Kwani polisi wanafeli wapi mpaka tuanze kulipa hela ya sungu sungu

Kwani polisi wanafeli wapi mpaka tuanze kulipa hela ya sungu sungu

Pentamycin

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2023
Posts
210
Reaction score
281
Nagongewa mlango kufungua wadau wanataka Hela ya ulinzi shirikidhi a.k.a sungusungu,na juzi wakati narudi usiku waliwweka limiti ya mtu kutembea usiku,hii SI sawa ,polisi wafanye majukumu Yao, ninalipa Kodi, haiwezekani kwenye nchi ambayo tunalipa Kodi zetu washindwe kudumisha usalama wetu ,sitetei wizi ila ni wajibu wa wanaotumia kodi zetu kutulinda
 
Kataa kulipa buku ya ulinzi subiri uje kulipa fine mahakamani ya shilling laki tatu au uende jela.

Kupanga ni kuchaguwa, ujuwaji uliponza wengi.
 
Polisi hawawezi wakakaa kila angle kuwalinda patrol ndio wanafanya Ila polisi ni wachache mno hawawezi wakachukua kazi ya sungusungu na sungusungu haikuanza Jana Wala Juzi imeanza tangu wewe hujazaliwa
 
Sheria inasemaje kuhusu hili? Mbona maeneo mengine hao watu hawapo? Kama kuna kifungu naomba share hapa tukione.
Wewe fuata utaratibu uliowekwa sio kujifanya kuhoji sheria inasemaje wakati wenzako wanafuatwa utaratibu, watu km nyinyi ndio mnashirikiana na wahalifu mnahamasisha watu wasichangie ulinzi shirikishi kisha wakiacha mnawavamia na mapanga na kuanza kuwafanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria,
 
Kwani Mkuu umesahau kwamba Sera ya Nchi inasema jukumu la ulinzi na usalama ni LA kila Mtanzania Linda nchi yako Acha kujishaua.

Tulibana matumizi ili tuwe na Walioajiriwa Kwa kazi hiyo hivyo pengo lake lazima tulizibe.
 
Wewe fuata utaratibu uliowekwa sio kujifanya kuhoji sheria inasemaje wakati wenzako wanafuatwa utaratibu, watu km nyinyi ndio mnashirikiana na wahalifu mnahamasisha watu wasichangie ulinzi shirikishi kisha wakiacha mnawavamia na mapanga na kuanza kuwafanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria,
DIvision four ndo waombe u polisi

"Simbachawene"

Badala ya kujibu hoja ni sheria ipi wewe unakuja na porojo, jambo likifanywa na watu wengi halafu ni kosa, halihalishi ubaya wake.
 
Sheria inasemaje kuhusu hili? Mbona maeneo mengine hao watu hawapo? Kama kuna kifungu naomba share hapa tukione.
Sungusungu ni mradi wa upigaji kuanzia kwa mwenyekiti wa mtaa na kwa wajumbe,,

Ukitaka kuthibitisha hilo uliza mapato na mgawanyo wa pesa zinazochangwa na wanainchi,,

Utapewa Jina la ukorofi unataka kuvuruga ulinzi.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom