Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Swali kwa wapinzani.

Kwani mngegomea kushiriki haya maigizo ya uchaguzi wa 2020, mngepungukiwa na nini?

Na hivi mlivyoshiriki, mme-gain nini?

Mimi msimamo wangu uko wazi. Unajulikana.

Hakuna kushiriki chaguzi za maigizo ambazo mtu hauhitaji hata uwe genius kujua matokeo yake yatakuwaje.

Kushiriki chaguzi za hivyo, chaguzi za kutimiza wajibu tu, ni umajinuni.

Baadhi yenu mmetaja chaguzi za serikali za mitaa mwaka jana ambapo wapinzani walizisusia.

Kwanza, chaguzi za serikali za mitaa si sawa na uchaguzi mkuu.

Pili, migomo ya kushiriki chaguzi za maigizo ni lazima iwe endelevu.

Kama mwaka jana mligoma na CCM wakajipa ushindi wote, mwaka huu mmeshiriki na mmeambulia nini zaidi ya kipigo cha mbwa?

Zigomeeni hizo chaguzi. Wekeni mashinikizo mpaka zipatikane taasisi zilizo huru za kusimamia na kuendesha chaguzi.

La sivyo, mtaendelea kutegemea hisani ya CCM kupata ushindi.

Na siku mkikutana na jitu lenye roho mbaya, hata hizo nafasi chache mnazoshindaga, mtanyimwa.

Na jinsi mlivyo na vichwa vigumu, si ajabu mkaanza ule upuuzi wenu wa twende na Shangazi 2025.

Bure kabisa.
 
Unahitaji watu wenye values, wanaoelewa au waloumizwa sana kufanya hayo. Wanasiasa wa upinzani wanajua hili bado wanafikiri wana nafasi ya kuwaonesha hivyo.

2014 nikiwa na familia yangu walokuwa na vibe la upinzani niliwaambia CCM watawaletea Magufuli na mtampigia wenyewe kura.
CCM ni kokoro lenye samaki wa kila aina wengi wana adabu na unafiki wa kiafrika. Wengi wakihitaji kupendelewa na mfumo hata kama hawana wanachoifaidisha jamii. Na wako tayari kufanya chochote kubaki humo kulinda mali na vyeo walivyopata namna hiyo.

Upande mwingine, watanzania maskini wanaamini maisha yao ni Mungu anaamua na huku wakidondoshewa neema ndogo ndogo na hawa viongozi wanaoamini ni masihi. Ndio maana kila siku wanaomba barabara na wanasubiri waletewe maji.

Si haba ila mbegu ya upinzani inakua. Ilikuwa nadra 2015 kuona mikutano mikubwa ya upinzani huko vijijini. Nafikiri yakifanyika majumuisho ya kura walizopata wabunge wa upinzani ( hizi hizi zinazodaiwa kuchakachuliwa) kuna ongezeko asilimia tofauti 2015.
 
Walipogomea uchaguzi wa Serikali za mitaa walipata nini?

Anyway, Zanzibar walipogomea uchaguzi wa marudio kilitokea nini?
Kugomea kunatakiwa kuwe sustained.

Mambo ya kisiasa huwa hayana matokeo ya papo kwa papo.

Hata makaburu wa Afrika Kusini walipotengwa na jumuia ya kimataifa, hawakuacha ubaguzi wao siku ya kwanza.
 
Ushauri wako wa kwenye keyboard ni tofauti kabisa na hali halisi. Hata huyu diktekta uchwara alikuwa ame-set mambo ili wapinzani wagomee.

Alishaandaa na wapinzani bandia ili washiriki kwenye uchaguzi wa bandia na wapewe viti vichache. Hali ilikuja badilika pale alipokuja Lissu na kubadilisha upepo hivyo ikabidi technics zibadilike.

Kuhusu upinzani umepata nini kwa kushiriki uchaguzi well mimi nadhani watanzania wote na Magufuli mwenyewe wamejua hali halisi ya wananchi wanaionaje serikali ya Magufuli. Nadhani hata Magufuli mwenyewe ameshangaa jinsi alivyokataliwa pamoja na kudhani anapendwa sana.

Kwa kifupi hisia za wananchi zimejionyesha hadharani. Hii inaweza kutumia kama foundation ya kudai tume huru japo kwa namna navyowajua watanzania walivyo waoga kuwa-convince waingie barabarani ni ngumu mno.
 
Back
Top Bottom