Kwani tukiacha madirisha haya ya aluminiam na PVC, ndiyo kusema sisi hohehahe hatuna madirisha yetu mengine ya kisasa jameni?

Kwani tukiacha madirisha haya ya aluminiam na PVC, ndiyo kusema sisi hohehahe hatuna madirisha yetu mengine ya kisasa jameni?

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,877
Reaction score
2,314
Binafsi si shabiki wa madirisha yanayotamba siku hizi, aluminiamu na pvc. Sababu kubwa ni kutokuwa na uimara wa kutosha na pia hata yakifunguliwa yanachukua sehemu kubwa ya dirisha na hivyo kuzuia hewa.

Hii ni mbaya zaidi kwa mimi wa sehemu ya joto. Madirisha haya yakifungwa, huko ndani mtajuta kuishi ndani hilo jengo. Kwani madirisha mengine ya kisasa ni yepi tukiacha yale ya tulipotoka?

Ndiyo tumekwama hapo?

Wabunifu mpo wapi?
 
Kwa sasa madirisha ya 'kisasa' ni hayo uliyotaja, kama unataka tutoke hapa basi buni mapya tupige hatua.

Ila sababu zako ulizotumia kuyaponda ni dhaifu mno, huenda tu huzitaki mbichi hizi…!!
 
Mbona unateseka, endelea kutumia nyavu au magunia…. you just got to hate what you can’t conquer!!

Ngoja tukutekenye basi, ni kweli hayo madirisha HAYAFAI…. hicho ndo unataka kusikia.
Mara nyingi type yako ni zile za kukalia tako moja huku unatype. Ni vigumu kuwa na hoja ama kusaidia. Wewe tayari...
 
Kwa sasa madirisha ya 'kisasa' ni hayo uliyotaja, kama unataka tutoke hapa basi buni mapya tupige hatua.

Ila sababu zako ulizotumia kuyaponda ni dhaifu mno, huenda tu huzitaki mbichi hizi…!!
Kwamba ukifungua ile space iliyofunguka ni ndogo kulingana na madirisha mbadala?

Unaona hiyo point ni duni?; Kwanza Faida ya Dirisha au umuhimu wa Dirisha ni nini?

Ukijibu hayo utaona mleta uzi ana point ya maana sana...
 
Mleta Uzi una point sana aisee wewe ni peponi moja kwa moja, now kwangu nimeweka grill tu nimetia na nyavu basi kwa sasa kwani kuna jirani yangu kayaweka anapata tabu sana fikiria umeiweka dirisha la 5×5 ukiweka hayo madirisha maana yake dirisha linakuwa 2.5
 
Kwamba ukifungua ile space iliyofunguka ni ndogo kulingana na madirisha mbadala ?

Unaona hio point ni duni ?; Kwanza Faida ya Dirisha au umuhimu wa Dirisha ni nini ?

Ukijibu hayo utaona mleta uzi ana point ya maana sana...
Bora hata umsaidie huyo. Akili yake inamuwezesha kurudi nyumbani tu kama kuku. Wala hayajui hayo madirisha ninadhani. Shukrani sana ndugu.
 
Hayo madirisha ni maalum kwa maeneo yenye baridi mfano Arusha, Moshi, Iringa na Mbeya hata Rukwa.

Sasa wabongo sisi wazee wa fasheniiz tumejikuta mpaka maeneo ya joto tunafunga vioo kwakuwa tumeamua acha twende tutafanyaje Sasa

Wale walioishi nje ya nchi na ndani ya nchi maeneo yenye baridi watakuwa mashahidi maeneo ya baridi dirisha la kioo ndio mahala pake ili baridi isingie ndani

Hii sawa ya ujenzi wa nyumba

Mfano Dar es Salaam wangapi mmeona nyumba za matofali ya kuchoma kwa sababu ipi, hakuna ni kutokana na upatikanaji wa udongo wa kufuatilia hizo tofali ni adimu sana, tofauti na Rukwa, Iringa, Songea na Mbeya uko ndio penyewe kwa tofali za kuchoma maana udongo upo na unafaa

Sasa ni ajabu uende eneo ambalo mchanga mwingi unakomaa na kutafuta tofali za kuchoma badala ya block
 
Jaribu hayo mkuu.
574685d7e2cebbccda5ecc7e189ed3d7.jpg
555a67b468117ffbf00ef03fb6cb893c.jpg
5831c6c2702c3dc1b856d243024d65d0.jpg
ec4eadb4c218f306ea71ce2bcce57277.jpg
6aefd8f55e2ee7f07d8828d979fac52e.jpg
c1ec0e42ace03cbade058ff5a07b7e44.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom