Kwani lazima kuoana?

Kwani lazima kuoana?

Unachukia kuoa kwa sababu hauko tayari kwa unachoita 'relatioship stress...' labda wewe bado ni dogo sana, kuna mtu alikudanganya kuwa watoto wa ku-adopt wote ni malaika??? Je kwa bahati ukikumbana na mwenye usumbufu utafanyaje?! Stress ziko kwenye mambo mengi utayakimbia yote?? Kama huna hisia zozote za kuwa na mwanamke hapo sawa, lakini kama unataka kuchakachuwa tu bila kuoa una laana kubwa. HAKUNA ANAYEKULAZIMISHA KUOA ila kumbuka, mara nyingi ukipingana na nature itakula kwako..... Tafakari.
 
Miaka 22? We bado mdogo, sawa mdogo angu, soma kwa bidii kama unasoma, kama unafanya kazi, fanya kwa bidii pia weka akiba timiza malengo yako ya kiuchumi. Hayo ya mahusiano yanakuja yenyewe tu, kama ndoto vile, sawa dogo?
 
Kuhusu mimi:Male 22 yrs,cna girlfriend and No plans to have one,i'm happy with my life.Kuna kitu kinanikera sana,hivi kwani ni lazima kila mtu aoe?????? kwanini nikisema nataka kuadopt mtoto watu wananiona mutant?:typing: i've seen people do it(stay single and they are happy)i'm not ready for Relationship Stress and i'm not sure if i will someday.:and one thing; I HATE MARRIAGE!!!!!!!!MARRIAGE SUCKS!!!!!!!!lol!

I can smell a problem there.
Please, if you don't mind, tell us about your family...
 
Olewa wewe basi ionekane moja wewe KIPENZI...hata Elton John idol wako kaadopt mtoto so follow your role model....
 
That means, you don't want to live With Idiot For Ever.
i'm not sure if WIFE is the acronym of that statement,i mean't single life sio kuchezea watoto wa watu,I think there are many things to do in this world other than marry and i can find many things to keep me busy.I was raised by my Mother alone, and sina bahati ya kukaa na baba hata wiki moja pamoja (si kwamba amekufa),I guess he don't care and i don't either,I'm working as a Network Admin. at a certain Org(Planning to go back to college) and i really hate when People asks me Utaoa lini.Meanwhile, Thanks JF Members,You are my Friends thou i can't see you.
 
Ndoa ni maamuzi yako. Una sound kama una psychological problems zinazo originate from you past. Tafuta msaada kama hutajali.
 
Paka hapo wakulaumiwa ni baba yako inaonekana alimlaghai mama yako then akamtelekeza.so umepata upendo wa upande 1,inatokea lakini kunakipindi utatamani kuwa nae (mke)mi nildhani we si rejali..
 
Mwenzenu jana tulikuwa na mjadala nyumbani kwetu, na mada kuu ilikuwa ni juu ya namna nzuri ya kupata mwenza.Dada yangu mkubwa ndiye aliyeanzisha huo mjadala kwa kumuuliza mama kuwa kwanini zamani ilikuwa ni jambo la lazima mtu kutafutiwa mke au mume wa kuoa au kuolewa?

Mama alikuwa na haya ya kusema. Alisema kuwa kimsingi hapo zamani wazazi walikuwa wakiwatafutia watoto wao wenza wa kuoa au kuoelwa na lengo kuu lilikuwa ni kutaka mtoto wao aangukie katika mikono salama na mojawapo ya vigezo vikuu vilivyokuwa vikiangaliwa ilikuwa ni historia ya ukoo husika, kwa mfano, je ukoo huo unaanguka kifafa?

Je ni ukoo wa wachapa kazi kwa maana ya kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii (Ikumbukwe kuwa zamani kazi kuu ilikuwa ni kilimo). Je Sio ukoo wenye mkono mrefu, yaani sio wezi ( Sijui kwa nyakati hizi kuna haja pia ya kuwajumuisha na mafisadi yaani kama ukoo una hulka ya ufisadi)Jambo lingine lilikuwa ni kuangalia kama ukoo unashambauliwa na magonjwa sugu, kama vile anemia (Upungufu wa damu wa mara kwa mara) Kansa, kisukari na maradhi mengine yaliyokuwa yakitafsiriwa kuwa yanaweza kuushambulia ukoo.

Sina hakika kama vigezo hivyo bado vinazingatiwa kwani kule vijijini bado utaratibu wa kutafutiana wenza upo lakini sio kwa kiwango kama cha zamani kwa sababu ya mabadiliko yaliyoikumba jamii, kwani kila mtu sasa na lwake.
 
Ingawa utaratibu huu umepitwa na wakati kwasasa lkn zamani baadhi ya wazazi waliamua kuwatafutia wenza vijana wao Ili kuonyesha namna wanavyo wathamini, pia mwenza utakayetafutiwa Ilikuwa lzma atoke kijiji'wilaya au mkoa wenu ili Iwe rahisi kujua tamaduni na mila zenu...wazazi waliamini mwenza waliyekutafutia atakukumbusha kuwathamini na endapo mtapata mafanikio Itakuwa rahisi kukushauli mkawekeze nyumbani"
 
lengo lilikuwa zuri kwa kweli watoto siku hizi wengi hawajui mila za kwao wala lugha sanasana ni kiswahili au kiingereza inategemea mtoto anasoma wapi maadili yamepungua wengine wanageuza ndoa ni fashion ndio wanakaa miezi sita wanatengana
 
Wazazi wanafikia atua ya kutaka kutoa radhi kisa mtoto ataki kuoa.
 
Okya

Kuoa au kuolewa sio la lazima, ila kwa maadili yetu ya ki africa marriage ni jambo la heshima
 
Binafsi naona ni heshima tu iwapo wanandoa wenyewe wataiheshimu hiyo ndoa.

Huwezi kuwa kwenye ndoa na kunguru au kicheche wa kike/kiume , mtu asotimiza majukumu yake, asokuthamini wala kukujali na wewe eti uone unapata heshima ya kuoa/kuolewa.
 
Binafsi naona ni heshima tu iwapo wanandoa wenyewe wataiheshimu hiyo ndoa.

Huwezi kuwa kwenye ndoa na kunguru au kicheche wa kike/kiume , mtu asotimiza majukumu yake, asokuthamini wala kukujali na wewe eti uone unapata heshima ya kuoa/kuolewa.

kwa hiyo we unafikiri ndoa ipo kwa ajili ya heshima tu? No more eeeh manka!
 
Ukiona hivyo ujue hujatulia....
Kuoa si lazma ila km hujatulia ni bora uoe

Erickb52
Uoe ili umletee mapepe mkeo!!!!!!!!!?? Hapana kwa kweli, mimi I disagree. Kama hujatulia bora ubaki hivyo hivyo, zigo la familia au la walimwengu 😱hwell:!!
 
Back
Top Bottom