Kwani ni lazima kila ibada atakayohudhuria Rais, azungumze?

Kwani ni lazima kila ibada atakayohudhuria Rais, azungumze?

Na haya mambo ya kuzigeuza madhabahu za kidini kuwa majukwaa ya kisiasa inanikera sana, na yamesababisha mzuka wangu kwa mambo ya kiroho ushuke.

Siasa zina majukwaa yake, Mahubiri/Mawaidha yana madhabahu zake. HAYA MAMBO YASICHANGANYWE!

Faustine Munishi, mwimbaji wa nyimbo za injili wa miaka ya 90' , alikuwa sahihi kuhusiana na jambo hili kwenye wimbo wa 'Siasa,Injili Pamoja' kwenye albamu ya 'Malebo'.
 
Acha upuuzi wewe...

Ina mana wageni wakija kwako huwa hawaongei??

Wanaondoka kama mabubu?

Kila kanisa Rais akienda anakua kama mgeni..lazima asalimie waumini.


Hata wageni wakija kwako lazima muongee story mbili tatu...kama mna muda na kinywaji juu...

Tatizo liko wapi??...au wivu wa kike
 
Wakuu Salamu,

Husika na kichwa cha uzi huu, napenda kuuliza hivi ni sheria za kanisa au nchi kwamba kwa kila ibada atakayo hudhuria rais wa nchi ni lazima apewe muda wa kuzungumza?

Maana naonaga hapa kwetu tu, kwani marais wa nchi zingine duniani huwa hawaendagi kwenye nyumba za ibada? Mbona hatusikii hotuba zao wakiwa makanisani au misikitini?

Au hawana dini?

Au ni lazima kila akienda church media zitangaze?
Anapenda kuonekana kwenye tv,pia ni mtakatifu asie na tone la dhambi yeyote,anapenda sana kusaidia masikini ndio mana humuona akigawa pesa za serikali kama za familia yake
 
Ana karibishwa wewe acha ushamba hata huko unaposema maraisi wao wakienda pahala lazma waongee sema huwezi jua sababu hukai huko zinalostiwa na local media tu...

Yule Rais wa nchi kupata ugeni wake sio jambo dogo iwe msibanj iwe wapi lazma atapewa kipaza asalimie watu
 
Inaonekana hufahamu nguvu ya viongozi wa mataifa. Viongozi wa mataifa wana mkono wa Mungu (soma kitabu cha Wafalme). Hivyo ni jambo jema sana kwa viongozi wa mataifa kuongea na watu wao na hata kuwatakia baraka wapatapo fursa, maana Mungu alisema nitawabariki utakaowabariki.
Labda viongozi wa zamani ndiyo walikuwa na mkono wa Mungu (kwa mujibu wa kitabu cha Wafalme).
Viongozi wa sasa wana Mungu/Miungu yao ambayo huwafanya wawe wana-act wanavyo-act.
 
Huwa wanatuhubiria nyumba za ibada zisitumike kisias lakini huyu mtu kila akienda kusali lazima ahutubie alete siasa....najiuliza wangefanya upande wa pili sijui ingekuaje hilo povu.
 
Naamini anaombwa atoe salamu. Huwa kuna kipindi cha matangazo na hata kukaribisha wageni kama wapo kanisani. Nini kimekuudhi kwa hili? Kimekuuma kitu gani?

Muwe na sababu za msingi za kukosoa, sio kukosoa tu hivihivi. Mimi huwa namkosoa JPM kwa kuminya demokrasia, lakini anapofanya jambo zuri namsifia. Na akifanya jambo halina sababu ya kuzungumzia, kama kuongea kanisani, nakaa kimya.

Kwani huna cha maana zaidi cha kuandika?
Kwani uzi unamhusu JPM au umekurupuka tuu?
 
Wakuu Salamu,

Husika na kichwa cha uzi huu, napenda kuuliza hivi ni sheria za kanisa au nchi kwamba kwa kila ibada atakayo hudhuria rais wa nchi ni lazima apewe muda wa kuzungumza?

Maana naonaga hapa kwetu tu, kwani marais wa nchi zingine duniani huwa hawaendagi kwenye nyumba za ibada? Mbona hatusikii hotuba zao wakiwa makanisani au misikitini?

Au hawana dini?

Au ni lazima kila akienda church media zitangaze?
Kwani kuna ubaya akihutubia?,Vipi unakereka akihutubia?.
 
Wakuu Salamu,

Husika na kichwa cha uzi huu, napenda kuuliza hivi ni sheria za kanisa au nchi kwamba kwa kila ibada atakayo hudhuria rais wa nchi ni lazima apewe muda wa kuzungumza?

Maana naonaga hapa kwetu tu, kwani marais wa nchi zingine duniani huwa hawaendagi kwenye nyumba za ibada? Mbona hatusikii hotuba zao wakiwa makanisani au misikitini?

Au hawana dini?

Au ni lazima kila akienda church media zitangaze?
Yupo addicted na camera na mic(hasa camera) Kama mwanae Bashite hivyo solution ni kumuweka mbali na hivyo vitu.
 
Aliwahi kusema anataka kuwa kiongozi wa malaika. Watu tukawaza huenda anaamini yeye ni mungu-mtu fulani.
Sasa kwa style hiyo, lazima alazimishe kupewa madhabahu za kidini ili aongee.
Sio kiongozi wa malaika tena,cheo chake kwa Sasa ni Yesu wa ccm
 
Wakuu Salamu,

Husika na kichwa cha uzi huu, napenda kuuliza hivi ni sheria za kanisa au nchi kwamba kwa kila ibada atakayo hudhuria rais wa nchi ni lazima apewe muda wa kuzungumza?

Maana naonaga hapa kwetu tu, kwani marais wa nchi zingine duniani huwa hawaendagi kwenye nyumba za ibada? Mbona hatusikii hotuba zao wakiwa makanisani au misikitini?

Au hawana dini?

Au ni lazima kila akienda church media zitangaze?
Magufuli ana mashauzi tu.

Kwa wadogo wasiojua historia, Mwalimu Nyerere alikuwa anasali sana. Si kila Jumapili, kika siku.

Alikuwa anatoka Msasani, anapitia St. Peters Oysterbay karibu kila siku akiwa Dar.

Na Jumapili pia alisali.

Lakini tulikuwa hatumuoni kujipeleka peleka mbele kanisani kuongea.

Alijua kitu kinaitwa "separation of Church and State".

Rais Benjamin Mkapa yeye kanisa lake lilikuwa Palm Beach Hotel na sakramenti yake ilikuwa Scotch Whisky.

Lakini kwa heshima ya urais, alivyopata kuwa rais tukaanza kumuona kanisani St. Immaculata Upanga.

Lakini hakuwa mtu wa kujipeleka mbele kanisani. Alikuwa anakaa na waumini, anasali, anajikata zake.

Hawa marais wasomi walijua kitu kinaitwa "separation of church and state".

Sasa kaja huyu country bumpkin, kika akienda kanisani anataka kuongea.

Inaharibu sana "separationnof church and state". Rais anakuwa kama kasisi. Mpaka wananchi wa imani nyingine wanajiona rais ni wa upande wa pili. Rais anatumia mimbari ya nyumba za dini kujipaisha kisiasa. Wakfu wa nyumba za dini unachafuliwa na siasa.

Anaharibu sana taratibu nzuri za marais waliopita ambao walijua kutwnganisha vizuri kazi zao za dini na siasa.
 
Back
Top Bottom