Kwani mkiachana lazima muwe maadui?

daxy Jr

Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
88
Reaction score
307


Muigizaji Vin Diesel aliachana na mpenzi wake wa miaka mitatu, lakini walipoachana, hakumtoa nje ya nyumba yake, aliogopa kwamba angeishi maisha ya chini, hivyo alimuachia nyumba yao na yeye akaenda kupanga nyumba nyingine.
Sio hivyo tu, aliendelea kulipia bili zote kwaajili yake na binti yao na alikataa kabisa chombo chochote cha habari kuingilia au kuchapisha chochote kuhusu kutengana kwao. Baada ya miaka 6 huyo ex wake alipata ajali na alihitaji kuongezewa damu. Vin Diesel aliwahi haraka hospitalini kwenda kumuongezea damu na alipopona wakarudiana!

𝗖𝗛𝗔 π—žπ—¨π—π—œπ—™π—¨π—‘π—­π—”: Nadhani tunatakiwa kuishi pamoja kwa upendo na unyenyekevu Ila ikitokea tumetengana basi isiwe vita, upendo na heshima ubaki kati yetu bila kujali kitakachotokea!
 
Mimi pia mke wangu alihamishiwa Dodoma kikazi, akawa analiwa na bosi wa wizara! Nikagundua tukaachana,

Lakini nyumbani nilipobaki na watoto chumba cha wageni ndio kilikuwa chake akija kusalimia watoto.

Akapata kesi kikazi mimi nilimchomoa kwenye msala kupitia kwa mjomba wangu aliye na nafasi kwenye vyombo vya sheria.

Sikukuu ya pasaka alikuja nyumbani tukafurahi kama hakuna jambo baya kati yetu.
Watoto wanaona sawa tu hawajui kinachoendelea.

Hatulali pamoja na hatushiriki ngono,ni marafiki sana,akiwa ana shida najiotoa kusaidia,hivyo hivyo nikiwa na shida namcheki.

Tunataniana pia ikibidi.

Pamoja na yaliyotokea bado ndiye mwanamke bora kabisa kuwahi kuwa naye , namuheshimu na kumpenda pia.
 
Ebanaeh Respect sana kwenu, wachache sana wanaweza kufanya hivyo!
 
Hiyo labda huko ulaya,huku kwetu ni full kurogana...
 
...Mh, Ngumu..!
 
Ni sawa na kutumia muwa Kama mkongojo, wakati una njaa....utaulaa tu[emoji23]
 
Bado kurudiana tuu hapo na wewe uwe kama jamaa juu hapo
 
Bado kurudiana tuu hapo na wewe uwe kama jamaa juu hapo
Hapana nimeshaharibika! Tukio hilo lilinitikisa sana...

Nimekuwa malaya mno mkuu[emoji1][emoji1] ,nina wanawake wengi mno hadi najionea huruma.

Kurudiana ni ngumu kwasasa namuona kama mama yangu mzazi ,sitaki hata kuona paja lake,sina mzuka nae kabisa.
 
Duuuh kweli hiyo ni hatari nyingine..
Yaani hata upashi kiporo kabisa anπŸ₯±πŸ₯±πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…