Kwani mahari gharama gani?

Nimerudia hiyo quote yangu ili uelewe tena ninachomaanisha. Kwa mzazi ambae anategemea kuwa huyo mkwewe ataendelea kuwa kama mwanae; na kuwajibika kuja na mafurushi ya vyakula wakati anamtembelea. Na hata kusaidia matibabu ama elimu za ndugu na majukumu ya kiafrika. Sidhani kama atadai mahari ya hela nyingi. Roho ya kimaskini tu hiyo, kijana wa watu anakaa nyumba ya kupanga halafu udai mahari milioni mbili?

Nikupe mfano tu, mie najua mtu alielipiwa mahari Tshs 1,000/= tu. Hiyo ilikuwa ng'ombe wanne na mbuzi tatu za wajomba. Hapo mbuzi ya mama ilipelekwa physically na mablanket na vitenge vitatu. Sio kila familia haijastaarabika kaka
 

Nimekupata sista..lakini pia mahari ya buku..mh! as a man, i wouldn't be happy either.
 
You wont kwa sababu unamthaminisha mwanamke kwa pesa yako. Binafsi mzee Mtambuzi angetaka mahari hata ya laki mbili tu kutoka kwa Paw ningemkasirikia na urafiki ungrisha ukabaki ubaba tu. Kuolewa sio kuhama nyumbani. Im still his daughter. Kuna shemeji yangu yeye wanae wote wanaolewa kwa mahari ya Tzs 100 tu. Alifariki mwaka jana, baada ya hapo bintie akiolewa hata mama yake alisema kauli ya baba still holds.

Lazma unakuwa offended ukikutana na wadada wanaoshare bills eh? Usipopigwa mizinga unahisi haupendwi?
Nimekupata sista..lakini pia mahari ya buku..mh! as a man, i wouldn't be happy either.
 
Last edited by a moderator:

Dada yangu aliolewa bila mahari, i didin't understand my dad then...! Niliona kama kamshusha thamani sista lakini baadae niligundua kitu. Hakutaka kumuuza binti yake, na vile ndio binti pekee kwenye familia....!

Sipendi mizinga, na nikiona ni mizinga (kwa maana ya kutapeliwa kimapenzi) isiyoisha huwa najitoa taratibu hadi atashangaa mwenyewe...lakini pia sipendi kutolewa out na mdada, kama sina mkwanja nitazuga hadi jioni ipite, japo pia naamini sharing is caring,. kwa hiyo unaona jinsi wengine tulivyo complicated katika mambo ya mahaba..!
 
hahaha natamani kukuuliza umri wako kaka. Lakini umemuelewa baba sasa; najua hutajisikia vibaya kudaiwa mahari buku moja. Essence is; mahari ni kama bond na sio biashara. Ulishajiuliza hata mkipewa 5 mil kama mahari as a family kama itamaliza shida zenu zote ama vipi? Mahari ya hela ndogo ni kama token ama alama tu ya kuweka undugu.

In actual sense sie kwetu mahari haimalizwi. Na ukiwa na jambo la kuhitaji wazee unawaita kupunguza deni na ndio inafungua mazungumzo. Mahari ni kama utani na sio biashara kwa kweli
 
Kwetu mahari ni bure kama binti alipigwa mimba kabla ya kuchumbiwa
 
Mtathimin 2b wako utajua tu gharama yake...wakizdisha,we gomaaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…