Kwani TANROAD barabarani wasipande miti ya matunda kuliko hii ya sasa


Hata hivyo umefikiri vizuri
 
Kama nikudhuru magari kuna matunda ni madogomadogo. Wangepanda hata mikwaju. Hii haidhuru ikianguka. Sehemu kama dom ingekuwa poa sana. Kuna mazambarau na mang'ang'a pia.
 
Jiongeze mkuu hiyo miti ya matunda itapandwa pembeni sana mwa barabara.. Alafu ikumbukwe kitu njaa haswa kipindi cha itakuwa historia
Mbali na barabara?!!
Tanzania hasa kwenye miji na majiji yetu kuna nafasi hiyo?
Kupata hiyo nafasi ndogo tu imelazimu kuvunja nyumba za watu.

Kumbuka pia kuna eneo la kuweka miundombinu mingine pembeni ya barabara ambayo haiwezi kuwekea sehemu yenye hiyo miti kikubwa ya matunda.

Wakiwavunjia nyumba wapande hayo matunda utakuwa kulaumu hapa wanaongea watu.
Sam Nujoma Road ilipopanuliwa na kuachwa nafasi kubwa katikati watu walilalamika mbona wamevunjia watu, wamechukua nafasi kubwa na kuiacha katikati?
Leo faida yake imeonekana kwenye Ubungo Interchange/flyover toka mataa kuelekea Mwenge.

Akina Kakobe walipiga kelele mradi muhimu wa umeme grid ya taifa ulipopitishwa karibu na kanisa lake, leo uwaambie wavunjiwe ili ipandwe miembe kupendezesha jiji na watu wafaidi matunda?!!!
 
Kwahiyo hayo maembe yakianza kuzaa yatakuwa yanakusanywa na watu wa manispaa au itakuwa ni free range,kila mtu anajilia anavyotaka...?
 
Wasipande miti ya matunda aiseee, hebu fikiria uko kwenye gari la mkoa halafu pembeni ya batabara unaona maembe yameiva na huwezi kuchuma kwa sababu upo kwenye gari. Yaani kwa mimi safari nzima roho itakuwa inaniuma.
 
Nafikiri sana sana wanachozingatia katika kupanda miti kwenye hifadhi ya barabara ni : -mizizi ya miti iwe ya kwenda chini, si mirefu kwa uelekeo wa kusambaa ili kuepusha mizizi kuweka cracks katika kingo za barabara.

-Tree canopy isiwe pana.

-Kipindi cha uchavushaji baadhi ya miti huchafua mazingira.

- Kuepusha uwepo wa nyuki kipindi cha uchavushaji.

- Miti ya mapambo kwaajili ya kupendezesha barabara.
 
Upumbavu wa kusingizia wakoloni utawaisha lini ninyi waafrika? TABORA ILE MIEMBE Pembezon mwa barabara imekatwa miaka ya hivi karibuni baada ya kuonekana ina ingia barabarani na pia inaharibu barabara kutokana na mizizi mirefu.

Ile miti ilipandwa na wakoloni miaka hiyo tumekuja kukata sisi miaka hii. Huu ni upumbavu when we fail tunatafuta wa kuwasingizia ku fail kwetu. Tukubali tunaposhindwa then tujirekebishe.
 
Fikiria tu upo speed 100 mara embe dodo linaanguka hiyo break utakayokamata bila kukumbuka wa nyuma yako. Then unashuka mnaanza kugombea embe na dereva mwingine aliyekuwa mbele yako. No wasipande matunda aisee....
 
Kama barabara kubwa kutoka katikati hifadhi ya barabara ni mita 30 kwa sasa hatuna iwezo wa kujenga barabara eneo lote hilo hivyo eneo hilo ndo litumike kupanda miti hiyo, barabara haitaguswa na matunda ya kudondoka hata zaidi ya miaka 100
 
Wanataka ipanwe mipalachichi, michungwa au mikungu nk, matunda yasiyoweza kuleta madhara.

Msimu wa mavuno ukifika kuwepo na wakala wa mavuno.
Yapandwe hata mapera,makoma manga and the like.Wanyama,ndege na watoto wetu watajilia matunda ya bure na kudumisha Afya zao.
Tulipokuwa wadogo huko kigoma barabara ilijaa miti ya miembe na mizambarau tulifaidi sana matunda na tuliboresha afya zetu.Siku hizi matunda mpaka uende sokoni, hiii dhuluma kwa watoto wetu.
 
Hii ishu inatakiwa watu wajitolee tu, kwa maafisa wetu wa serikali haitokuja kutokea labda vizazi vijavyo sio hawa meneja vitambi.
Kuna yule injinia walio kuwa wanarekebisha daraja la Dom mpaka Magufuli akampa kubwa jinsi alivyofuga kitambi,sasa utarajie ubunifu kwa injinia kama Huyo hata balanced diet tu imemshinda, akupandie wewe matunda.
Dini ya kiislamu imeagiza mtu atakaepanda matunda atapata thawabu sawa na mlaji wa hilo tunda.
Ifike muda tufanye mabadiriko bila kuitegemea sana serikali, serikali zetu zimeisha prove failure hivyo wananchi wafanye Yale yanayowapendeza.u
 
Jamani, hivi huyu Mfugale si ni mwenyeji wa Mbeya?
Juzi tulikuwa Mbeya. Tukatembelea maeneo ya Majengo, Ghana, Nonde, nk.
Ee bwana ee!!, hizo barabara hata baiskeli haipiti. Hivi Mbeya kuna nini? Mbona watu hawalalamiki?
 


Wewe unataka balaa zingine zitokee!!, haitakuwa sahihi kwa matunda ya aina hiyo kuachwa watoto wavune holela bila nidhamu fulani, katika hali hiyo ndiyo maana wahusika wameamua kupanda miti isiyo na matunda ya kula.
 
Natamani kama Tanroads wangesoma hii post!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…