Kwani ni lazima wanawake wadeke?

Kwani ni lazima wanawake wadeke?

Mtu kila weekend anaumwa Mara anataka umshikilie anapokwenda chooni, umpikie chakula kwa sababu anadai anasikia kizunguzungu, umwogeshe, umfulie Ch&@i yake, ukitoka kidogo mesegi kibao kwamba umemtelekeza. sasa Ashadii anasema ni kutaka attention mimi kwa uelewa wangu lengo la kudeka ndiyo hilo la kuvuta attention.

Sasa na kulia ndiyo huko tena. Jambo dogo chozi hilo.... Nakubaliana na Tz1 kwamba kama kudeka basi wanawake dekeni wiki mbili baada ya hapo mnakera jamani. Maana wakati mwingine mnaongea au unamwelekeza jambo la maana yeye ghafla anabadili sauti na kuanza kuongea kama mtoto mdogo. Aaargh! Inakera bana.

teh teh teh teh kama mtoto.
 
Aisee, mimi huwa ninapenda mwanamke anayedeka, yaani mpaka raha. Anakuwa kama mtoto vile. Napenda awe anadeka kwangu tu.
 
Aisee, mimi huwa ninapenda mwanamke anayedeka, yaani mpaka raha. Anakuwa kama mtoto vile. Napenda awe anadeka kwangu tu.
kweli bwana inapendeza somtmz mwanamke wako anapodeka, lakini isiwe ndiyo formula ya maisha yenu!! Na siyo hata sehemu inapohitajika seriousness.
 
Sio wakali bana. Ndugu watajazanaje mpaka mke ajifanye mgonjwa? Kama wana kwao, wakae huko huko!
Si unajua uafrika ndugu ni baraka. wana kwao lakini kuja kwako kwa muda tuu ndiyo u-act unaumwa? Mbona ndugu zenu wakija mnawafanyia na sherehe?
 
kweli bwana inapendeza somtmz mwanamke wako anapodeka, lakini isiwe ndiyo formula ya maisha yenu!! Na siyo hata sehemu inapohitajika seriousness.

kweli kabisa ndugu yangu. Kudeka kwa mwanamke kuna raha yake, cha msingi adeke katika mazingira mazuri, kama ulivyosema, sio katika mazingira ya seriousness
 
kuna wanawake akiona ndugu wa mume wamejaa kwenye nyumba,ataumwa weeh mpaka wapungue....lol

No kaka, Kudeka anakosema ni kwa mwanaume yaani mmewe sio kwa ndugu, mawifi wengine ukiwadekea mbona balaa, Na huyo atakayeumwa mbele ya ndugu ili wapungue basi hao ndugu wamemfanya mwanamke ni kibalaka humo ndani kila kitu afanye yeye ndio sababu njia ya kujikomboa anaona bora aumwe mpaka hao ndugu wapungue.
 
kudeka raha bwana mimi nadeka humuhumu
 
kudeka raha bwana mimi nadeka humuhumu
Teh! Teh! Teh! Teh! Kweli bwana nilikuona ulivyodeka na kutishia kuondoka mpaka watu wote tukaacha kazi zetu na kukubembeleza. lakini siyo kwenye kila ishu binti mzuri, mwisho wa siku tutakuchukia.
 
teh! Teh! Teh! Teh! Kweli bwana nilikuona ulivyodeka na kutishia kuondoka mpaka watu wote tukaacha kazi zetu na kukubembeleza. Lakini siyo kwenye kila ishu binti mzuri, mwisho wa siku tutakuchukia.
nilitukanwa bwana vibaya mno hata usinikumbushe nitaondoka tena
 
Jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia kwamba wanawake kuumwaumwa ni aina yao ya kudeka ili wajue kama mwanaume unampenda kweli au magumashi. Pia siyo kila kilio cha mwanamke ni kilio cha kweli.

Hata mimi naamini kwamba wakati mwingine wanawake "wanaumwa" ili wawe karibu na wapenzi wao.Au wanalia ili wabembelezwe.

Sasa kwani ni lazima wanawake wadeke ndiyo wajue wanapendwa kwa kubembelezwa?

unadhani ni wanawake tu wanajua kudeka?kuna wanaume wanadekaga kwa wake/wapenzi wao mpaka kero yani.sababu za mijimaume kudekea wake/wapenzi ni izo izo za wanawake.
 
sio lazima wadeke....
ukimdekeza atadeka, usipomdekeza hatodeka!!
 
Back
Top Bottom