Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Magufuli ana roho mbaya sijapata kuona. Walimwita JK dhaifu. Kweli Magufuli sasa atakuwa Rais wa maisha ila wananchi wajiandae kulia.
Ukiwa kama mtanzania mwenye upeo na mambo ya demokrasia na maendeleo hebu tuambie wewe unadhani njia gani zitumike kudai tume huru? Kwangu mimi nadhani wakati mzuri sana wa kudai tume huru ni kushiriki kwenye uchaguzi halafu matokeo yanapobakwa kama yalivyobakwa sasa hivi watu wanapata ''hasira na hamasa'' ya kuingia mitaani kudai tume huru. Kenya ilitokea hivi hivi. Kina Odinga wangekuwa wameamua kususia kama unavyo-suggest wewe mpaka leo pengine tusingekuwa na tume huru Kenya.
Tume huru mnayo tatizo mgombea wenu hakuwa na uwezo hata robo wa kupambana na MAGUFULI ,,kuweni wapole tu
 
Kwa Taarifa Yako unadhani kila aliekua anamshamgilia lissu ni mfuasi wake? Nadhani uwajui vyema watanzania😆 Yaan lissu alishangiliwa na watu 1000 wakati Mkoa huo una watu laki 9

Bro Nadhani mpaka sasa Nyangabu kawaambia maandamano ajenda yenu aina mvuto kwa Watanzania labda kwa wez na vibaka wanaotaka kupora maduka ya watu
Mkuu kama maandamano hayana mashiko kwa watanzania tambua kuwa hata kususa hakuna mashiko yoyote.....utasusa wewe wenzako watakula tu

Kama kweli upinzani ulishinda na ukaibiwa maana yake ni kwamba upinzani unawafuasi wengi kuweza kudai haki zao kwa maandamano
Lakini kama unaamini ccm ndio yenye wafuasi wengi basi upinzani hauna sababu ya kulalamika maana utakua umeshindwa kihalali

Binafsi naamini kususia ndio njia nyepesi zaidi ya kumpa uhalali ccm maana kuna akina shibuda kama 20 hivi watashiriki

Kama maandamano hayawezekani basi tuna safari ndefu sana
 
Tume huru mnayo tatizo mgombea wenu hakuwa na uwezo hata robo wa kupambana na MAGUFULI ,,kuweni wapole tu
1604242848410.png
 
Swali kwa wapinzani.

Kwani mngegomea kushiriki haya maigizo ya uchaguzi wa 2020, mngepungukiwa na nini?

Na hivi mlivyoshiriki, mme-gain nini?

Mimi msimamo wangu uko wazi. Unajulikana.

Hakuna kushiriki chaguzi za maigizo ambazo mtu hauhitaji hata uwe genius kujua matokeo yake yatakuwaje.

Kushiriki chaguzi za hivyo, chaguzi za kutimiza wajibu tu, ni umajinuni.

Baadhi yenu mmetaja chaguzi za serikali za mitaa mwaka jana ambapo wapinzani walizisusia.

Kwanza, chaguzi za serikali za mitaa si sawa na uchaguzi mkuu.

Pili, migomo ya kushiriki chaguzi za maigizo ni lazima iwe endelevu.

Kama mwaka jana mligoma na CCM wakajipa ushindi wote, mwaka huu mmeshiriki na mmeambulia nini zaidi ya kipigo cha mbwa?

Zigomeeni hizo chaguzi. Wekeni mashinikizo mpaka zipatikane taasisi zilizo huru za kusimamia na kuendesha chaguzi.

La sivyo, mtaendelea kutegemea hisani ya CCM kupata ushindi.

Na siku mkikutana na jitu lenye roho mbaya, hata hizo nafasi chache mnazoshindaga, mtanyimwa.

Na jinsi mlivyo na vichwa vigumu, si ajabu mkaanza ule upuuzi wenu wa twende na Shangazi 2025.

Bure kabisa.
Ha!

Kidogo kidogo mtakuja kunielewa tu.

Hata wale wenye vichwa vigumu kama mawe, nao ipo siku watanielewa tu.
 
Back
Top Bottom