Kwani Rais huoni hili tatizo la CWT?

Kwani Rais huoni hili tatizo la CWT?

Doto12

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
640
Reaction score
1,141
i) Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?

ii) Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?

iii) Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.

Mbona mamlaka yako yanakuruhusu kuingilia hapa kwani huoni au hawakuambii watu wako
 
Ahh CWT Tena? Walimu wenyewe hampendani. Wakati ule mfuko umenona kina mwalimu alawi wakajichotea mahela wakajenga mapartment kibaha na kugombea. Hata awekwe Nani hapo ataiba tu.

Jipangeni, boresheni mfuko,muweke option ya kuwa mnakopeshana,aidha nyumba, gari au fedha taslimu
Lasivyo hela zenu zitaendelea kuliwa na wajanja, Simba na Yanga.
 
Ni kweli na ndio maana kuna mamlaka.

Mwl akishapata diploma ana mdharau wa certificate

Akipata degree moja, atamdharau wa chini, kisifasifa akichukua master(maana haitambuliki) anadharau na kama akiteuliwa kuwa afisa elimu wilaya, kata dharau na kuwato.mba walimu wa kike, hii ndio balaa.

Tena akipewa posho ya madaraka wenyewe wanaziita stahiki... ndio kabsaaaaa kuna mmoja mjinga sana wa halmashauri moja mkoa wa na wilaya kanda ya mashariki moro- pwani na dsm.

Degree ya 2 au Master ni afadhali waitambue kwenye ualimu au waiondoe kabsa
 
Vyama vya wafanyakazi ni legacy ya sera ya ujamaa. Vipo kuwanufaisha viongozi wa vyama hivyo na ccm ili waweze kucontrol kirahisi wafanyakazi lakini kamwe havimsaidii mtumishi.

Sheria inapaswa kubadilishwa na vyama hivi viwe option mtu kujiunga badala ya kulazimishwa kwa mujibu wa sheria
 
Vyama vya wafanyakazi ni takwa la Dunia sio takwa la Serikali, ILO CONVENTION 87,97
 
rais aingilie kati,usajili wa wanachama CWT uanze upya,cwt akufe kifo cha mende,nachukia CWT mimi
 
i) Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?

ii) Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?

iii) Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.

Mbona mamlaka yako yanakuruhusu kuingilia hapa kwani huoni au hawakuambii watu wako
Hivyo si ni Vyama vyenu nyie walimu ndio mchukue hatua au?
 
Vyama vya wafanyakazi ni takwa la Dunia sio takwa la Serikali, ILO CONVENTION 87,97
Takwa la dunia ni uwepo wa nyama, membership ni voluntary......

Watu wana ujinga wa kufikiria kufukuzwa kazi na kwa hivyo kujiunga na vyama wanaiona kama insurance policy kwamba ukipata matatizo chama kitakutetea...yaani unaanza kazi na kuwazia matatizo, huo ni ujinga!
 
Ahh CWT Tena? Walimu wenyewe hampendani. Wakati ule mfuko umenona kina mwalimu alawi wakajichotea mahela wakajenga mapartment kibaha na kugombea. Hata awekwe Nani hapo ataiba tu.

Jipangeni, boresheni mfuko,muweke option ya kuwa mnakopeshana,aidha nyumba, gari au fedha taslimu
Lasivyo hela zenu zitaendelea kuliwa na wajanja, Simba na Yanga.
Majaliwa mwenyewe alikuwa CWT akachomokea huko
 
Takwa la dunia ni uwepo wa nyama, membership ni voluntary......

Watu wana ujinga wa kufikiria kufukuzwa kazi na kwa hivyo kujiunga na vyama wanaiona kama insurance policy kwamba ukipata matatizo chama kitakutetea...yaani unaanza kazi na kuwazia matatizo, huo ni ujinga!
Hakika umenena ni upumbavu tupu, TUCTA wananenepa tu town kwa pesa za wajinga kama hawa
 
Jibu rahisi ni kwamba tatizo analiona na analijua, kwa sababu cwt ilivyo ni makisudio ya ccm na serikali. Yaani kusiwe na chama cha wafanyakazi chenye nguvu ili kisisumbue wakubwa kwenye ulaji . Nani anataka chama cha walimu chenye kuleta usumbufu serikalini?
 
"Serikali" ni sehemu ya tatizo hili ndio maana haliwezi kuapata ufumbuzi mapema.
Hili halina tofauti na KADCO ilivyokuwa kwani mkono wa ulaji ndio ilikuwa kikwazo kuiondoa
 
Kwanini asione wakati serekali ni sehemu ya tatizo.Hivyo vyama ni miradi ya watu na chama kilichoko madarakani ni mnufaika mkubwa.Kwahiyo kamwe usitegemee jambo la tofauti.
 
Vyama vya wafanyakazi ni legacy ya sera ya ujamaa. Vipo kuwanufaisha viongozi wa vyama hivyo na ccm ili waweze kucontrol kirahisi wafanyakazi lakini kamwe havimsaidii mtumishi.

Sheria inapaswa kubadilishwa na vyama hivi viwe option mtu kujiunga badala ya kulazimishwa kwa mujibu wa sheria
Poor Dad Rich Dad kitabu kizuri sana
 
Mh Rais hiyo tarehe 13 desemba ikimpendeza atoe tamko la kwamba kila mwl achague chama cha kumtetea kati ya viwili au vitatu vilivyopo kwa mapenzi yake mwenyewe pasipo kulazimishwa .Hiyo fomu namba 15( TUF 15) iliyojazwa na mwl husika iwekwe kwenye mfumo wa mishahara (HCMIS) Kama sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 inavyotamka.Napendekeza hivyo kwa sababu Malalamiko ya walimu wengi karibu 95 % kuhusu Cwt ni kukatwa mishahara yao pasipo ridhaa yao kwa sababu hawajawahi kujiunga na kujaza fomu hiyo Tuf 15 inayotoa idhini kwa mwajiri kukata mshahara wa mtumishi kisheria . Serikali ikiachia ujambazi huu uendelee itadhoofisha utendaji kazi wa walimu nchini kwa maslahi ya kikundi cha hao viongozi wa siwitiii walioamua kusaka ngawila liwe jua iwe mvua.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom