YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Sio lazima kuna vitu vingi zaidi ya hivyo vya ukuu wa mkoaIli uwe mkuu wa nchi Tz ni muhimu kutokea ukuu wa mikoa huko serikali unaijulia kupitia mikoa
Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Mtu achape kazi tu eneo lake wanaojua kuangalia watampa tu
Magufuli alipata kwa njia hiyo tu hakuhonga wajumbe, wala uraisi alikuwa hataki akashinikizwa baada ya kuona kuna moto.Kuwa kuna uwezekano wa CCM kupigwa chini 2015
CCM ikalazimika isitake itafute mtu analia na wananchi hata kama ndani ya chama hakubaliki sana!!! Kwa traits za tabia yake!!
Cha msingi fundi na kibarua hujulikana law kazi zao
Ushauri wangu kila mtu achape kazi eneo lake ikiwa nzuri hata mbele ya Safari Mungunatakuwa mtetezi wake na atamsaidia.Kwenda juu
Watu wajifunze kilichotokea 2015
Giants wenye pesa na connections na kukubalika ndani ya Chama walibwagwa chino na Magufuli ambaye hakuwahi kushika cheo chochote cha huchaguliwa ndani ya CCM hata cha ujumbe wa nyumba Kumi hadi Professor Mwandosya alilalamika kuwa mtu kama huyu asiye na uzoefu ndani.ya CCM anapewaje uenyekiti taifa kwa kuteuliwa ugombea uraisi?
Watendaji ndani ya CCM na Serikalini.chapeni kazi mlizopewa maeneo yenu.Ndiyo yataamua future zenu sio.kuchonga mifomo tu na kuuza sura kwenye press!!
Lowasa alikwama pamoja na kuwa Press zote zilikuwa kiganjani mwake