani unaipenda serikali ama waipenda nchi?

Kama waipenda nchi hutaona ugumu kutoa ushauri kwa sekta zote, lakini kama waipenda serikali utajikita kwa serikali tu.

Chaguo ni lako!
Mimi ninaipenda kwanza nchi yangu alafu serikali. Sekta binafsi siwezi kuishauri ndani ya jamiiforums. Ninaweza kuishauri nje ya mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom