Busara gani hasa..?
The only busara iliyo wazi kabisa kwa sasa ni:
1. Freeman Mbowe akae pembeni, aachie uongozi wa chama kwa watu wengine...
2. Kama akisema "sanduku la kura liamue", basi asijaribu kuhujumu uchaguzi huu kwa kusaidiwa na TISS ya CCM na mbinu zao chafu Ili mradi tu abaki madarakani...
3. Sambamba na namba 2 hapo juu; uchaguzi ufanyike ktk mazingira ya uwazi, haki na kila mtu aone kila hatua ya haki ikitendeka Ili atakayeshinda ionekane wazi na kila mtu kuwa ameshinda kwa haki.
Hili likifanyika sawasawa, lita minimize damage mara baada ya uchaguzi kupita na itasaidia wanachama na chama kuwa kimoja.
Lakini kwa hali ilivyo sasa, inaonekana wazi kuwa Freeman Mbowe hataki kuachia kiti kwa amani na anaweza kutumia njia zozote haramu kujishindisha ktk uchaguzi huu na CCM wako kwenye mikakati mizito ya kumsaidia kufanikisha hili kwa kutumia fedha maarufu kama "pesa za Abdul" na mifumo ya kiserikali - TISS....
Hili likiwa hivi, ndo nasema patawaka moto. Yale tuliyoyaona yakitokea kwenye vyama vya CUF na NCCR watu kufungiana milango na kugawana ofisi yatatokea CHADEMA pia...
Na ikitokea hivi, I am afraid kusema kuwa CHADEMA inaweza kubaki Machame na pale makao makuu DSM pekee!
Mbowe ana busara hii kweli..?