adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 12,207
- 26,521
Moja kwa moja
Kwa utafiti wangu mfupi usio rasmi niliofanya mimi binafsi kupitia stori na watu mbalimbali, vijiweni, mitandaoni nk. nimegundua mara watu wengi wakilalama kuwa wanapata wakati mgumu mara nyingi wakihudumiwa na watumishi wakike tofauti na wakiume kutokana na jinsi wanavyoreact katika kuhudumia wahitaji.
Mimi binafsi kuna nilikuwa nafuatilia kitambulisho cha uraia NIDA katika moja ya ofisi zao ikatokea kuchaguliwa watu kama wa tano kuingia chumba fulani baada ya kufika mtumishe wa kike alianza kusema kwa ukali "mmefika baada mkae kwenye benchi mnaanza kuganda kama masanamu nyinyi ni watu wa aina gani"
Haikupaswa yeye kutoa kauli kama hiyo tena kwa ukali wakati kuna watu waliokuzidi umri tena wazee bali alipaswa kutuelekeza mahali pa kukaa kwani mabenchi yalitengwa na watu wanakaa sehemu husika kutokana na shida zao .
Kwa kumalizia hali kama hii haipo sehemu moja kwani nimeshuhudia sehemu kibao ikiwemo Rita .Sasa sijui wanawake wanakua na matatizo gani kupelekea hali hiyo mpaka wakati mwingine mtu unajiuliza kama ulishawahi kumkwaza siku fulani au la ..