KERO Kwanini baada ya mwaka mmoja taarifa za mtu aliyefanya usaili na kufaulu katika Ajira Portal zinaonekana zime-expire?

KERO Kwanini baada ya mwaka mmoja taarifa za mtu aliyefanya usaili na kufaulu katika Ajira Portal zinaonekana zime-expire?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto katika mfumo wa Ajira Portal, ambapo baada ya kupita mwaka mmoja, taarifa za mtu aliyefanya usaili na kufaulu huonekana kuwa zime-expire.

Hali hii imekuwa changamoto kwa vijana wanaotafuta ajira, kwani mtu anaweza kufaulu usaili wa awali lakini baadaye akashindwa usaili mwingine, jambo linaloweza kumfanya akose fursa ya ajira licha ya kuwa aliwahi kuthibitisha uwezo wake kupitia usaili wa awali.

Tunaomba Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma itafakari upya utaratibu huu na kuangalia uwezekano wa kuboresha mfumo ili matokeo ya usaili wa mtu aliyefaulu yaendelee kutambulika kwa muda unaofaa, badala ya ku-expire baada ya mwaka mmoja.

Hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto kwa vijana na kuongeza ufanisi na usawa katika mchakato wa ajira za Serikali.
 
Kwa nini mtu aliyefaulu usaili arudie usaili baada ya database ku-expire?
Kama sifa na taaluma bado ni zilezile, kwa nini pass yake isiendelee kutambuliwa?
Je, database inaweza kuhuishwa badala ya kufutwa kabisa?
Je, nafasi mpya zinazofanana na taaluma za waliofaulu zinaweza kwanza kuangaliwa kwenye database?
Uwazi kuhusu idadi ya waliofaulu, walioajiriwa kupitia database na waliobaki baada ya database ku-expire.
 
Back
Top Bottom