Mufti kuku The Infinity
JF-Expert Member
- Sep 21, 2019
- 6,053
- 10,032
jiulize utaifanyia nn nchi na sio ikufanyie nini?
so kapande ww miti
so kapande ww miti
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fikiria embe dodo au fenesi limemuangukia mtu au limeangukia kioo cha mbele cha gari!
Fuatilia miembe inavyo katika matawi au inavyo anguka ovyo wakati wa vuli au masika.
Fikiria miembe inavyo kuwa na matawi mapana sana na kuingia barabarani.
Fikiria tabia ya hatari ya makuti ya mnazi kupeperuka toka kwenye mti na kupiga vioo vya magari.
Labda tupande matunda jamii ya michungwa.
Kumbuka miti yenye mizizi mirefu kama mikungu jinsi ilivyo kuwa inaharibu lami au kingo za barabara au mitaro kule Posta na Oyesterbay...
Hata hivyo umeleta wazo zuri.
Mbali na barabara?!!Jiongeze mkuu hiyo miti ya matunda itapandwa pembeni sana mwa barabara.. Alafu ikumbukwe kitu njaa haswa kipindi cha itakuwa historia
Upumbavu wa kusingizia wakoloni utawaisha lini ninyi waafrika? TABORA ILE MIEMBE Pembezon mwa barabara imekatwa miaka ya hivi karibuni baada ya kuonekana ina ingia barabarani na pia inaharibu barabara kutokana na mizizi mirefu.Huu ujinga wa kupanda ma miti yasiyo na faida uliletwa na wakoloni kipindi hicho wanatutawala lengo likiwa ni kutengeneza utegemezi kwa maana watu wakose chakula na wakafanye kazi kwenye mashamba yao
Wakoloni waligundua matunda yaliyopo kwenye mazingira yanasaidia sana kukinga njaa na pia yanapunguza matumizi makubwa ya vile vyakula vya msingi kama mahindi, mchele na ndizi
Kwa hivyo ikafanyika kampeni ya kundoa miti ya matunda kwenye mazingira
Ukiacha sababu za kihandisi za kutopanda miti ya matunda barabarani hasa barabara kuu, utaona hata kwenye ma taasisi wamepanda miti ya hovyo isiyokua na faida yoyote mfano kwenye viunga vya shule za msingi secondary na vyuo
Hata kwa baadhi ya watu unaenda kwake unakuta kapanda ma miti ya ovyo ovyo lakini hana mti hata mmoja wa matunda.
Kule Isimani Iringa walikua na kampeni ya kupanda miti ili kutunza mazingira, hiyo aina ya miti waliyopanda sasa ni kituko tupu, mpaka unajiuliza hawa watu wanatumka akili au makalio kufikiri.
Yapandwe hata mapera,makoma manga and the like.Wanyama,ndege na watoto wetu watajilia matunda ya bure na kudumisha Afya zao.Wanataka ipanwe mipalachichi, michungwa au mikungu nk, matunda yasiyoweza kuleta madhara.
Msimu wa mavuno ukifika kuwepo na wakala wa mavuno.
Yapandwe hata mapera,makoma manga and the like.Wanyama,ndege na watoto wetu watajilia matunda ya bure na kudumisha Afya zao.
Tulipokuwa wadogo huko kigoma barabara ilijaa miti ya miembe na mizambarau tulifaidi sana matunda na tuliboresha afya zetu.Siku hizi matunda mpaka uende sokoni, hiii dhuluma kwa watoto wetu.