Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmmh...ng'ombe athaminishwe kwa buku saba? Unafanya utani eeeh! Siku hizi wazee wamepata mwanya coz wanachaji cash...ng'ombe si chini ya laki mbili. Pamoja na mazagazaga mengine...hadi jasho la meno litakutoka. Tulienda huko gonja Rafiki yangu kapigwa 2m....acha kabisa!!!
Hiyo mahari uliyotaja wala hujakosea. Ila ka vile ng'ombe na mbuzi hawaletwi physically inabakia tamaa ya familia tu hapo. Kama ni watu wastaarabu unaweza kudaiwa sh elfu 50 jumla kwa maana ya ng'ombe mmoja tsh 7000 na mbuzi 3000. Na hizo hela sijui kirongoria mwana zikawa buku buku. Mbuzi ya mjomba, vitenge vya shangazi na blanket ndio vinakuwa physical.
Hivi ni mzazi gani saa hizi atadai mahari milioni moja? Labda kama mwanae ni kylinn na anaolewa na reggie.
si nazungukia mbali unataka mpaka wajue nakuoa humu? BRENDA 18 bhana
Hujambo lakini?
hata sielewagi ngoja niulize
nyie kwenu itkua bure lol!!!
Nimerudia hiyo quote yangu ili uelewe tena ninachomaanisha. Kwa mzazi ambae anategemea kuwa huyo mkwewe ataendelea kuwa kama mwanae; na kuwajibika kuja na mafurushi ya vyakula wakati anamtembelea. Na hata kusaidia matibabu ama elimu za ndugu na majukumu ya kiafrika. Sidhani kama atadai mahari ya hela nyingi. Roho ya kimaskini tu hiyo, kijana wa watu anakaa nyumba ya kupanga halafu udai mahari milioni mbili?
Nikupe mfano tu, mie najua mtu alielipiwa mahari Tshs 1,000/= tu. Hiyo ilikuwa ng'ombe wanne na mbuzi tatu za wajomba. Hapo mbuzi ya mama ilipelekwa physically na mablanket na vitenge vitatu. Sio kila familia haijastaarabika kaka
Nimekupata sista..lakini pia mahari ya buku..mh! as a man, i wouldn't be happy either.
You wont kwa sababu unamthaminisha mwanamke kwa pesa yako. Binafsi mzee Mtambuzi angetaka mahari hata ya laki mbili tu kutoka kwa Paw ningemkasirikia na urafiki ungrisha ukabaki ubaba tu. Kuolewa sio kuhama nyumbani. Im still his daughter. Kuna shemeji yangu yeye wanae wote wanaolewa kwa mahari ya Tzs 100 tu. Alifariki mwaka jana, baada ya hapo bintie akiolewa hata mama yake alisema kauli ya baba still holds.
Lazma unakuwa offended ukikutana na wadada wanaoshare bills eh? Usipopigwa mizinga unahisi haupendwi?
Dada yangu aliolewa bila mahari, i didin't understand my dad then...! Niliona kama kamshusha thamani sista lakini baadae niligundua kitu. Hakutaka kumuuza binti yake, na vile ndio binti pekee kwenye familia....!
Sipendi mizinga, na nikiona ni mizinga (kwa maana ya kutapeliwa kimapenzi) isiyoisha huwa najitoa taratibu hadi atashangaa mwenyewe...lakini pia sipendi kutolewa out na mdada, kama sina mkwanja nitazuga hadi jioni ipite, japo pia naamini sharing is caring,. kwa hiyo unaona jinsi wengine tulivyo complicated katika mambo ya mahaba..!