kwani mfumo wa cash less unasua sua Tanzania

Lipa namba shida ni makato....
Binafsi lipa namba natumia kutoka NMB tu, maana NMB kwenda lipa namba yeyote hamna gharama yoyote na pia napenda kutrack matumizi yangu.
NMB kila nikilipia kitu nakatwa 10% ya muamala so kila tarehe ya mwisho wa mwenzi naangalia nimekatwa sh ngapi.
 
Naona wanabadilika taratibu na vijana ndo wanapenda lipa namba.


Juzijuzi nimefanya shoping maduka mawili tofauti maana duka la kwanza alikuwa na mzigo ila sikuuelewa nikachukua kidogo nikasogea duka la pili nikachukua mzigo.

Cha ajabu wa duka la kwanza nimelipa fresh kwa lipa namba na discout juu ila huku kwa kikongwe mshangazi kwanza nimekuta amepauka😀😀😀inaonekana siku nzima hajauza ila anamajivuno nikachuka mzigo mda wa kulipa analazimisha nikatoe hela kwa wakala ndo nimpe nikamchana laivu mbona huwa nafanya manunuzi kwa lipa namba na inakubali.

Huyu old skul aling'ang'ana na visingizio kibao mara lipa namba inasumbua mara hela inaweza isifike, nikaona isiwe kesi ngoja nifanye anavyotaka nisepe.Ila kibiashara hizi ng'ombe haziwezi kutengeneza loyal customers zaidi zaidi unakuta mtu miaka nenda rudi yupo vilevile biashara haikui na anaingia kundi la wachuuzi sugu🤝

Watu wengine hatuwezi kuzurura na madafu inakuwa kero kuzurura na cash nyingi isiyo na thamani wakati mpaka kuna migahawa unalipa kwa LIPA NAMBA.

📌📌📌Serikali ilipigie chapuo hili swala la kupunguza matumuzi ya cash na ikiweza ifanye system intergration kuweza kujikusanyia kodi bila TRA kuzungukia maduka na kutoa room ya kubargain kati yao na wafanyabiashara.Ambapo ndo milango ya rushwa inaanzua hapo.
 
NMB wapo vizuri, na mimi naitumia hiyo🤝
 
Mzee info track..tra na taskforce...mchinahapa bongo anataka Kash only
 
ushamba tu! mitozo kibao!
 
kwahiyo wewe kwa akili yako wakiacha kutoza hizo mia mia unahisi watafanya vipi maintainance ya hiyo mifumo.

Unahisi kampuni zitajiendeshaje labda??!!!
Hapo ndo penye kipengele cha kuhamishia watu huko kwenye cashless
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…