Kwani mtoto chini ya mwezi mmoja huwa analia sana

Kwani mtoto chini ya mwezi mmoja huwa analia sana

Gas inatoka kwa njia ya kujamba, sijaelewa ni njia ipi mbadala ya kumtowa mtoto gesi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto anaponyonya maziwa ya mama huwa kwa kiwango kidogo huingiza na hewa wakati ananyonya...na ndiyo maana kwa binadamu kuna jinsi ya kumfundisha mama mzazi namna ya kumnyonyesha mtoto ili kwa mtoto anyonye maziwa vizuri na mengi kwa kadri anavyoweza na pia kupunguza kuingiza hewa tumboni.

Inashauri mara umalizapo kunyonyesha ni vizuri mama mzazi akamchukua mtoto na kumweka kifuani akiwa amesimama mama huyo mzazi na kuanza kumpiga piga kwa mkono mgongoni kwa mtoto ili kuitoa hewa toka tumboni kwa mtoto kwa njia ya mdomo.
 
Kuna daktari alituambia baada na sisi kusumbuliwa na mtoto kwa kilio

Kwanza namna ya kumyonyesha mtoto ule ukaaji wake watu wengi (wanawake) wanakosea nafikiri clinic wanafundisha hili

Pili mtoto anapo nyonya inatakiwa chuchu yote ya mama iweze kuwa ndani ya mdomo wa mtoto nafikiri anaponyonya asiingize hewa (gas)tumboni

Tatu , baada ya mtoto kushiba inatakiwa awekwe began kidogo , yaani tumbo la mtoto liwe begani ili kutoa hewa (gas)

Lakini pia inawezekana mtoto analia labda kuna shida kubwa ya ugonjwa japokuwa sehem kubwa ya vilio vya watoto ni njaa, muwasho hasa akijisaidia haja zote ni muhimu kumbadilishia pampers mara tu ajisaidiapo

Kwa Dar pia kuna Dokta wanajitahidi kujua magonjwa ya watoto

Dkt Massawe (kinondoni)
Dkt Ameer (Kariakoo karibu na fire stand)
 
huyo mtoto hashibi ,mpeni hata kaugali kidogo ahaa just kidding
ila ukweli analia njaa hashibi huyo dogo .mkamulie maziwa itakuwa hajui kuvuta vizuri
 
Kama swali liliulizwa sababu ni nyingi na zinatofautiana Mtoto na Mtoto.
Ila kuna zile ambazo zinajulikana kwa wengi.
1. Mtoto analia sababu ana njaa
2. Mtoto analia sababu anajisikia tu kulia.[emoji6]
3. Mtoto analia sababu anahitaji kubadilishwa nepi.
4. Mtoto analia sababu hajiskii vizuri, pengine anaumwa /maumivu
5. Mtoto analia sababu amechoka anahitaji Kulala.
6. Mtoto analia sababu anataka kubebwa.
7. Mtoto analia sababu anasikia joto au baridi.

Kama yote hayo hayamuhusu basi mwache alie akichoka atalala, jinsi anavyozidi kukua atapunguza nakuacha kabisa.
Hapa umenena vema.
 
Back
Top Bottom