Kwanini baadhi ya wasanii wetu hawapendi kutoa support kwenye Media zetu za nyumbani?

Kwanini baadhi ya wasanii wetu hawapendi kutoa support kwenye Media zetu za nyumbani?

victor moshi

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
829
Reaction score
1,061
Mimi ni mdau mkubwaa sana wa mziki sana. Huwa napenda kufuatilia kila mwanamziki awe mdogo au awe mkubwa.
Tatizo lina kujaa palee baadhi ya wanamuziki wanapotoa music video utasikia anaenda ku premiere video kwenye vituo vingine vya out na Bongo utadhani Tz hakuna music television. Na kama ukikuta ana premiere video yake Bongo mpaka aombwee sana.

Katika kulifuatilia hili nimegundua most wasanii wa njee sijaona eti msanii ameanzaa ku premiere video yake out side of his country kama wapo ni silimia ndogo sana akasahau mashabiki zake waliomfikisha pale (Tunajua si WaTz wengi hua tunatazama free Tv station kwenye ving'amuzi vyetu hatumudu kununua vifurushi vya hivyo ambavyo international music tv zinapatikana)

Huyo mwanamziki haoni kuwa ana mnyima haki yule shabiki wake wa hali ya chini haki ya kuwa wa kwanza kuitazama video yake?

So katikaa hayo, nikajiuliza maswali matatu ambayo nimekosa majibu;

1) Hivi Mwanamziki ukitaka kufikia level za International lazima u premiere video nje?
2) Hapa Tanzania hakuna TV Station ambazo zinafikia level za kimataifa na wenzetu wakaona umuhimu wa ku-premiere video zao kwenye TV za Tanzania?

3) Au potelea mbali Media za Bongo a.k.a Tz mizinguo tu na ubabaishaji mwingii???

Nawasilishaa #mtazamowangutu
 
Mimi naamini lengo si baya bali lengo ni kuvusha muziki wetu nje ya mipaka!

Vituo vya nyumbani vina mchango mkubwa sana kwa wasanii wetu ndio maana wengi wanao kwenda nje wana hakikisha wamesha teka mashabiki wa ndani kwanza ndio wana vuka mipaka na hakuna msanii anaye vidharau vituo vya ndani maana vyenyewe ndio vina wakuza kabla ya kwenda nje!

Bado naamini lengo ni jema kabisa...

Pia bado hatuna kituo cha burudani kinacho angaliwa kwa wingi na watu dunia nzima nayo ni sababu!
 
Msanii kama Diamond haitaji kutumia nguvu sana kufanya wimbo wake upigwe kwenye vituo vya bongo coz anajua wimbo wake utapigwa tu, soko la ndani ni lake tayari, but kupigwa kwenye vituo vikubwa vya kimataifa kunahitaji nguvu ya ziada, inabidi ujipendekeze kwelikweli
 
Back
Top Bottom