Tukirejea katika Bunge lililopita, laiti vyama vya Upinzani vingekuwa na Wabunge wengi, huenda wangefanikiwa kuishinikiza Serikali ifanye "lockdown" jambo ambalo kama ilivyotokea kwa nchi jirani lingepelekea mateso makubwa kwa mamilioni ya wananchi. Kwa kuzingatia ukweli kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mazingira ya COVID 19 duniani, haikwepeki kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa ni kipimo cha uongozi.
Kama inavyoeleweka, nyakati za majaribu ni nyakati za uongozi. Watu ama hubadilisha uongozi kwa kutafuta jemadari mpya, ama huwekeza imani zaidi kwa jemadari aliyepo anayefanya vizuri.
Watanzania wameling'amua hilo-na wamejibu katika sanduku la kura kuizawadia CCM ushindi wa kishindo. Haishangazi pia kuwa Serikali zilizoshindwa kuendesha mapambano haya kwa ufanisi- zimeadhibiwa na wapiga kura. Siku chache zijazo tutaona yatakayotokea katika uchaguzi wa Marekani. Laiti Kenya ingefanya uchaguzi mwaka huu, Rais Uhuru Kenyatta na Chama chake Jubilee wangeanguka vibaya sana.
View attachment 1617270