Kwanini Ali Kiba kaanza kukamata pesa ndefu tangu zamani lakini bado sio tajiri?

Kwanini Ali Kiba kaanza kukamata pesa ndefu tangu zamani lakini bado sio tajiri?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ali Kiba kaanza kuimba zamani sana aisee, miaka ya 2006 jamaa aliwahi kupewa milioni 200 kwa mauzo ya kaseti na cd zake, hio milioni 200 ya enzi hizo naweza kusema ni kama milioni 600 ya sasa.

Hakuishia hapo tu aliendelea kupiga mikwanja mizito endelevu miaka na miaka mpaka sasa lakini bado hawezi kuwekwa level ya kiwango cha msanii tajiri.

Kiuchumi yupo vizuri ila hatuwezi kumweka level za tajiri kama wasanii wengine wa Afrika ambao wamo kwenye list ya matjiri.

Magari - Gari zake nyingi ni toyota za mjapani ambazo hazivuki milioni 100, wasanii matajiri wengi hununua magari ya ulaya na marekani ya kuanzia milioni 500 mpaka mabilioni, hata range huwa inaonekana gari ya kawaida

Makazi - Nyumba anayoishi nayo nzuri lakini haijafikia viwango vya jumba la kifahari, wasanii matajiri huishi kwenye mijumba ina swimming pools, back up generators, nk

Mavazi - Nguo anazovaa za kawaida sana, kumkuta kanyuka hata Gucci kama ilivyo kwa wasanii wengi matajiri ni nadra

Ali anafeli wapi ??
 
Ali hela anayo ila mnawakosea sana wasanii wa bongo kutaka walingane na Diamond.

Mkiweka kipimo cha Diamond kuwa ndio kuwa na pesa kwa msanii basi hata wasanii wakubwa tu wa South Africa na Nigeria mtasema hawana pesa.

Bado kidogo mumfilisi Harmonize kwa madeni baada ya kuanza kukopa hela ili ashindane na Diamond mwisho akachemka ameacha siku hizi.

Diamond ni lidude likubwa zaidi ya media income yake kwa mwezi ni hatari tupu.
 
hapo kwenye hela aliyonayo nadhani kibongobongo anayo lakini kwenye levels za kuwa na mpunga wa kuendana na wasanii wenye pesa africa akiwemo mdogo wake Chibu, hapo hafikii hata theluthi

Nadhani ali kiba kitu pekee anachotegemea kupata hela ni muziki tu ndio maana hafiki mbali, kwa wanaijeria huko mziki unaweza kulipa lakini kibongo bongo mziki pekee ni ngumu.

Akitegemea mziki peke yake gari atazoweza kuzimudu ni kama hizi za kina harmonize range rovers mtumba za milioni 100.
 
Ali hela anayo ila mnawakosea sana wasanii wa bongo kutaka walingane na Diamond.

Mkiweka kipimo cha Diamond kuwa ndio kuwa na pesa kwa msanii basi hata wasanii wakubwa tu wa South Africa na Nigeria mtasema hawana pesa.

Bado kidogo mumfilisi Harmonize kwa madeni baada ya kuanza kukopa hela ili ashindane na Diamond mwisho akachemka ameacha siku hizi.

Diamond ni lidude likubwa zaidi ya media income yake kwa mwezi ni hatari tupu.
South Africa ipi??? Diamond mwenyewe hamfikii Somizi kwa pesa, lol. Unachekesha sana wee, hapa sio FB.
 
Ali Kiba hajitumi kuzisaka pesa kwa kiwango kile cha kujituma,anaonekana ni mtu wa kuridhika sana tofauti na watu kama Diamond Platinumz,Harmonize n.k. hivyo kumfanya awe na hela ya kawaida tu.Wasanii kama Diamond,wanaingiza pesa kila sekunde,dakika na SAA,hata yale tunayoona anamiliki,jamii inaona anastahili,ingawa watu wengine wanaona Diamond hana pesa,najiuliza,mtu anajituma vile,hela zinazoingia zinaenda wapi ili tuseme watu kama Alikiba ambao mbanga za kutafuta pesa kwao hatuzioni,wamzidi?

Tofauti ya Kiba kimaendeleo lazima iwepo kutokana na kipato cha kawaida.
 
Sema kuna watu ni low key ana make moves chini chini sana kama huyu mwamba..mana kiba ana tag la nguvu kwanzia kwa mama mwenye nchi na wazito wote serikalini bila kusahau kina 001.. na utajiri ni watu aisee asikuambie mtu! siamini konde ana mtonyo kuliko kiba japo konde anajitutumua kweli kweli
 
Konde kwa alikiba hapana bado Sana... Harmonize nivile anajitutumua ila ukiangalia kazi yake ya mziki, shows and everything ni kawaida Sana.. ALIKIBA alianza siku nying kuji weka Sawa kiuchumi idnt think so kama anamuweza Ali..... Ila diamond ndo iko wazi bwana mdgo hela anapiga angalia miezi mitatu iliopita kashapiga show za nje zaidi ya tano tena ulaya wakati huo hakuna msanii wa Tz aliegusa ulaya kwa miezi mitatu iliopita... Kwene digital platforms kila mwezi unaona yeye ndie anaefanya vzur Tena kwa kuwa acha mbali sana wanaomfwata
 
Utajiri ni siri juhudi pekee hazileti utajiri

Utajiri ni Roho

Fuatilia kuhusu Mammon siku nikipata mda nitaandika kuhusu mungu (gods) wa utajiri au Mshana Jr mshana aeleze kidogo ili watu waelewe elimu ya Mammon
 
Watakuja kusema ni wivu lkn huo ndio ukweli mchungu.

Huyo jamaa kinachomponza ni kiburi na kutotaka kusikiliza maoni ya watu, jamaa anaoneakana ni mtu wa kuridhika sana, yaan hapendi mambo mengi, pia hana ubunifu.

Itoshe kusema huyo jamaa haimbii shida bali anaimba kuwafuraisha mashabiki wake ambao hawavuki mipaka ya East afrika, ama tuseme Tz na Kenya[emoji23][emoji23][emoji23].

Jamaa angekuwa mbunifu na mpambanaji kama akina fulan basi East afrika nzima hakuna ambaye angethubutu kujifananisha naye, yule angekuwa level za akina davido ama zaid maana kaanza muziki zaidi yao kaishi ndani ya gemu kwa muda mrefu lkn kawa USELESS kwa taifa hafai kuwekwa viwango vya kuiwakilisha taifa[emoji1787][emoji1787].

At least kwa kipindi hiki kaanza kuchange baada ya kuona mambo yanavyotakiwa kwenda sasa kaanza kufuata taratibu za gemu, kaanza kushirikiana na wanamuziki wa nje ili kuisambaza kazi yake, naona hata akina rudeboy wanampata, tofaut na hapo mwanzo alijikita na collaboration za akina underground wakina aslay na baraka da prince kumbe level zake akina wizkid[emoji23][emoji23].

All in All muziki wake si biashara bali burudan hivyo haumpi maendeleo kama wanayofanya wasanii wanaojua sanaa ya biashara ktk muziki[emoji23][emoji23].

Kina kondeboy, marioo na Rayvann washampita huyo jamaa yenu
 
Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba alikipa hela alizopiga ni za Fiesta tu na show kadhaa lakini pia anapiga madili madogo madogo tu kutoka katika makampuni ya hapa bongo ila Diamond mbali na muziki pia ana biashara nyingi sana zinazomuingizia pesa ikiwamo na online platforms kama websites, YouTube's Instagram yani Alikiba kifedha atasubiri sana kwa mtoto wa tandale...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda hajaamua kujikweza na karidhika na alichonacho

sio lazima wote tufanane style za maisha
 
Back
Top Bottom