Kwani tukiacha madirisha haya ya aluminiam na PVC, ndiyo kusema sisi hohehahe hatuna madirisha yetu mengine ya kisasa jameni?

Hii tumei discuss sana na mwanangu mmoja hivi, ni kweli haina maana zaidi ya show tuuu, dirisha linatumika nusu
 
Kwamba ukifungua ile space iliyofunguka ni ndogo kulingana na madirisha mbadala ?

Unaona hio point ni duni ?; Kwanza Faida ya Dirisha au umuhimu wa Dirisha ni nini ?

Ukijibu hayo utaona mleta uzi ana point ya maana sana...

Hayo madirisha unayoita mbadala ni yapi ambayo huhitaji hufunguka yote?

Kama hata hujui faida za dirisha ni ngumu kujadili kwa weledi.
 

Hiyo futi 2.5 upana ambayo unaona haitoshi kuingiza hewa ndani unalinganisha na dirisha la aina gani?

Madirisha ya Aluminium ndo maana yamewezesha kuweka upana unaohitaji wewe, huwezi kulinganisha na yale ya nondo na wavu usiofunguka ambayo mara nyingi yalikuwa madogo kiasi.

Bado unajichanga tu ila zikitimia utaweka madirisha, acha wivu kwa huyo jirani kakutangulia tu…. jipe muda utamfikia au endelea kujitekenya.
 
Vitu viko on point mno. Mafundi sasa hapo uende akutengenezee hivyo atakutolea kitu cha ajabu mpaka ushangae

Halafu kitu kingine nilishawahi kunote na kusema humu. Tanzania ni kama hatuna architecture binafsi. Majengo yoote karibia tunajenga mjengo wa aina moja tofauti yetu ni ukubwa wa vyumba tu

Watu hawaji na idea mpya za majengo zaidi ya Yale Yale na mapaa Yale Yale sijui wenye hela za kujenga kwanini mmejificha kwenye kaboksi

Ngoja mie nijikusanye nijenge niache mdomo kusema ya watu😂😂
 
Hii tumei discuss sana na mwanang mmoja hivi, ni kweli haina maana zaidi ya show tuuu, dirisha linatumika nusu
Tatizo wabongo tunskurupukia mambo,hizo dirisha za aluminum ni lazima iwe kubwa minimum futi 5*5 sasa mtu hata futi 4 anaona kubwa eti anakwepa gharama.

Design ya hayo madirisha yanataka hivyo, pili zile vents za juu ziwe wazi hata ukilala ucku
 
Wabunifu wapo tatizo ni ushamba na kuona eti kulipia ramani ni ghali wanachukua ya fundi Michael, kingine ni uoga wa gharama kwa vitu vipya.

Matokeo yake nyumba zote mtaani zinafanana tofauti ni ukubwa na rangi za mabati, mtaani kuna nyumba za ajabu Sana.
 
Yeah dirisha linakuwa wazi nusu, inabidi watengene ya kuzama chini kama vioo vya magari watie na power windows😂😂😂
Ongeza ukubwa wa dirisha ndio design ya hayo madirisha badala ya hivyo viduchu eti mtu anakwepa gharama lazima italeta shida
 
Yaaani mimi hata huwa sielewi mtu anaposema kajenga nyumba Kali nikija kuiona naona ile ile tu kama lodge tunazolala na nyumba nyingine.

Hakuna uniqueness katika architecture ya bongo kabisa.
 
Ulipaswa wewe ndio utupe mbadala badala ya kuwatupia wengine mzigo.
 
Kuingiza mbu kwenye madirisha ya aluminium ni tatizo la fundi wako.
 
Kuna madirisha ya vioo ya BUGANDO M.C ni ya kizamani sana ila wame design vizuri sana yanafunguka kwenda juu kioo chote, na hewa inapita vizuri.
 
Tatizo wabongo tunskurupukia mambo,hizo dirisha za aluminum ni lazima iwe kubwa minimum futi 5*5 sasa mtu hata futi 4 anaona kubwa eti anakwepa gharama.

Design ya hayo madirisha yanataka hivyo,pili zile vents za Juu ziwe wazi hata ukilala ucku
Ehee! Kuna kitu wajengaji wa siku hizi wanakisahau.

Siku hizi nimeona hawaweki venti. Nilimuuliza jamaa yangu mmoja kwa nini hajaweka venti, akasema ni ushamba!

Jamani, venti ni muhimu ili hewa iingie ukifunga hilo dirisha la alluminium. Ukiliacha wazi usiku, vibaka wanatamani kuja kujaribu bahati yao.

Venti zirudi jamani, tena zile zinazoonesha mwaka zilikuwa poa kweli!

Unaweka frame na wavu kwenye venti safii!
 
Asante sana. Haya ni mazuri mno. Kwa mimi, aluminium haziingii hapa hata kwa 1/4. Swali ni , wavu wa mbu unakaa wapi hapo?
Ukipata fundi mzuri anakutengenezea inakuwa na double shutter, ndani kunakuwa na shutter za wavu halafu nje zinakuwa hizo.. Hapo mbu utawasikia kwa jirani.
 
 
Ukipata fundi mzuri anakutengenezea inakua na double shutter, ndani kunakua na shutter za wavu alafu nje zinakua hizo.. Hapo mbu utawasikia kwa jirani.
Hili ndio suluhisho. Kuna Nyumba niliwahi kuona hii kitu. Wameweka na wavu wa kuslide kwa ndani ya dirisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…