Mimi nilitimuliwa home nikiwa na miaka 22 tu mzee kaniambia nioe au nikavue dagaa,niliondoka kweli na form four yangu ya 26 nikaingia mtaani nilianza kuchoma mawe na kupasua nauza nikawa nasukuma na mkokoteni kama mwaka mmoja hivi huku naishi kwa mama mdogo mwaka uliofuata nikaenda veta nikagonga miaka mitatu fani bomba nikakomaa mwenyewe kila kitu ndani ya miaka mitatu pale musoma na ule wa kupiga kazi ya mkokoteni ukawa mwaka wa 4,2016 nikamaliza mafunzo yangu nikakaa miaka 4 2020 ndo nikapata ajira leo hii mzee anapiga simu sana anaomba pesa nampa na mpaka sasa nasomesha mdogo wangu anachukua diploma ya civil engineering
Pengine wanataka ukajitegemee akili ifanye kazi