Kwani mahari gharama gani?

Kwani mahari gharama gani?

Sina uhakika kwa waumini wa Uislam, lakini kwa walio Wakristo wengi hufuata namna imani zao za kikabila zinavyoelekeza...

Ni mwendo wa kuchojolewa hela hadi ukija kuoa adabu unakuwa umeipata...

yategemea...kuna wengine wanafuata mila za kidini...mfano wachaga wengi ambao ni Waislam hutumia mila ya kiislam...Hata sh. 100 unaolewa nayo au ahadi yeyote au zawadi
 
wapare ni ng'ombe nne mahari na dume la tano la mjomba mtu kama binti amefundwa coz mjomba ndo anagharamia garama zote za binti kufundwa enzi hizo,mbuzi tatu za mama mtu,pimbe ya wazee ,sukari ya wamama, blanket la bibi mtu, jembe na shoka, baada ya hayo yote ukishaoa ukakaa na mkeo una tafuta siku unaleta mbuzi jike hapo ndo umekombos mkeo mazima hata ukimuacha lazima arudishe huyo mbuzi laa sivyo hata akiolewa akazaa ni mkeo na anayehitaji kumuoa lazima akurudishie hizo mahari zote. swali lingine kuhusu mahari za kipare uliza
 
Usiombe uoe uchagani au umasaini...utajuta kuzaliwa

Kwa gharama ya maisha haya ya sasa hivi ukioa mchaga wa mjini jiandae kutokwa na kitita kama cha milioni 3 kwenda juu...

Nawaachia mwanamke wao napanda gari nageuza
 
Natamani sana siku hyo ambayo nitaoa kabila ambalo linahtaj mahari kubwa

walahi hyo ndoa itashindikana nitawaachia mwanamke wao wamtafutie mume.. Mimi nitaendelea na maisha yangu pumbafu watu washafanya ndoa mradi wa kujikimu... Unamtoza mahari milion 3. 5. 8?
kumbe ndo mana wanawake.wananyanyaswa kwenye ndoa... Mana inakuwa kama ameuzwa
 
Kwa huku Lindi na mtwara baruavunaweza kuweka hata buku 20
mahari ni maridhiano tu.. Bila kujali ni mkristo au muislam

mahari inaweza kuwa 100000, 200000, 300000 kibingwaaa ingawa inaweza fika hata 1000000 la msingi ni makubaliano tu.. Na sijawahi sikia wazazi wanakataa binti asiolewe kwa misingi ya mahari

ndugu zetu wachaga na wasukuma wameshafanya mabinti zao miradi....
 
Mimi pia ni mfano hai....yamenikuta haya ya mahali kubwa nilipoenda kutoa posa kwa mchumba wangu na kukubaliwa..mambo yalikuwa hivi
1.Mahali-2000, 000/=
2.Ng'ombe watatu
3.Mkaja wa mama
4.Mashemeji-300000/=
5.Mbuzi wawili, ,mmoja kwa mjomba na mwingine shangazi
6.Kreti tatu za bia na tatu za soda
7.Blanketi mbili za babu na vitenge viwili vya bibi
8.Mikungu miwili ya ndizi
Majibu yalipoletwa na mshenga wangu nlichoka hoi....
 
yaani imenibidi nicheke hawa watu wanataka kufungua pub? hizo kreti za soda na bia Andfaru
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa maada murua kabisa. Kwetu ni ng'ombe watatu mmojawapo akiwa ni dume, blanket, kitenge na vihela kidogo wanaita 'unyago'. Lakini najiuliza mahari hasa ni nini? ina maana gani? na kwa nini itolewe. Mimi ni mkristo, katika maandiko inaelezwa katika kitabu cha Mwanzo (Biblia) 2.24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" sasa nashangaa kusikia habari ya mahari wakati anayetakiwa kuondoka ni mwanamume na si mwanamke!
 
Hiyo mahari uliyotaja wala hujakosea. Ila ka vile ng'ombe na mbuzi hawaletwi physically inabakia tamaa ya familia tu hapo. Kama ni watu wastaarabu unaweza kudaiwa sh elfu 50 jumla kwa maana ya ng'ombe mmoja tsh 7000 na mbuzi 3000. Na hizo hela sijui kirongoria mwana zikawa buku buku. Mbuzi ya mjomba, vitenge vya shangazi na blanket ndio vinakuwa physical.

Hivi ni mzazi gani saa hizi atadai mahari milioni moja? Labda kama mwanae ni kylinn na anaolewa na reggie.
wapare ni ng'ombe nne mahari na dume la tano la mjomba mtu kama binti amefundwa coz mjomba ndo anagharamia garama zote za binti kufundwa enzi hizo,mbuzi tatu za mama mtu,pimbe ya wazee ,sukari ya wamama, blanket la bibi mtu, jembe na shoka, baada ya hayo yote ukishaoa ukakaa na mkeo una tafuta siku unaleta mbuzi jike hapo ndo umekombos mkeo mazima hata ukimuacha lazima arudishe huyo mbuzi laa sivyo hata akiolewa akazaa ni mkeo na anayehitaji kumuoa lazima akurudishie hizo mahari zote. swali lingine kuhusu mahari za kipare uliza
 
Usiombe uoe uchagani au umasaini...utajuta kuzaliwa

Kwa gharama ya maisha haya ya sasa hivi ukioa mchaga wa mjini jiandae kutokwa na kitita kama cha milioni 3 kwenda juu...

Kumbe millioni 3 tu??
 
Wakati vijana wanaoa kwenye biblia tunasoma mzazi alituma mtu na ngamia na mifugo kibao. Was it isaka? Wakati anaoa mtu alitumwa na akaenda kusubiri kisimani. Yakobo akitaka kuoa alitumikia ndo akapewa mke manake hakuwa na mahari.

Mahari ni symbolic lakini zawadi lazma itolewe kama ishara kuwa mtoto wenu atatunzwa na hatolazwa njaa.
Nashukuru kwa maada murua kabisa. Kwetu ni ng'ombe watatu mmojawapo akiwa ni dume, blanket, kitenge na vihela kidogo wanaita 'unyago'. Lakini najiuliza mahari hasa ni nini? ina maana gani? na kwa nini itolewe. Mimi ni mkristo, katika maandiko inaelezwa katika kitabu cha Mwanzo (Biblia) 2.24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" sasa nashangaa kusikia habari ya mahari wakati anayetakiwa kuondoka ni mwanamume na si mwanamke!
 
Mimi pia ni mfano hai....yamenikuta haya ya mahali kubwa nilipoenda kutoa posa kwa mchumba wangu na kukubaliwa..mambo yalikuwa hivi
1.Mahali-2000, 000/=
2.Ng'ombe watatu
3.Mkaja wa mama
4.Mashemeji-300000/=
5.Mbuzi wawili, ,mmoja kwa mjomba na mwingine shangazi
6.Kreti tatu za bia na tatu za soda
7.Blanketi mbili za babu na vitenge viwili vya bibi
8.Mikungu miwili ya ndizi
Majibu yalipoletwa na mshenga wangu nlichoka hoi....

Dahhh hapo kaka hii ni business plan kabisaa ungeitumia kufanya biashara
 
Viol kikubwa mpatie binti mimba tuu..utampewa kwa mahari ndogo kama hawataki watabaki na huyu bint plus mimba
 
Last edited by a moderator:
Viol kikubwa mpatie binti mimba tuu..utampewa kwa mahari ndogo kama hawataki watabaki na huyu bint plus mimba

Ndo kilichobaki..ulijuaje kwanza? Mimi baada ya kupewa ule mchanganuo tu ahh nikapotezea mpk leo nakula kimya kimya mpk watanielewa tu!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimelipa kama ifuatavyo
Kifagio 200000
Kinyago 150000
Héla ya mama 500000
Fimbo ya baba 70000
Ng'ombe 4
Blanket 2na shuka 2.
Yaani nilikomaje!
Lakini nililipa na arusi tarehe 28/2/15
KARIBUNI SANA
 
Hiyo mahari uliyotaja wala hujakosea. Ila ka vile ng'ombe na mbuzi hawaletwi physically inabakia tamaa ya familia tu hapo. Kama ni watu wastaarabu unaweza kudaiwa sh elfu 50 jumla kwa maana ya ng'ombe mmoja tsh 7000 na mbuzi 3000. Na hizo hela sijui kirongoria mwana zikawa buku buku. Mbuzi ya mjomba, vitenge vya shangazi na blanket ndio vinakuwa physical.

Hivi ni mzazi gani saa hizi atadai mahari milioni moja? Labda kama mwanae ni kylinn na anaolewa na reggie.

Mmmh...ng'ombe athaminishwe kwa buku saba? Unafanya utani eeeh! Siku hizi wazee wamepata mwanya coz wanachaji cash...ng'ombe si chini ya laki mbili. Pamoja na mazagazaga mengine...hadi jasho la meno litakutoka. Tulienda huko gonja Rafiki yangu kapigwa 2m....acha kabisa!!!
 
Viol hujataja kabila langu mbona???mlengwa wa posa si mie au🙄🙄
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom