pCpCp RICH THINKER
Senior Member
- Apr 5, 2021
- 121
- 103
FURSA
Fursa ni mwanya, nafasi ama uwezekano wa kufanikisha jambo fulani (kwa minajili ya makala hii–tafsiri hii inatufaa).
Nikupe mfano:
Nikupe mfano:
Chukulia mmefungwa kwenye chumba, tuseme watu mia moja na dhima yenu hapo ni kutoka nje. Hata hivyo, kanuni inasema: “atakae toka basi anakuwa huru”. Chumba kina paa, madirisha kadhaa, mlango mwembamba na kuta za maana tu. Tena kanuni inasema “mtu anaweza kufanya jambo lolote ili kujiokoa”.
Katika mfano wetu, namna yoyote itakayomwezesha mtu kutoka nje hiyo nifursa. Fursa ni uwezekano wa mtu ‘kutoka’. Kama kuna kitu ama hali inayoweza ‘kukutoa’ kimaisha hiyo ni fursa !
Dunia hii ina fursa ‘kibao’ zinazoweza kumtoa mtu. Pamoja na hayo, tabaka la ‘wasionacho’ na ‘walionavyo’ halijawahi kuisha–fursa. Umaskini na utajiri ni hali zinazotengenezwa, haziji kwa bahati mbaya. Uwezekano wa mtu kuwa tajiri ama maskini ni juhudi za mtu mwenyewe, mtu anachagua. Wazazi/walezi wako kuwa maskini hiyo sio hoja; wewe kuwa maskini unahoja ya kujibu. Ni suala la kuchagua tu, usiwe na visingizio jiwajibishe.
Fursa zimejaa kila kona, fursa zinawazunguka watu na zingine wanazikanyaga lakini watu hawatoki—umaskini unawatafuna watu. Mpaka unaowatenga maskini na matajiri unazidi kuwa mpana. Sababu ni kuwa kila mtu anang’ang’ania anachokijua: tajiri anaona fursa; maskini haoni kitu. Tajiri anawajibika, anatumia fursa; maskini analaumu, anatafuta huruma. Mwenye nacho anaongezewa zaidi.

TABIA ZA FURSA
a. Fursa ina tabia ya ‘kufa’ na ‘kuzaliwa’, ‘huzaliwa’ hapa ‘hufa’ pale. Fursa huibuka na kupotea. Mazoea , acha mazoea—dunia yetu pendwa inabadilika kila uchao. Dunia ikibadlika ‘fursa pendwa hufa’; fursa mpya huzaliwa. Dunia ni watu. Fursa ‘huzaliwa’ hapa na ‘kufa’ pale kwa sababu ya: maendeleo ya teknolojia, kubadilika ama kuhuishwa kwa mahitaji ya watu, kubadilika kwa tawala za kisiasa, kubadilika kwa sera na sheria za nchi, mabadiliko ya mazingira nakadhalika nakadhalika.
Chochote kikitokea hapo kuna fursa zinakufa na fursa mpya zinaibuka.

Kwa mfano: katika utawala wa nchi —akiingia kiongozi ‘x’ madarakani—kuna fursa zitakufa; kuna fursa zitazaliwa, ukifananisha na utawala wa kiongozi ‘Y’.
Kuwa mweledi na chunguza kipi ufanye na kipi usifanye ili ubaki kwenye ‘mdundo’. Kucheza kwa mdundo kupo katika kuendana na mambo ama kujinufaisha na hali iliyopo—yote haya yanakuhusu. Watu hufilisika kwa sababu ya kufanya mambo ambayo yamepitwa na wakati.
Miaka ya 2000 wakati simu za mkononi zinaingia-ingia, huduma ya vibanda vya simu ilikuwa ni fursa lakini kwa miaka hii ya 2021+? Tafakari katika hili na huisha akili yako.
b. Fursa hutengenezwa. Unaweza kuwatengenezea hitaji watu kwa kuwazoesha. Binadamu ni mhanga wa mazoea– katika hili unaweza kusimama upande chanya na kuvuna kitu kutokana na kasumba hii ya watu.
Kutengeneza fursa ni kuliona hitaji ambalo watu wanalo japo wao hawaoni kama wanalo. Ni kitendo cha kuibua hitaji. Kama unaibua, tafsiri yake ni kwamba hitaji hilo ‘lilikuwa fiche’ kwa hiyo wewe umelifichua. Kama unaamini kwamba unaweza rahisisha utendaji wa mambo fulani fulani kwa kuleta huduma ama bidhaa fulani— tayari umejitengenezea fursa. Kwa kutumia ubunifu na fikra tunduizi watu hutengeneza fursa.
c. Kama fursa inaangaliwa na macho mengi hiyo sio fursa kwako; ni ‘takataka’. Fursa ikiangaliwa na watu wengi hukosa kuwa fursa. Ushindani unatokana na watu wengi kuishughulikia fursa moja. Katika fursa moja watu hufanya njia tofauti tofauti ili kusudi tu kupata walaji. Fursa ikiwa ni pana inaweza kuwatoa watu lakini kama ni finyu itakufa ama itakuwa ni ngumu kwa watu wengine kufanikiwa katika mwanya huo. Usifuate mkumbo, tathmini unachokifanya kitakuwa ni fursa miaka ijayo ama ‘takataka’.
Fursa ikiwa imejaza watu wengi huibua ushindani. Ushindani ni faida kwa mlaji (mteja). Wenye nguvu ndio huweza kutoka katika fursa za namna hii. Kama kila mtu anafanya manake mlango uko wazi—wenye nguvu ndio huweza kutoka katika fursa za namna hii. Kama huna nguvu, fursa ya namna hii sio fursa kwako –hautafika mbali.
Kwa mfano:
Unaweza kutengeneza soda lakini ni fursa ambayo haiwezi kukutoa kwa sababu ushindani ndani yake ni mkubwa, hautauweza. Utashindana na Coca-Cola™ ama Pepsi™ ? Utatoka kwa wakati? Katika mfano wetu, wa watu mia ndani ya nyumba, ni sawa na watu wote kung’ang’ania kutokea mlangoni. Hapo ndipo watu husema huwezi kuwa tajiri kama hakuna historia ya utajiri katika familia yako.
Fursa zimetofautiana katika uhai na mapana. Kuna fursa za muda mfupi, fursa za muda mrefu na fursa za wakati wote. Usivae miwani ya mbao, hautafika mbali. Hakuna fursa ambayo inadumu milele! Maisha yanakuwa magumu wakati mwingine kwa sababu ya kuamini fursa fulani itakuwepo wakati wote. Mathalani,
Fursa fupi: wakati wa korona, mwanzoni mwa mwaka 2020,hapa kwetu Tanzania watu waliuza vipukusi, barakoa na sabuni— ni fursa ambayo iliibuka. Baada ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza kwamba “sasa hakuna korona Tanzania ”, wajasiriliamali wengi waliochangamkia fursa hii walipata wakati mgumu sana.
Huo ni mfano wa fursa fupi.
Usafirishaji ni fursa pana lakini ndani yake kuna ‘vitengo’ tofauti tofauti. Hii ni fursa pana na inaweza kuwa ni fursa ya wakati wote. Fursa hii itakufa ikiwa watu wataacha kutembea —kitu ambacho nadra sana. Hata hivyo, kuna jambo ambalo ni bayana, watu wanaweza wasiache kusafiri lakini wakabadili ‘vionjo’ katika kusafiri. Kwa hiyo kutoka kwako kwenye fursa pana kunategemeana na namna gani unavijua ‘vionjo’ vya walaji na muhimu zaidi ni kwa ufanisi upi unakidhi katika kutimiza vionjo husika.
Katika fursa moja kunaweza kuwa na mseto wa matakwa ya wateja. Dunia hii inaongozwa na nini wateja wanataka (uhitaji); ukijua kutimiza nini watu wanataka katika fursa husika, fursa hiyo itakutoa. “Akili mukichwa” siku zote.
Jiulize “je, fursa niliyonayo itadumu kwa muda gani?” Jiulize, “je, itakuwa fursa mwaka mmoja, miwili au mitano ijayo?”
d. Fursa hutegemeana na uoni wa mtu. Wanasema unaona unachoamini, kwamba unaamini ndipo unaona na sio kinyume chake. Katika jambo moja watu tunaweza kuona tofauti tofauti. Kwa mwingine ikawa ni fursa, kwa mwingine ikawa takataka; kwa mwingine ikawa ni matatizo. Ni katika kuona huku ndiko kunaleta tofauti katika jamii.
Huyu anahitaji picha kamili ili aione fursa, yule anahitaji nukta mbili za kuunga ili aione fursa. Mwingine anaona takataka; mwingine anaiona fursa miaka kadhaa ya usoni. Habari mbaya ni kwamba hakuna awezaye kufikiri kwa niaba yako katika suala zima la kuiona fursa. Fikra zikiwa butu utaona vitu visivyoeleweka.
Habari njema ni kuwa unaweza kujifunza kuziona fursa. Ukifanya mazoezi ya kunyenyua vitu vizito, ‘vyuma’ una nafasi kubwa ya kuwa ‘tuna’—baunsa. Halikadhalika izoeshe akili yako kufikiri utaona tofauti na wanavyoona wengi. Kuwa wakipekee ni lazima ufikiri. Kipi kwako nihalisi na kipi sio halisi? Unachoamini utakiona.
Katika mfano wetu wa kwanza— watu 100 ndani ya nyumba— mtu anaweza kufikiria kutokea juu ya paa; wakati wengi waking’ang’ania kutokea mlangoni.
e. Fursa zipo kila sehemu. Hakuna sehemu amabayo hakuna fursa, hakuna! Kama kuna watu, basi kuna fursa. Shida ‘iko’ na wewe; ‘haiko’ sehemu uliyoko wala haiko na watu ulionao. Unaona nini? Taswira kubwa? Taswira ndogo? Ama hauoni chochote?
Watu wengine huhama sehemu ambazo wanajulikana, labda wamezaliwa hapo na kuenda ‘kutafuta maisha’ sehemu zingine. Hata hivyo hii haina maana kwamba pale walipo hakuna fursa; wao nd’o hawazioni! Watu wengi huzamia mjini kwenda ‘kutafuta fursa’. Fursa zipo kila sehemu ila fursa huwa fursa kutegemeana na uoni wa mtu katika sehemu husika.
Itoshe tu kusema kuwa kama sehemu uliyopo ‘haujaona’ fursa sio mbaya kuhama. Kuhama kwako inaweza kuwa fursa ama takataka kwako. Itakuwa fursa ikiwa utatumia uzoefu ulionao sehemu uendayo. Unaenda kutengeneza fursa nyingine. Sio lazima lakini kama ndivyo unavyoamini kuhama kwako kunaweza kuwa fursa sehemu nyingine, utahamasika hivyo kwa sababu ndivyo unavyoona.
f. Fursa huanza na wazo; ‘mazingira’ yanayolizunguka wazo huamua kama wazo ni fursa ama ni udhahania tu. Kwa maneno mengine ni kwamba sio kila wazo ni fursa . Ikiwa wazo halitekelezeki katika mazingira uliyonayo basi hilo wazo sio fursa. Wazo linatakiwa kutunga mimba ya kukupatia kile kinachotakiwa, ama sivyo wazo linapaswa kusitishwa ama kusubirishwa ama ‘kusanifiwa’ upya ili lipate uhalisia katika kulitenda.
Wazo lenye hatma ya kuwa fursa lazima likupe picha inayoonekana muwazaji (mtoa fikra) vinginevyo liache likomae, kwa sababu mazingira hayaruhusu kustawi kwake. ‘Wazo bichi’ halitekelezeki kwa sababu kwa sababu ni geni hata kwa muwazaji. ‘Wazo bichi’ lazima lipewe muda au lipitishwe katika ‘tanuri’ la fikra ili kuondoa udhania mwingi uliomo ndani yake.
Mazingira kama watu (walaji), muda, sehemu, na teknolojia vitaamua kama wazo ni fursa au ni wazo tu.
‘Wazo bichi’ litakuchelewesha. Maana yake ni lazima uwe mwangalifu katika kuchagua mawazo sio kila wazo linaweza kukufanikisha kwa muda mwafaka—kwa kuzingatia mazingira uliyonayo. ‘Wazo likikomaa’ litakidhi vigezo vingi na litakufanikisha ‘chapu–kwa haraka’. Usifanye kazi ya kuchemsha mawe; hayataiva na utalala njaa!
g. Fursa haingojewi. Kama huwezi kuitengeneza basi ifuate; ukiingoja hautaipata. Watu waliobwetesha bongo zao hutafsiri mafanikio kama bahati. Wameridhika na hali zao kwa sababu wameamini hatima zao zipo katika wao kuwa na bahati ama kutokuwa na bahati—kamali ya mafanikio.
Hoja makini ni hii, na ni kweli tupu: KILA JAMBO LIPO KWA KUWA LIMESABABISHWA, hakuna jambo ambalo halina sababu ama chanzo. Kufanikiwa ama kutokufanikiwa vyote vinatengenezwa na mtu— na hii pia ni kweli tupu. Kama ni kufanikiwa basi sisi sote tuna bahati. Kama una uhai na unapumua hiyo ni bahati kubwa uliyonayo na ya msingi. Bahati ndogo ndogo unaweza kizitengeneza mwenyewe, kikubwa ni kujindaa. Ndio kwa sababu bahati humpata aliyeitengenezea mazingingira, bahati humpata aliejianda. Kama hujajiandaa huwezi kubahatisha.
Usingojee fursa kama mtu aliye kituoni akimsubiri ndugu yake kutoka safari ya mbali.
Fursa kama donge kubwa inaanzwa kwa kumegwa katika vijitonge vidogo vidogo. Inawezekana vipi ni suala la wewe kujichechemusha na kuzimua akili yako vinginevyo hakuna kitu ambacho kitawezekana katika dunia hii. Ukiamini hakuna kinachowezekana katika dunia hii hii asili itaungana na imani yako na kukuletea matunda yaliyosawa sawa na imani hiyo!
Kuingojea fursa ni kuupalilia umaskini. Kuichangamkia fursa nini kufanya maandalizi mazuri ya kuipata fursa. Kumeng’enya kubwa la fursa ni kuanza na ‘vijifursa’ vidogo vidogo vinavyokuweka katika mazingira ya kuivuna fursa kubwa. Matajiri huchangamkia fursa; maskini hutafsiri mchakato huo kama tamaa.
Usiingojee fursa kwa sababu haitakufikia na kama itakufikia nachoona itakuwa imehafifika mno. Ongeza uwezo wa kufikiri, fikra zako zitaakisika katika maisha yako. Amka!
h. Kwa sababu pana watu, pana fursa. Fursa zipo kwa sababu kuna watu. Hata kama mko wawili tu, hapo kuna fursa bwerere. Fursa hazikomi, fursa haziishi kwa sababu binadamu tuna mahitaji mengi na hakuna mtu ambaye anajitosheleza. Uwepo wa mtu ‘A’ na mtu ‘B’ katika sehemu fulani hapo kila mtu kuwa fursa ya mwanzake. Fursa haziishi kwakuwa hakuna binadamu amabaye anajitosheleza; ondoa vumbi kwenye ‘bongo’ zako. Hakuna mtu anaejitosheleza katika dunia hii iwe: mtu na mtu, kikundi na kikundi, taifa na taifa, naam bara na bars—mahitaji hayakomi. Afrika, Marekani, Ulaya, Asia, na Australia wote tunategemeana na, ni katika utegemezi huo basi utitiri wa fursa huibuka.
Dhana ya huyu bora, yule dhaifu ni ‘kujimwambafai’ ambako hakuna misingi yenye mashiko ya kweli. Utumwa hutokea kwa sababu mtu ‘A’ amegundua kwamba uwepo wa mtu ‘B ’ ni fursa na ameamua kuitumia ili hali mtu ‘B’ hajaona chochote kutoka kwa mtu ‘A’ kama fursa. Utumwa hauwezi kukomeshwa kwa mtu ‘A’ kuacha kumtumia mtu ‘B’ —kwa maana ya kupata usawa; bali utaondoka kwa mtu ‘B’ kung’amua fursa kutoka kwa mtu ‘A’.
Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi nukuliwa akisema “...akili ya mwenzio changanya na ya kwako”. Haya ya mneno yangu sas: ...kama akili yake imeendelea sana akili zenu hazitachangamana; utitumia ya kwake tu, utaishia kuinakili kama kama ilivyo. Utumwa huanzia hapo.
“Penye watu pana fursa”, maana yake kama nina uhitaji na siwezi kupata hitaji langu ama kuna ugumu ambao kwangu ni changamoto; na wewe umegundua unaweza kunipatia hitaji langua kwa njia rahisi sana, mimi nimekuwa fursa kwako. Penye watu lazima pana kitu cha kufanya ambacho kinaweza kukutoa kwa wakati uliopo.
Hatuwezi kukataa ukweli kwamba wakoloni walitutawala. Hata hivyo, kuhusu umaskini wa mtanzania ama mwafrika kwa ujumla sababu zake sio sahihi kumbebesha mkoloni. Umaskini wa mwafrika mizizi yake sio ukolon:
Afrika haijawa na ni maskini kwa sababu ilitawaliwa na mkoloni. Mkoloni ameondoka zaaidi ya miaka 30 ama 50 iliyopita lakini bado adui umaskini yupo palepale miongoni mwa wa watu.
Hoja ni kwamba wakati wenzetu wanatutumia sisi kama fursa, sisi hatujawatumia wao kama fursa—wana tuzidia hapo kete. Wananajitengenezea fursa kibao kwa kuwepo kwetu lakini sisi tunatengeneza fursa dhaifu kwa kuwepo kwao katika sayari hii. Wao wanaona tuna uhitaji mkubwa sisi hatuoni kitu ama tunaona kiinimacho tu.
i. Hakuna uhaba wa fursa bali kuna utele wa fursa, fursa hazijawahi kuwa adimu. Kwamba kuna uhaba wa fursa huo ni uwongo, fursa hazijawahi kuwa adimu. Binadamu tupo na tustawi kwa kutoshelezana, tuna tegemeana. Ukijua shida ya mwenzako na namna ya kuitatatua, huyo atakuwa fursa kwako. Usichanganye mambo, ‘kutegemeana’ hakuletwi na dhana za: utajiri na umaskini, ‘wasionacho’ na ‘walionavyo’; waliosoma na wasiosoma n.k.
Uwepo wa matabaka hayo hauna mchango wowote katika kutegemeana— na hayo ni kweli tupu. Ni uongo na imani potofu kuamini kwamba ‘tajiri yupo kwa sababu maskini yupo’ ama kusema mtu ‘A’ amekuwa tajiri kwa sababu mtu ‘B’ kawa maskini.
Ni uongo na hakuna kweli zozote katika kuamini ‘hatuwezi kuwa matajiri sisi sote; nani atakuwa maskini?' Hizo ni fikra finyu na funge. Fikra huru na nyumbulifu ni hivi: kwa sababu pana watu ; pana fursa. Maisha yanaenda kwa sababu tunahudumiana. Ukihudumiwa, hudumia pia. Ukisema “sina chakuhudumia” ni uongo. Uongo uliojirudia huwa ukweli.
Kama huna cha kuhudumia maana yake huna chakuuza— tafsiri yake ni unanunua sana na huna cha kuuza. Ukweli mchungu maskini huhudumiwa sana na wao huhudumia kidogo ama kutohudumia kabisa . Wanakwama hapa!
Tuchunguzane, tujuane mahitaji yetu ni yapi. KUWA TAJIRI; KUWA MASKINI, ni hatma inayochaguliwa na mtu mwenyewe. Ukubali ukatae kuhusiana na hili, haifanyi kanuni hii kutofanya kazi kwako—uchaguzi wako unakupatia matunda unayostahili. Wote tunaweza kustawi na dunia ikaenda, cha msingi tujue kuhudumiana.

Upvote
2