Kwani TANROAD barabarani wasipande miti ya matunda kuliko hii ya sasa

Kwani TANROAD barabarani wasipande miti ya matunda kuliko hii ya sasa

Weka picha ya miti hiyo,, tukae kwenye kivuli ndo tujadili Uzi wako
 
Mbali na barabara?!!
Tanzania hasa kwenye miji na majiji yetu kuna nafasi hiyo?
Kupata hiyo nafasi ndogo tu imelazimu kuvunja nyumba za watu.

Kumbuka pia kuna eneo la kuweka miundombinu mingine pembeni ya barabara ambayo haiwezi kuwekea sehemu yenye hiyo miti kikubwa ya matunda.

Wakiwavunjia nyumba wapande hayo matunda utakuwa kulaumu hapa wanaongea watu.
Sam Nujoma Road ilipopanuliwa na kuachwa nafasi kubwa katikati watu walilalamika mbona wamevunjia watu, wamechukua nafasi kubwa na kuiacha katikati?
Leo faida yake imeonekana kwenye Ubungo Interchange/flyover toka mataa kuelekea Mwenge.

Akina Kakobe walipiga kelele mradi muhimu wa umeme grid ya taifa ulipopitishwa karibu na kanisa lake, leo uwaambie wavunjiwe ili ipandwe miembe kupendezesha jiji na watu wafaidi matunda?!!!
Basi wapande hata mipela au michungwa na hiyo mikubwa ya miembe ipandwe highway..
 
Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpaka maeneo ya Osterbay hadi baadhi sehemu za Masaki.

Ukienda Morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli.

Mfano nimeenda nchi za kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani hata minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti, langu wazo tu asanteni.
Tukipanda miti ya matunda barabarani halafu matunda yakaiva itakua vifo kwa watoto wetu.
Madereva wenyewe wa Tanzania unawajua. Akishakaa nyuma ya usukani mtoto anayemdhamini Ni yule aliyemzaa tu.
Chief wazo lako Ni zuri lkn things on the ground does not favour your proposal.
 
Wewe unataka balaa zingine zitokee!!, haitakuwa sahihi kwa matunda ya aina hiyo kuachwa watoto wavune holela bila nidhamu fulani, katika hali hiyo ndiyo maana wahusika wameamua kupanda miti isiyo na matunda ya kula.
Nimeandika hapo juu,tulipokuwa watoto huko barabara ya kigoma ujiji tulikuwa tunashinda kuangua maembe na hakuna kilichotutokea wala gari lililovunjika kioo kwa kudondokewa na embe.
 
Nimeandika hapo juu,tulipokuwa watoto huko barabara ya kigoma ujiji tulikuwa tunashinda kuangua maembe na hakuna kilichotutokea wala gari lililovunjika kioo kwa kudondokewa na embe.

Ni Barabara ipi ya kigoma -ujiji??!
 
Hats hapo mwanga kulikuwa na miembe, lubengela kulikuwa kuna miembe.Kama umezaliwa juzi huwezi jua hilo asilimia kubwa miembe hip imekatwa.Tulikuwa tunashinda ktk miembe tukipopoa maembe hio 80's inawezekana ulikuwa protini ya maharage au dagaa mim nilikuwa nshakuwa damu na nimeikuta hio miembe.kuna shule inaitwa muungano opposite kulikuwa na miembe na hata bembea zikuwa zinafungwa maeneo hayo Siku za sikukuu. Sizungumzi hadithi bali kitu nilichokiona.
Nakuongezea na hii,Tabora kuna Barbara nadhani ya unyanyembe ilikuwa miembe pande zote mpaka katikati kulikuwa na kivuli. Uliza wazee wakujuze.
Kigoma kuna mahala paliitwa mwembe togwa, huo mwembe ulikuwa barabarani kabisa. Nimehama Kigoma 1987 lakini bado nakumbuka,kanusha kama hakukuwa mwembe togwa barabarani
 
Wewe unazungumzia Kigoma mjini ya mwaka 1980🤣, Barabara moja ya lami kutoka Railway station hadi Ujiji, magari yaliyokuwa yakipita kwa wingi ni Town Bus (UKI), magari ya serikali, Tax na magari machache ya watu binafsi, katika mazingira hayo unadhani ajali za maembe, watoto na magari zingwezaje kutokea??--- Lubengela palikuwa na miembe miwili hivi pale kando ya daraja nayo ilikuwa mbali kidogo na barabara, juu ya yote miembe uliyoitaja katika mazingira hayo nafasi ya ajali kutokea ilikuwa finyu mno.

Miembe ungeweza kuitaja kwa kigoma mjini ni ile iliyopo Ujiji- kagera (iliyokuwa njia ya Watumwa zamani), miembe ya aina hiyo ipo hata Morogoro Boma Road ipo pande zote za barabara, wingi wake ndio mtu unaweza kusema inaweza kuleta ajali kama kungalikuwa traffic kubwa. Kigoma mjini mji ambao unayo miembe mingi ni Ujiji.
Sehemu nyingine katika barabara hiyo ya Lumumba iliyokuwa na Mwembe ni pale Hospitali ya Maweni, sehemu kama Mnarani Miembe ilikuwa mbali sana na barabara, kifupi ni kwamba miembe uliyoitaja ilikuwa ni michache na wala isingekuwa tishio kwa usalama wenu na magari yalikuwa yakipita kwa nadra.

Leo kulingana na Wingi wa magari huwezi kupanda miti ya matunda ukitaraji kwamba watoto wawe wakichuma bila kila siku kupata vifo kutokana na ajali za magari vinavyohusu watoto.

Nakumbuka nilipokuwa naishi DSm mtaa wa jamhuri karibu na Posta mpya, kule posta ya zamani katika vituo vya UDA kulikuwepo na miti ya mikungu pale jirani kuna shule ya msingi na sekondari Forodhani sikuona hata siku moja watoto wakiokota Kungu sio kwamba walikuwa hawapendi ila walihofia maisha yao kutokana na wingi wa magari, lakini katika shule za magomeni Mikumi kama Karume, Turiani nk, watoto walikuwa wakifakamia kungu ile mbaya.
 
Hii ishu inatakiwa watu wajitolee tu, kwa maafisa wetu wa serikali haitokuja kutokea labda vizazi vijavyo sio hawa meneja vitambi.
Kuna yule injinia walio kuwa wanarekebisha daraja la Dom mpaka Magufuli akampa kubwa jinsi alivyofuga kitambi,sasa utarajie ubunifu kwa injinia kama Huyo hata balanced diet tu imemshinda, akupandie wewe matunda.
Dini ya kiislamu imeagiza mtu atakaepanda matunda atapata thawabu sawa na mlaji wa hilo tunda.
Ifike muda tufanye mabadiriko bila kuitegemea sana serikali, serikali zetu zimeisha prove failure hivyo wananchi wafanye Yale yanayowapendeza.u
Unaishi mji gani? Huku mji nilipo mimi huruhusiwi kufanya modification ya aina yoyote baada ya ukuta wa nyumba yako au geti bila kibali cha mamlaka husika, mfano labda nje ya geti lako yanajaa maji mvua ikinyesha huruhusiwi hata kujaza kizege ili kuchepusha maji, etc sembuse kwenda kujitolea kupanda miti barabarani? Huo mnyororo wa vibali utakaokutana nao utarudi kwako kupika uji unywe na familia.
 
Kwa jinsi navyowafahamu wabongo imagine magari yanapita huku raia wakirusha majabali ili kudondosha matunda.
Na pia kukipandwa miti ya matunda itakua ni chanzo cha uzalishaji taka hasa mijini.
Miti inayofaa ni ile ya kupendezesha tu mji au barabara na kama issue ni kupunguza njaa ni bora kuanzisha kampeni ya upandaji miti ya matunda kwenye mazingira tunayoishi
 
Fikiria embe dodo au fenesi limemuangukia mtu au limeangukia kioo cha mbele cha gari!

Fuatilia miembe inavyo katika matawi au inavyo anguka ovyo wakati wa vuli au masika.

Fikiria miembe inavyo kuwa na matawi mapana sana na kuingia barabarani.

Fikiria tabia ya hatari ya makuti ya mnazi kupeperuka toka kwenye mti na kupiga vioo vya magari.

Labda tupande matunda jamii ya michungwa.

Kumbuka miti yenye mizizi mirefu kama mikungu jinsi ilivyo kuwa inaharibu lami au kingo za barabara au mitaro kule Posta na Oyesterbay.

Hata hivyo umeleta wazo zuri.
Wapande matunda kama , michungwa, stafeli, machenza, kuna matunda madogo madogo ambayo hata yakiangukia kwenye kitu hayaleti madhala

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo hayo maembe yakianza kuzaa yatakuwa yanakusanywa na watu wa manispaa au itakuwa ni free range,kila mtu anajilia anavyotaka...?
Matunda yataliwa hata kabla ya kukomaa, ni bora ipandwe miti ya kawaida
 
Wanataka ipanwe mipalachichi, michungwa au mikungu nk, matunda yasiyoweza kuleta madhara.

Msimu wa mavuno ukifika kuwepo na wakala wa mavuno.
Wakala tena? Mi nilifikiri wakala ni yule anaepita kwa muda huo likidondoka tunda ni lake
 
Wakala tena? Mi nilifikiri wakala ni yule anaepita kwa muda huo likidondoka tunda ni lake

🙉🙉🙉 Tunda lidondoke ndipo liokotwe??, kila mahali patakuwa na uchafu wa matunda mabovu yaliyopasuka, isitoshe sio jambo la Afya mtu kula matunda yaliyoanguka chini yenyewe hata kama yataoshwa, pia ni hatari kwa usalama wa wapita njia na magari pia.

Kazi ya wakala ni kuvuna, kuuza, kupata pesa na kusimamia usafi na utunzaji wa hiyo miti, pesa atakazo pata zitahusika na utunzaji wa hiyo miti nk.
 
Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpaka maeneo ya Osterbay hadi baadhi sehemu za Masaki.

Ukienda Morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli.

Mfano nimeenda nchi za kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani hata minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti, langu wazo tu asanteni.
Acha hizo!
Ati miti ya matunda, watoto watanzania barabarani!
 
Back
Top Bottom