Kwanini baadhi ya vigogo au wenye ukwasi hawawaamini madaktari wa Bongo?

Kwanini baadhi ya vigogo au wenye ukwasi hawawaamini madaktari wa Bongo?

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,751
Nchi kama za Uchina na India Wananchi wake wote hutibiwa na madaktari wa nchi zao kwenye hospitali za nchi zao. Wanawaamini ssana madaktari wao na hospitali zao kuliko wa nje. Vigogo wao wote hutibiwa nchini mwao na hujisikia kuwa salama zaidi kuliko kutibiwa hodpitali na madaktari wa nchi za nje.

Sisi hata check up tu ya kuona kama mfupa umeunga au vipi, vigogo na matajiri wetu hawawaamini madaktari bingwa wetu wa mifupa hata kama wana ma PhD kibao waliyoyapata huko huko ulaya au marekani. Ili mradi wako Bongo hawawaamini. Watamwamini yule aliyoko ulaya au marekani hata kama ana ka master degree pekee!

Kipi kifanyike na mind setting ya vigogo wa aina hii?
 
Kama mnajengewa tu barabara bado hamjitambui nani atawaamini ?
Kwa hiyo hata wahandisi wetu nao hatuwaamini? Watalaam wetu wote wandani wakiwemo na huyo mwanasheria hatuna imani nao? Tunawaamini tu hao wa mataifa makubwa? Lini tutaanza kuwa na imani nao?
 
Watu wanafuata ubora wa huduma. Bahati mbaya zaidi hao wanaoenda hizo hospitali zetu za ndani ni kwa sababu hawana uwezo wa kufuata huduma bora nje ya nchi hii.

Naomba nikupe mifano hai,

Mfano wa kwanza, mzee wangu aligundulika na saratani steji ya kwanza mwaka 2009, akaanzishiwa matibabu pale hospitali ya Ocean Road. Akawa vizuri kabisa lakini baadae ilirudi na 2016 alifariki.

Mfano wa pili, kuna Doktari mtanzania anafanya kazi Urusi, alikuwa anauguliwa na dada yake saratani steji ya kwanza. Alikuja kumchukua hapa kwetu na kumpeleka Urusi kutibiwa na yule mama alipona na kuishi miaka 20 zaidi.

Kupitia mfano huo wa kwanza na wa pili unaweza kupata picha ya ubora wa huduma tunaozungumzia.
 
Kwa hiyo hata wahandisi wetu nao hatuwaamini? Watalaam wetu wote wandani wakiwemo na huyo mwanasheria hatuna imani nao? Tunawaamini tu hao wa mataifa makubwa? Lini tutaanza kuwa na imani nao?
Hao ambao hawaamini wana taaluma na wataalam wetu, ndio haohao wanaotutengenezea sisi na wanetu mitala ya elimu. Wanatupa elimu duni na watoto wao hawasomi na wetu, ili watutawale vizazi na vizazi
 
Tunawaamini labda useme Magonjwa yetu ndiyo hayawezekani kutibika Tanzania hii.
 
Kama daktari hajui kama wewe kwanini umuamini. Sasa wewe kwenye issue za Tiba, unazungumzia ma PhD. PhD inahusu nini kwenye matibabu?
 
Kwa hiyo hata wahandisi wetu nao hatuwaamini? Watalaam wetu wote wandani wakiwemo na huyo mwanasheria hatuna imani nao? Tunawaamini tu hao wa mataifa makubwa? Lini tutaanza kuwa na imani nao?
Dr acha tu wengine wasikuamini ila mm nakuamini nikiumwa ntakuja kwako.😁

Kwanini hawaaamini? Mi kwa sababu misingi ya elimu tangu awali ilikuwa mibovu, mtu anahisi huyu hayupo vizuri. Coz ni ngumu kwenda hospital ukauliza huyu dr alisomea ulaya ama? Au huyu dr anajua hili kweli? So mgonjwa anapoenda hospital anajua ni wale wale hata kama umesomea ulaya.hasa ukiwa kwenye hospital za serikali.

Sababu nyingine huduma mbovu. Juzi nilikuwa na mteja nikawa namuuliza mbona baba yako alikuwa ni mwelewa kwa nini hakuandika hata urithi? Akajibu alikufa gafla, alipelekwa hospital wakawa wameenda na hela ndogo mwingine akaifata nyumbani mgongwa alichelewa kutibiwa wakisubiri malipo yakamilike. Aliyeleta hela alichelewa kama 2hr mgonjwa hajaguswa hata kidogo. Pesa inaletwa na mzee anatangulia kwa baba.

Sasa mwenye pesa zake kwa nini asiende ulaya ambako anajua hata akijamba dr anataka ajue kwa nini kajamba ushuzi mbaya?😂😂

Hivyo basi kama unataka wakutambue kuwa private, huko watu wako huru mgonjwa akifika anasema nakata kumuona dr fulani.

Note: sisi watu wa kawaida tunawaani ma dr wetu.

Mkapige kura jamani.
 
Ni mazingira ya Tz yanawafanya wasijiamini (hasa waliosoma baada ya uhuru) na kupelekea kutoaminika.
Mfano wangu ilitokea mtu anaumwa, tumbo limemvimba, daktari wa enzi hizo ambaye alishastaafu tangu miaka ya 90 akasema huyu utumbo umefunga kwa kumuangalia tu. Daktari wa .com akataka afanyiwe MRI na vikorombwezo kibao, vikachukua muda mrefu mgonjwa akafa na matokeo ni kweli utumbo ulikuwa umeziba au kufunga (bowel obstruction).
 
Hao ambao hawaamini wana taaluma na wataalam wetu, ndio haohao wanaotutengenezea sisi na wanetu mitala ya elimu. Wanatupa elimu duni na watoto wao hawasomi na wetu, ili watutawale vizazi na vizazi

Kwa comment hii namwombea Bujibuji msamaha, Moderator mpunguzie adhabu aachiwe kwa onyo tu.
 
Kama huyu mgombea urais mwenye uraia wa ubeligiji
 
Kuna tofaut ndogo sana kati ya mganga wa kienyeji na madokta wa kibongo
 
Nchi kama za Uchina na India Wananchi wake wote hutibiwa na madaktari wa nchi zao kwenye hospitali za nchi zao. Wanawaamini ssana madaktari wao na hospitali zao kuliko wa nje. Vigogo wao wote hutibiwa nchini mwao na hujisikia kuwa salama zaidi kuliko kutibiwa hodpitali na madaktari wa nchi za nje.

Sisi hata check up tu ya kuona kama mfupa umeunga au vipi, vigogo na matajiri wetu hawawaamini madaktari bingwa wetu wa mifupa hata kama wana ma PhD kibao waliyoyapata huko huko ulaya au marekani. Ili mradi wako Bongo hawawaamini. Watamwamini yule aliyoko ulaya au marekani hata kama ana ka master degree pekee!

Kipi kifanyike na mind setting ya vigogo wa aina hii?
wanajua wabongo mnamtima nyongo mnaweza kuwamalizia ajili ya shida zenu. Tiba zenyewe mmeiga iga tu. Angalia nkapa kafa kamuacha mzee mwinyi.waryoba wanadunda.kujifanya eti home is de best!

Unaweza kwenda kutibiwa wakakubania kirahisi tu mara x ray haifanyi kazi. Mara utlasound inakichomi yaani hayaeleweki.

Madaktari wakuu na ma HR wana roho za kijicho ni usipime. Dr au nurse ukifanya jambo zuri wanakubania km Dr Sylvia Mamkwe anavobania watu.Akitibia mkubwa wa srikali akapona uzuri vinaanza visa.

Utapewa nafasi mpya. ukae mapokezi wkt weye ni Dr.

Jambo Lingine Usijibidishe kusoma zaidi!!! maneno utayopata utakaa chini. Labda uwahonge!

Sasa mleta mada nakuuliza ni nani atakubali kutibiwa na mtu mwenye visasi kinyongo?
Mkeo tu ukimuudhi hakupi papuchi vizuri.hakukaangii mboga uzuri. Sasa mtu baki je?

Waache waende kwa usalama wao hkn mtu anapenda kufa. Na wakifa huko ni bahati mbaya sana, hawatarudia kuua!
Hata km ni wewe huwezi tibiwa na mtu maskini .hajala,hana hela, ana kinyongo cha wazi. Visasi. Lugha hovyo ajili ya shida. Anasubiri timing ya part tomemuda wote.mchafu, ananuka kikwapa! Mlevi, mazingira ya ofisi machafu mfano OPD Temeke Hosp. Jamani!!!! Unakufa kwanza! Kabla hujatibiwa!

Kwa sababu ya njaa wamekaa kimachale sana. Na PCB wakikuona una nyama nyama hivi wanakuzonga sana.
NURSE anakutaka akukule!kwanza kabla! Na Drs ndo kabisaaaaaaa!!!!
 
Back
Top Bottom