Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi wapande hata mipela au michungwa na hiyo mikubwa ya miembe ipandwe highway..Mbali na barabara?!!
Tanzania hasa kwenye miji na majiji yetu kuna nafasi hiyo?
Kupata hiyo nafasi ndogo tu imelazimu kuvunja nyumba za watu.
Kumbuka pia kuna eneo la kuweka miundombinu mingine pembeni ya barabara ambayo haiwezi kuwekea sehemu yenye hiyo miti kikubwa ya matunda.
Wakiwavunjia nyumba wapande hayo matunda utakuwa kulaumu hapa wanaongea watu.
Sam Nujoma Road ilipopanuliwa na kuachwa nafasi kubwa katikati watu walilalamika mbona wamevunjia watu, wamechukua nafasi kubwa na kuiacha katikati?
Leo faida yake imeonekana kwenye Ubungo Interchange/flyover toka mataa kuelekea Mwenge.
Akina Kakobe walipiga kelele mradi muhimu wa umeme grid ya taifa ulipopitishwa karibu na kanisa lake, leo uwaambie wavunjiwe ili ipandwe miembe kupendezesha jiji na watu wafaidi matunda?!!!
Natamani kama Tanroads wangesoma hii post!
Tukipanda miti ya matunda barabarani halafu matunda yakaiva itakua vifo kwa watoto wetu.Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpaka maeneo ya Osterbay hadi baadhi sehemu za Masaki.
Ukienda Morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli.
Mfano nimeenda nchi za kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani hata minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti, langu wazo tu asanteni.
Nimeandika hapo juu,tulipokuwa watoto huko barabara ya kigoma ujiji tulikuwa tunashinda kuangua maembe na hakuna kilichotutokea wala gari lililovunjika kioo kwa kudondokewa na embe.Wewe unataka balaa zingine zitokee!!, haitakuwa sahihi kwa matunda ya aina hiyo kuachwa watoto wavune holela bila nidhamu fulani, katika hali hiyo ndiyo maana wahusika wameamua kupanda miti isiyo na matunda ya kula.
Nimeandika hapo juu,tulipokuwa watoto huko barabara ya kigoma ujiji tulikuwa tunashinda kuangua maembe na hakuna kilichotutokea wala gari lililovunjika kioo kwa kudondokewa na embe.
Hats hapo mwanga kulikuwa na miembe, lubengela kulikuwa kuna miembe.Kama umezaliwa juzi huwezi jua hilo asilimia kubwa miembe hip imekatwa.Tulikuwa tunashinda ktk miembe tukipopoa maembe hio 80's inawezekana ulikuwa protini ya maharage au dagaa mim nilikuwa nshakuwa damu na nimeikuta hio miembe.kuna shule inaitwa muungano opposite kulikuwa na miembe na hata bembea zikuwa zinafungwa maeneo hayo Siku za sikukuu. Sizungumzi hadithi bali kitu nilichokiona.
Nakuongezea na hii,Tabora kuna Barbara nadhani ya unyanyembe ilikuwa miembe pande zote mpaka katikati kulikuwa na kivuli. Uliza wazee wakujuze.
Kigoma kuna mahala paliitwa mwembe togwa, huo mwembe ulikuwa barabarani kabisa. Nimehama Kigoma 1987 lakini bado nakumbuka,kanusha kama hakukuwa mwembe togwa barabarani
Unaishi mji gani? Huku mji nilipo mimi huruhusiwi kufanya modification ya aina yoyote baada ya ukuta wa nyumba yako au geti bila kibali cha mamlaka husika, mfano labda nje ya geti lako yanajaa maji mvua ikinyesha huruhusiwi hata kujaza kizege ili kuchepusha maji, etc sembuse kwenda kujitolea kupanda miti barabarani? Huo mnyororo wa vibali utakaokutana nao utarudi kwako kupika uji unywe na familia.Hii ishu inatakiwa watu wajitolee tu, kwa maafisa wetu wa serikali haitokuja kutokea labda vizazi vijavyo sio hawa meneja vitambi.
Kuna yule injinia walio kuwa wanarekebisha daraja la Dom mpaka Magufuli akampa kubwa jinsi alivyofuga kitambi,sasa utarajie ubunifu kwa injinia kama Huyo hata balanced diet tu imemshinda, akupandie wewe matunda.
Dini ya kiislamu imeagiza mtu atakaepanda matunda atapata thawabu sawa na mlaji wa hilo tunda.
Ifike muda tufanye mabadiriko bila kuitegemea sana serikali, serikali zetu zimeisha prove failure hivyo wananchi wafanye Yale yanayowapendeza.u
Wapande matunda kama , michungwa, stafeli, machenza, kuna matunda madogo madogo ambayo hata yakiangukia kwenye kitu hayaleti madhalaFikiria embe dodo au fenesi limemuangukia mtu au limeangukia kioo cha mbele cha gari!
Fuatilia miembe inavyo katika matawi au inavyo anguka ovyo wakati wa vuli au masika.
Fikiria miembe inavyo kuwa na matawi mapana sana na kuingia barabarani.
Fikiria tabia ya hatari ya makuti ya mnazi kupeperuka toka kwenye mti na kupiga vioo vya magari.
Labda tupande matunda jamii ya michungwa.
Kumbuka miti yenye mizizi mirefu kama mikungu jinsi ilivyo kuwa inaharibu lami au kingo za barabara au mitaro kule Posta na Oyesterbay.
Hata hivyo umeleta wazo zuri.
Matunda yataliwa hata kabla ya kukomaa, ni bora ipandwe miti ya kawaidaKwahiyo hayo maembe yakianza kuzaa yatakuwa yanakusanywa na watu wa manispaa au itakuwa ni free range,kila mtu anajilia anavyotaka...?
Wakala tena? Mi nilifikiri wakala ni yule anaepita kwa muda huo likidondoka tunda ni lakeWanataka ipanwe mipalachichi, michungwa au mikungu nk, matunda yasiyoweza kuleta madhara.
Msimu wa mavuno ukifika kuwepo na wakala wa mavuno.
Wakala tena? Mi nilifikiri wakala ni yule anaepita kwa muda huo likidondoka tunda ni lake
Acha hizo!Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpaka maeneo ya Osterbay hadi baadhi sehemu za Masaki.
Ukienda Morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli.
Mfano nimeenda nchi za kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani hata minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti, langu wazo tu asanteni.