Uko sawa mkuu,pia uchaguzi wa mwaka huu tofauti kabisa na chaguzi zote,umekuja na aina mpya ya campaign.Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa ni juu ya maswala(ISSUES) na bla bla.
CCM walijiuza kwanza kwa kueleza WAMEFANYA nini miaka mitano iliyopita (wananchi wanatafakari na kuona kweli)Kiisha wanaomba kura na kuwaambia wanachi WATAFANYA nini miaka mitano ijayo(wananchi wanaona kuwa ni kweli maana waneona nini kimefanyika).
Ukienda upande wa pili hupati picha.
Mgombea kila kukicha issue ni yeye kupigwa risasi,kumtukana aliyeko madarakani,kulalamika,na kwa bahati mbaya sana kujichanganya,alichosema leo anasahau na kurukia kingine-mifano.
Kabla ya uchaguzi alisikika akisema watamshitaki Magufuli kwa kuwa amefanya campaign kwa miaka mitano baadaye amegeuka na kushangaa inakuwa ccm wameshinda wakati wao wamefanya mikutano mingi kuliko Magufuli?Sasa hapa uchue lipi?
Pili alisikika akisema wao wanataka maendeleo ya watu na sio vitu,Mara kauli hiyo akaisahau alipopand mwendokasi kwenda shopping kariakoo,akasikika akisema usafiri huu ni mzuri unapaswa uenezwe mji mzima EBO sasa ukienezwa mji mzima inakuwa maendeleo ya watu au vitu? Mtu kama huyu unamuelewa vipi?
Tatu amekuja na sera ya majimbo,alipobanwa kidogo tu hakuzungumza tena kuhusu majimbo.Sasa watu watakuelewaje?
Nne Kaja wa wakili Mr Armstadaum.Akawa mtovu wa nidhamu kupindukia anamwandikia mkuu wa nchi barua au waraka usiokuwa na heshima,anatisha na kusubutu kusema kwa nini CCM ipo wakati vyama vyote vilivyoleta uhuru vimekufa?
Ebo,mbona ahoji kwa nini Labour Party au Conservative vya Uiongereza bado vipo? Kwa nini haoji Republicane au Democratice vya marikani bado vipo?