Kwani mahari gharama gani?

Kwani mahari gharama gani?

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Tuambizane basi posa/mahari huwa ni kiasi gasi kwa kabila yenu?maana suala la kuoa huwa huwezi kukwepa utaratibu wa kikabila.

Mnapokea viumbe wanaohema wangapi kama mbuzi, kuku, ng'ombe, kondoo? Kabila langu dume la ng'ombe mmoja (hata awe mdogo), ndama mmoja,kondoo wawili.

Inavyoonekana wasukuma na wamasai wana dau kubwa,sijui kama wahaya, wangoni, wasambaa, warangi, wambulu,wameru,wanyamwezi,waluguru, wazaramo, wachaga, wapare,wazanaki, wamakonde etc.

Naomba kujua kabila lenu mahari ni kiasi gani,je hao wanaotaka ng'ombe wengi msichana wao akikutana na kijana wa kizaramo(mfano),hiyo rules za mahari hawabadilishi?
 
Kwa upande wa Kiislamu ni suala la maridhiano tena hayatakiwi yawe ya gharama ,kuna jamaa alikwenda kuwowa ,akapigwa milioni nane ,jamaa alikuwa na noti ,akatoa harusi ikafanywa watu wakachawanyika ,sasa kisa ambacho ni true story wazee wa kike wakapanga safari kwenda kumuona mtoto wao ,walipofika wakasalimiana na mume wa mtoto wao,wakakaa hapo lakini hawakuona dalili ya mtoto wao ,ikabidi waulize ,fulani yupo wapi ,jamaa akajibu yupo juu hashuki chini ,wazazi wakasema tunataka kumuona,jamaa akaruka na kuwambia mnataka kumuona kwani wenu,huyu ni mke wangu na nyie hamna ruhusa wala si waruhusu ,haya tumekufanyeni nini akawambia nyie hamkuniozesha mtoto wenu mliniuzia na sasa ni mali yangu na kama mmekuja kumuona hilo halipo ondokeni nendeni kwenu huyu hamtamuona tena,basi mpaka leo jamaa hakumpeleka kwao wala hakuwaruhusu kumuona tena.

Hivyo mahari ni kitu kidogo sana kinachotakiwa ,na siku hizi si sana ukienda kuoa kukataliwa maana wanaume tumekuwa wachache sana ,utaona mtu anawatoto sita saba wa kike watupu ,na hajaenda hata mtu mmoja kupiga hodi kutaka kuoa na watoto wanapevuka ,hivyo uamuzi ni wako na wewe ndio mwenye mpini ,wakiweka hizo mila kwa miaka hii naona watachelewa sana.
 
1. Ng'ombe wanne, angslau wawili wanaotembea, wawili wanathaminishwa na unatoa cash.
2. Kitenge cha mama na bibi.
3. Blankets mbili, moja ya wazazi na nyingine babu na bibi.
4. Debe moja la pombe, kwa wale wasiotumia kilevi basi debe la sukari inasimama badala ya pombe.
5. Kondoo/mbuzi.

Japo siku hizi wanarahisisha kidogo...kila kitu wana round off Tu..mfano unaweza kuambiwa yote hayo lete 2,000,000tsh.
 
Kwa upande wa Kiislamu ni suala la maridhiano tena hayatakiwi yawe ya gharama ,kuna jamaa alikwenda kuwowa ,akapigwa milioni nane ,jamaa alikuwa na noti ,akatoa harusi ikafanywa watu wakachawanyika ,sasa kisa ambacho ni true story wazee wa kike wakapanga safari kwenda kumuona mtoto wao ,w
Kuna wazee wana masharti afadhali hao mkuu
 
1. Ng'ombe wanne, angslau wawili wanaotembea, wawili wanathaminishwa na unatoa cash.
2. Kitenge cha mama na bibi.
3. Blankets mbili, moja ya wazazi na nyingine babu na bibi.
4. Debe moja la pombe, kwa wale wasiotumia kilevi basi debe la sukari inasimama badala ya pombe.
5. Kondoo/mbuzi.

Japo siku hizi wanarahisisha kidogo...kila kitu wana round off Tu..mfano unaweza kuambiwa yote hayo lete 2,000,000tsh.

Mkuu we mwarusha nini,maana hayo masharti kama wao ingawa kuna process za kutambulishana nayo inataka hela aisee
 
Usiombe uoe uchagani au umasaini...utajuta kuzaliwa

Kwa gharama ya maisha haya ya sasa hivi ukioa mchaga wa mjini jiandae kutokwa na kitita kama cha milioni 3 kwenda juu...
 
Usiombe uoe uchagani au umasaini...utajuta kuzaliwa

Kwa gharama ya maisha haya ya sasa hivi ukioa mchaga wa mjini jiandae kutokwa na kitita kama cha milioni 3 kwenda juu...
Dah hiyo posa tu hapo bado harusi si kuuana huko
 
Ndio hivyo mkuu,

Mathalani kwa mila za uchagani, mwanaume anayeoa anagharimikia mahari pamoja na sherehe ndogo ya siku mahari inapokabidhiwa kwa wazazi wa binti...

Na wachaga wanavyopenda sherehe basi jiandae kulisha na kunywesha watu si chini ya 100...
Aiseee tutaishia kuwazalisha tuu, maana hawafikirii maisha ya wahusika baada ya sherehe wanataka kujinufaisha nafsi zao kupitia kwa wanao
 
Ndio hivyo mkuu,

Mathalani kwa mila za uchagani, mwanaume anayeoa anagharimikia mahari pamoja na sherehe ndogo ya siku mahari inapokabidhiwa kwa wazazi wa binti...

Na wachaga wanavyopenda sherehe basi jiandae kulisha na kunywesha watu si chini ya 100...
Hii kitu inaumiza we acha tu. Wanapiga hesabu ya msosi sahani sh. 20,000. Bia minimum 3 * 100, maji kilimanjaro, juice..dah!! Acha kabisa..! Ukitoka hapo hata sherehe huiwezi tena...na ukianza maisha ya ndoa mifuko imetoboka kabisa.
 
Posa hua tofaut na mahari. Posa ni kias kidogo.cha hela.ambacho hukiambatanisha na barua yako.kwenda kwa familia ya mke. Mahar inategemea sana kwetu hatuna mbwembwe yategemea na.mtu atataka nin ila kuna mkaja wa mama huu ndo mahela yote. Na mahari unaweza ukaelewana na.umuoae kua mim ntakua suala la mahar litakua deni au ntatoa nusu mahar yako nyingine ntakumaliza taratibu hapo anakua ashaingia jukum yy na mola wake akikutizimia sawa hakutimiza.deni hilo tena....
 
kwani we hujui kabila lenu mahari kiasi gani?

Im a Bemba bt ht hatufuati mambo ya kabila letu tunafanya kawaida tu. ....hakuna kiwango maalumu! ...bt mkaja wa mama...blanket cjui na jembe wanasemaga vinatolewa pia.
 
yategemea...kuna wengine wanafuata mila za kidini...mfano wachaga wengi ambao ni Waislam hutumia mila ya kiislam...Hata sh. 100 unaolewa nayo au ahadi yeyote au zawadi

Usiombe uoe uchagani au umasaini...utajuta kuzaliwa

Kwa gharama ya maisha haya ya sasa hivi ukioa mchaga wa mjini jiandae kutokwa na kitita kama cha milioni 3 kwenda juu...
 
ila wengi wanaokuwa wanaahidi kumalizia baadae huwa hawamalizii.. nshaona ndoa nyingi hadi watu wanaachana au kufa unakuta hajamalizia mahari ya mkewe.....

Posa hua tofaut na mahari. Posa ni kias kidogo.cha hela.ambacho hukiambatanisha na barua yako.kwenda kwa familia ya mke. Mahar inategemea sana kwetu hatuna mbwembwe yategemea na.mtu atataka nin ila kuna mkaja wa mama huu ndo mahela yote. Na mahari unaweza ukaelewana na.umuoae kua mim ntakua suala la mahar litakua deni au ntatoa nusu mahar yako nyingine ntakumaliza taratibu hapo anakua ashaingia jukum yy na mola wake akikutizimia sawa hakutimiza.deni hilo tena....
 
ila wengi wanaokuwa wanaahidi kumalizia baadae huwa hawamalizii.. nshaona ndoa nyingi hadi watu wanaachana au kufa unakuta hajamalizia mahari ya mkewe.....

Yeah ni kweli illuh wapo wanaofanya hivo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom