Kwanini 90% ya Mabao ya Mbwana Samatta ni Tap-Ins.?

Kwanini 90% ya Mabao ya Mbwana Samatta ni Tap-Ins.?

Mleta Mada ongeza bidii ,kijana hachani mkeka
IMG-20180930-WA0000.jpg
 
Nimekuwa nikijiuliza kwanini Mbwana Samatta ameganda pale pale Genk KRC pasi na kusonga mbele.?

Wamekuja wakina Bailey wamesepa..

Wamekuwa wakina Ndidi wamesepa...

Kwani uwezo wake unatia shaka wazungu?

Nilichogundua ni kwamba uwezo wa Samatta ni wa Ligi ndogo ndogo sana barani Ulaya.

Ukizingatia matakwa makubwa sana ya Mshambulizi kwenye soka ni kuwa na uwezo wa ziada na si kufunga mabao tu.. Mbwana amekosa mambo kadhaa ya kiufundi ambayo anatakiwa awe nayo mshambuliaji ili aweze kukidhi kumudu nafasi za juu kwenye klabu zitokazo kwenye ligi kubwa barani Ulaya.

Samatta kama Mshambuliaji amepewa vitu 2 na Mwenyezi Mungu.

1. Insticts (Inayozaa Anticipation)
2. Finishing.

Vitu ambavyo havitoshi kabisa kuhimili mikiki mikiki ya Wakubwa wa Bara la Ulaya.

Nimefualia karibia 90% ya mabao afungayo akiwa Genk ni Tap - Ins.
Kwa wasio elewa maana ya Tap-ins ni ile mipira inayokufikia miguuni au kichwani na kuikwamisha nyavuni mara mona pasi na kuipooza.

Ni nadra sana kuona Mbwana akifunga bao baada ya kupunguza walizi waliwi au watatu.

Kitu ambacho mshambuliaji aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa namna hiyo pia.

Kama akikutana na defence mechanism ambayo inafanya Man to Man marking jamaa anakuwaga anatoa jasho tu kama bomba wa maji ya Dawasco lililo toboka.

Nknachokiona ni kwamba Mbwana Samatta ataishia kucheza soka Genk pekee na mwisho wa siku kustaafu soka akiwa pale pale.

Samatta wetu ni wakawaida sana.View attachment 881959
Wapo wachezaji wengi wanafunga magoli ya aina hiyo kwenye ligi kubwa ulaya. Labda kama umeanza kufuatilia mpira juzi
 
Jamaa kaongea ukweli kbs, Samatta sijui kama anaweza chambua kama Hazard
Ko wew shida yako ni samagoal achambue Kama Hazard tatizo umekalia kichwa nasehemu yako yakukalia iko kichwani ko unachoandika ni takataka zilizoshindwa kumeng'enywa na mwili [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Unataka kusema samatta ameanza kufunga magoli kama ya CR7 (penaldooo) emu tuanze kujisifia i ni atua kubwa sana kwa nchi yetu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wabongo mpaka tumkubali bongo mwenzetu! Ujue parapanda linalia Yesu anarudi tena. Samatta alikuwa majeruhi ndio kwanza anarudi kwenye form yake tena.
 
Giroud ufungaji wake mabao hana tofauti na samata...ni mmaliziaji hana mbwembwe nyingi na yupo Chelsea. Acha roho ya kwanin mzee baba. Samata all day
 
Huko ligi kubwa kuna wanaofunga kama samatta wengi tu...
Mbona husemi akina AJIBU wanafanya nn hapa bongo.
 
nataman nimtukane mtoa mada ila baada ya kugundua kuwa ni mtanzania bas tu. watanzania huwa hatupendan.. wakt wakenya wanataman waanze kusema samatta ni mkenya baadhi yetu et tunataka kumsaliti. hata afunge kwa shingo sawa tu bhan... mpira magoli.
 
Soka la sasa limebadilika sana .....Thats why watu kama hao hawawezi kudumu kwenye soka la sasa Ulimwenguni....

Nitajie mshambulizi wa sasa mwenye kaliba ya Samatta kwenye Ligi kubwa .....
Diego costa, Olivier Giroud, Jamie vardy.
Hao mpira ukija anakufunga
 
Hivi mkuu lukaku anaweza kupunguza hata diffenders 2 lakn cha ajabu anachezea club bora kabisa duniani tupende vyakwetu hukuti mkenya akimkosoa mchezaj wake hata utayakuta bongo tu nimeamin usemi wa wahenga KIKULACHO.......
 
Kinachomsumbua mtoa mada ni ule ugonjwa wetu wa miaka yote. U Simba na U Yanga. Mtoa mada nadhani U Yanga wake unamsumbua. Jamaa Samatta hachezi Bongo yupo nje kama aliwahi Pitia Simba hiyo ni historia tuu. Ampe Sifa zake anazostahili.

Suala la tap ins pia ni sifa. Wenzetu wanaangalia umepata nafasi ngapi ume convert ngapi. Mtu mwenye chances 5 aka convert 5 hata kama ni tap ins anahesabika ni bora kuliko anaye dribble na mwisho kupoteza tuu.

Alicho nacho mtoa mada ni Asilimia kubwa ya Watanzania tulivyo. ROHO MBAYA.
 
Diego costa
olivier giroud
Álvaro morata
Chicharito
Mitchy batshuay
Pierre aubamayang
Hao je wana nini kingine cha ziada??
Wabongo tuna safari ndefu sana..
 
Hivi umeshawahi kumuona chicharito akicheza? Samata hicho anachokifanya ndicho anachokiweza.
Hapo alipofika ni mafanikio makubwa sana. Mimi nitaendelea kumhesabu kama shujaa.
 
Umeongea kitaalamu vizuri tu.. Sema Luna kitu umesahau.. Hata kina trosand magoli wanayofunga ni kama hayo tu.. Nafikiri ni mfumo tu wa kiuchezaji ndo unaosababisha.. Samata kakusanya sana vijiji mazembe huko
 
Giroud kamchukua beki gani, Na mbona yupo timu kubwa Uingereza?
 
Samata siyo Ronaldo wala Messi lakini kiwango chake ni kikubwa sana,ni goal poacher anajipanga kanika nasafi nzuri kama striker hiyo mipira haimuangukii tu kichwani na miguuni na kuelekea kwenye nyavu na makocha wengi wanapenda goal poachers,kama unamkumbuka Raul wa madrid enzi hizo,au Gyan assamoah wa Ghana,au Didier drogba nionyeshe video zao hata moja wamepiga chenga mabeki watatu na kutingisha nyavu,maoni yangu dogo aongezee bidii kwenye kupiga free kicks lakini siwezi kusema ni striker mbovu.
 
Hivi watanzania kwanini huwa hatupendi debate, ni mfumo wa elimu yetu au kitu gani. Kwa nini usimjibu kwa hoja.
90% ya uchambuzi wako ni chuki dhidi ya samatta ila sikushangai kwa kuwa ni mtanzania mwenzangu roho zetu zinajulikana kwenye mafanikio ya mtu
 
Back
Top Bottom