Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Ndio na hao viongozi sio lazima wawe viongozi/wagombea wa upinzani.

Hapa hadi maisha yatupige vizuri ndio tutaelewa.Leo viongozi waupinzani wakigoma watu watapiga kura kama kawaida.
Haya.
 
Hapana!

Hakuna kilicho kipya!

Mazingira ya uchaguzi wa 2020 ndo yale yale ya 2015, 2010, 2005!

Tatizo ni usahaulifu wenu tu.
Kama ndio hivyo basi wapinzani wajitathimi upya, sio kwa sababu ya tume kutokuwa huru bali kwa anguko kubwa la kukataliwa na wapiga kura.
 
Haondoki huyu. Katiba inakwenda badilishwa. Kisingizio ni ili amalizie miradi yake.

Na pia atawaambia vibaraka wake kuwa usalama wake uko hatarini, so ni vyema aendelee kupata kinga ya uRais ili asidhuriwe.. Hatoki huyu madarakani ng’o. Na ikifika hapo, wote wanaomshabikia sasa ni bora waufyate, kila mtu aenjoy show.
 
Sasa ndugu unaamini kuwa kura hazikupigwa? Hujashuhudia wizi wa kura wa kutisha?? Mbona hao unaowakejeli wamepiga kura sana tu. Tatizo hulioni?
 
Reactions: BAK
Kwani kura za mbunge lazima ziwe sawa na kura za Rais?

Naweza kuwa mwana ACT, kura ya ubunge nikampigia mgombea wa CHADEMA, ya urais nikampa wa CCM.

Nyie watu mmechanganyikiwa!
Acha kutetea. Ukienda kupiga kura unapewa karatasi zote. Unless usipige huko basi zingehesabika zimeharibika. Haihitaji elimu kujua huo mchezo hapo.
 
Acha kutetea. Ukienda kupiga kura unapewa karatasi zote. Unless usipige huko basi zingehesabika zimeharibika. Haihitaji elimu kujua huo mchezo hapo.
Sasa hoja yako hapa ni nini?

Kwani ukipewa karatasi zote unalazimishwa kuzitumia zote?

Huna akili kabisa wewe!
 
Je watakubaliana wapinzani wa vyama vyote ?

Je ikiwa hawatokubaliana wapinzani wa vuama vyote alafu ikawa vyama viwili vya upinzani vimegoma na vyama vitatu vya upinzani vimekubali je unadhani mgomo huu utasaidia kitu wakati kuna wapinzani tayari wameshakubali ?
 
Basi acha waendelee kushiriki...

Who the hell cares?
 
Yaani katika siku zote na mada zako zote hii ndio nimeikubali , Mimi niliandika nyuzi zisizopungua nne humu kupinga upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana lakini bado hawakujifunza tu .
 
Wewe ndiye utakuwa msahaukifu. Yakiyitokea 2010 na 2015 ni wizi wa kura.

Safari hii kura hazijaibiwa Bali wamejitangazia matokeo kama wanavyotaka.

Kwa hiyo raisi ni nani? Una akili wewe?
 
Basi acha waendelee kushiriki...

Who the hell cares?
Me naona wakigoma alafu wengine wanafanya ni kazi bure tu.

Kuwepo kwa vyama vingi vya upinzani hiyo ni kuunda upinzani ndani ya upinzani,jambo ambalo linazidi kudhoofisha upinzani tu.
 
Yaani katika siku zote na mada zako zote hii ndio nimeikubali , Mimi niliandika nyuzi zisizopungua nne humu kupinga upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana lakini bado hawakujifunza tu .
Duh!

Yaani baada ya miaka 14 hapa JF na mabandiko zaidi ya 80K, ni mada yangu moja tu ndo umeikubali?

Ina maana huwa naandika pumba nyingi sana? 🤣🤣

Anywho, utani pembeni, hili suala nimeanza kulizungumzia kwa muda mrefu sana.

Bahati mbaya wahusika wenyewe ni watu wenye vichwa vigumu sana.

Waache tu waendelee kujipotezea muda, la, watakuwa ni wamendea ruzuku na si watu wa kusimamia kanuni.
 
Me naona wakigoma alafu wengine wanafanya ni kazi bure tu.

Kuwepo kwa vyama vingi vya upinzani hiyo ni kuunda upinzani ndani ya upinzani,jambo ambalo linazidi kudhoofisha upinzani tu.
Sawa.

Wafanye wanavyotaka basi.

Mimi kamwe sitojihangaisha na kupiga kura chini ya haya mazingira. Kamwe daima!

Nyie anzeni kujipanga kwa ajili ya 2025 🤣🤣.
 
Wapinzani Kuna wakati tunakwamishwa na viongozi wetu,dalili zote toka uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilikuwa zinaonyesha bila katiba mpya bila tume huru ya uchaguzi Basi hakuna uchaguzi huru na wa haki ungefanyika.Sasa Kwanini viongozi walijitoa uchaguzi serikali za Mitaa lkn uchaguzi mkuu hawakujitoa?Viongozi wetu Ni wabinafsi.
 
Japo unatumia maneno makali lkn Kuna ukweli ndani yake.Viongozi wetu Ni wabinafsi. Uchaguzi wa mwaka huu umekuja na Neema ndani yake, nadhani Sasa hivi watapigania kile walichotakiwa kupigania Sasa. Haiwezekani kushiriki uchaguzi utakaoshindwa,Ila unashiriki tu kwa vile unahisi unaweza pitishwa. Sasa hivi wote wamekatwa nadhani SoMo litaeleweka
 
Wewe ndiye utakuwa msahaukifu. Yakiyitokea 2010 na 2015 ni wizi wa kura.

Safari hii kura hazijaibiwa Bali wamejitangazia matokeo kama wanavyotaka.
Dalili zilionekana toka serikali za Mitaa pia kwenye uchukuaji fomu.Kwanini hawakujitoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…