Kumekuwa na hili swala la kupokea sms mfululizo kutoka kwa namba zisizojulikana, yaani ukikaa kidogo utaona mara "iyo hela tuma kwa namba hii" mara "mzee nani nani anatibu mvuto, pete ya nini sijui" hujakaa sawa mara "jiunge na chama chetu" mara " mimi mwenye nyumba wako" na nyingine nyingi
Kwanini mamlaka husika zisiangalie namna ya kuzuia hizi namba mpya kutuma ujumbe kwenye namba ambazo hazijawahi kuwasiliana kabla, yaani kwa iwe kwamba ili nianzishe mazungumzo na mtu kwa njia ya text basi ni lazima kwanza niwe nishawahi kumpigia huyo mtu au yeye kunipigia mimi tukaongea. hii kitu inakera sana jamani