Mimi pia mke wangu alihamishiwa Dodoma kikazi, akawa analiwa na bosi wa wizara! Nikagundua tukaachana,
Lakini nyumbani nilipobaki na watoto chumba cha wageni ndio kilikuwa chake akija kusalimia watoto.
Akapata kesi kikazi mimi nilimchomoa kwenye msala kupitia kwa mjomba wangu aliye na nafasi kwenye vyombo vya sheria.
Sikukuu ya pasaka alikuja nyumbani tukafurahi kama hakuna jambo baya kati yetu.
Watoto wanaona sawa tu hawajui kinachoendelea.
Hatulali pamoja na hatushiriki ngono,ni marafiki sana,akiwa ana shida najiotoa kusaidia,hivyo hivyo nikiwa na shida namcheki.
Tunataniana pia ikibidi.
Pamoja na yaliyotokea bado ndiye mwanamke bora kabisa kuwahi kuwa naye , namuheshimu na kumpenda pia.