Kwanini bandari apewe DP World?

Kwanini bandari apewe DP World?

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Kabla hamjakimbilia kutuambia faida na hasara, chambueni kwanza vipengele vya mkataba na mjibu maswali yanayoulizwa.

Nia ya kumtafuta DPW ilitokana na report ipi ya uchanganuzi wa ufanisi wa bandari?

Tenda iliyozishindanisha kampuni tofauti tofauti kisha ikapatikana DPW ilitangazwa wapi?

Mgao wa Tanzania kwenye huu mkataba utakuwa ni upi? Umeainishwa wapi?

Majukumu ya Tanzania kwenye Huu mkataba ni yapi?

Ukomo wa mkataba ni wa muda gani? Kwa nini?

Kwanini mkataba unahusisha bandari zote za Tanzania?

Nimeitoa sehemu naona Serikali ingejikita kutoa ufafanuzi hapo

Hakuna ambae hataki wawekezaji.
 
Jitambulishe kwanza wewe ni nani na kiwango chako Cha elimu halafu uwasilishe hoja yako, maswali au mapendekezo ndivyo tunavyofanya kwenye mijadla mikubwa ya kiserikali kama hii.
🤣🤣🤣🤭
 
Hovyo kabisa kuwa nani na elimu yake haisuini ?

Kama PHD ndo za kina mwigulu?

Au wasomi kina bashe?

Wasomi wenyewe.

wezi,wanangalia matumbo yao,
Watu wa kawaida ndo wenye
uchungu na nchi
 
Jitambulishe kwanza wewe ni nani na kiwango chako Cha elimu halafu uwasilishe hoja yako, maswali au mapendekezo ndivyo tunavyofanya kwenye mijadla mikubwa ya kiserikali kama hii.

Ndio maana chenge anawapiga kila uchwao
 
Kabla hamjakimbilia kutuambia faida na hasara, chambueni kwanza vipengele vya mkataba na mjibu maswali yanayoulizwa.

Nia ya kumtafuta DPW ilitokana na report ipi ya uchanganuzi wa ufanisi wa bandari?

Tenda iliyozishindanisha kampuni tofauti tofauti kisha ikapatikana DPW ilitangazwa wapi?

Mgao wa Tanzania kwenye huu mkataba utakuwa ni upi? Umeainishwa wapi?

Majukumu ya Tanzania kwenye Huu mkataba ni yapi?

Ukomo wa mkataba ni wa muda gani? Kwa nini?

Kwanini mkataba unahusisha bandari zote za Tanzania?

Nimeitoa sehemu naona Serikali ingejikita kutoa ufafanuzi hapo

Hakuna ambae hataki wawekezaji.
We inaonekana uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana. We ulitaka apewe nani, mambo ya ushinadani wa tenda hayatangazwi hadharani, hata hivyo waziri Mbarawa akiwa Mwanza alitaja makampuni yaliyoshindanishwa na DP World. DP World ndio ameibuka mshindi kwa vigezo vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na uwezo kifedha, kiteknojia, uzoefu, na kuwa na mtandao mkubwa duniani.
 
Kabla hamjakimbilia kutuambia faida na hasara, chambueni kwanza vipengele vya mkataba na mjibu maswali yanayoulizwa.

Nia ya kumtafuta DPW ilitokana na report ipi ya uchanganuzi wa ufanisi wa bandari?

Tenda iliyozishindanisha kampuni tofauti tofauti kisha ikapatikana DPW ilitangazwa wapi?

Mgao wa Tanzania kwenye huu mkataba utakuwa ni upi? Umeainishwa wapi?

Majukumu ya Tanzania kwenye Huu mkataba ni yapi?

Ukomo wa mkataba ni wa muda gani? Kwa nini?

Kwanini mkataba unahusisha bandari zote za Tanzania?

Nimeitoa sehemu naona Serikali ingejikita kutoa ufafanuzi hapo

Hakuna ambae hataki wawekezaji.
Hana mpinzani
 
Hovyo kabisa kuwa nani na elimu yake haisuini ?
Kama PHD ndo za kina mwigulu ???
Au wasomi kina bashe ?
Wasomi wenyewe wezi,wanangalia matumbo yao,
Watu wa kawaida ndo wenye uchungu na nchi
Karudishe hela ya watu we huna uwezo wa kujenga hoja yoyote na huna ufahamu wowote utaishia tu kutukana wenzio. Shenzy type, mkafanye kazi halali.
 
Alisaini mikataba thelathini na kenda huko uarabuni,,, kelele mmeanza mapema sana watanganyika wenzangu embu tulieni tuone na huko kwengine walipokabidhiwa pia,,tunywe kwanza mtori labda nyama tutazikuta chini,,sasa sijui ni nyama au tutatupiwa mijifupa iliyokwisha liwa na wao nasi tumalizie kuisasambua!!
 
Hatari
 
Ndugu zangu hii Dp world ni kitu gani mbona kimekuwa gumzo sana hapa nchini?

Kila kona ni dp world ni nini hiki?

Sisi tunawajua kina

Chama
Mayele
Saidoo
Diara
Manula
Mo
Gsm

Je huyu kidudu anayeikosesha nchi raha ni nani?
 
0898D4DA-BB53-4C41-A3D5-828B3FDBF44F.jpeg
 
Back
Top Bottom