Kwa kifupi model ambayo nina uzoefu nayo kidogo ni hizi za 2005 - 2010. Zina specifications tofauti ila nitakuambia machache nayojua
Advantages
1. Ni gari ngumu, himilivu kuanzia body mpaka engine (uzoefu wangu engine za petrol J20 ya 2000cx na J24 ya 2400cc
2. Ni gari inayotulia barabarani, nzito, ina steering nzuri (precise) na haikupi mawazo ya uoga ukiie desha
3. Spare zipo na ni rahisi kufanya service
Disadvantages
1. Si gari yenye nguvu/kasi sana (hizi zenye cc2000)
na zile za 2400cc zina nguvu ila fuel consumption si nzuri sana kwa sababu ni 4 speed automatic.
Manual ni 5 speed na zinaweza zikakupa perfomance nzuri zaidi
2. Si gari comfortable sana (lakini si mbaya hata kidogo). Wind noise na engine noise zinaingia ndani kwa urahisi kiasi.
Nikikumbuka nyingine nitaongezea. Kama mtu una 25-28m na unaka SUV ambayo si pasua kichwa, imara na madhubuti, hii si chaguo baya hata kidogo