MAREKANI NDANI YA BIBLIA:
Taifa la Marekani lilitabiliwa ktk kitabu cha UFUNUO 13
"Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa
Mwana-Kondoo, akanena kama joka." UFUNUO 13:11-18.
Chukua ufunguo wa maneno haya ki unabii: .
Ufunuo 13:1 anaanza kwa
kumwelezea mnyama aliyeibuka toka baharini, mnyama (utawala) alikuwa na majimbo 10 ya Ulaya. Yaani huu ni
utawala wa Roman Empire uliokuwa na majimbo kumi 10.
Na utawala huo wa mnyama wa kwanza (Ile pembe iliyoibuka) wa Ufunuo 13 ulikoma mwaka 1798 ambao
kiongozi wao mkuu wa utawala huo uliong'oa pembe tatu aliuawa akiwa mateka kule Ufaransa.
Mnyama wa pili: MAREKANI.
Katika kipindi hicho cha kuisha utawala wa mnyama wa kwanza mwaka 1798, taifa la Marekani linaibuka kutoka
ktk "nchi". Amerika inaitwa nchi kwa sababu katika historia ya kale kisiwa hicho hakikuwa kikikaliwa na mataifa,
walikuwepo wawindaji wachache (Red Indians) na baadae wakimbizi wa mateso ya kidini kwa watu walioshikilia
misingi ya Biblia walikimbilia huko kujificha kuuawa (UFUNUO 12:6, WAEBRANIA 11:37).
Baadae karne ya 17 wakaanza kuwa taifa. Mwaka 1776 Marekani likawa taifa huru, mwaka 1787 likatengeneza
katiba yake, Bill of Rights 1791, na likatambulika kimataifa mwaka 1798 baada ya mkutano na azimio la Virginia
(General Assembly of Virginia 1798). Hakuna taifa ambalo lilivaa sifa zote zilizotajwa ktk Ufunuo 13:11
isipokuwa ni Marekani tu.
********************************
Marekani atanena kama Joka,maana yake kama ambavyo shetani anaongoza tawala na mtu mmoja mmoja
kumwasi Mungu, hivyo ktk SIKU SI NYINGI ZIJAZO Marekani itawalazimisha watu kuabudu kinyume na hitaji la
Mungu, lkn pia kinyume na katiba yao ambayo imejengwa juu ya itikadi mbili yaani pembe mbili zilizotajwa ktk
Ufunuo 13:11 (Civil and Religious Liberty) au "government without a king" and "Church without a Pope". Kwa hiyo katiba ya Marekani imejengwa juu ya itikadi hizo mbili hadi leo.
Mda si mwingi yatatimia hayo, akiwalazimisha atakuwa anamfanyia "sanamu" yule mnyama
wa kwanza wa Ufunuo 13.
Kwa hivyo tupo kwenye kilele cha utawala wa Marekani hapa duniani. Ndiyo maana mnaona leo Marekani
anapeleka majeshi Korea. Lkn hajaanza leo, ameangusha tawala kadha wa kadha aidha yeye mwenyewe au na
washirika wake. Msitegemee nchi yoyote kuishinda marekani, hata kama itarudi nyuma ktk vita yoyote, badae
itasonga mbele na itashinda tu.
Baada ya marekani utawala utakaofuata ni wa Mwana Kondoo Yesu (UFUNUO 14). Unaweza ukajua tupo karibu
na mwisho wa dunia kiasi gani. Basi ikiwa hivyo ndivyo, tujiandaeni si mbali mlango wa rehema utafungwa mara
tu marekani atakapotangaza amri ya kuabudu jumapili, kundi la tulioufahamu ukweli kisha kushupaza shingo
kuufuata tutafungiwa nje.
Utabaki kwa ambao hawajaufahamu ukweli ambao nao injili itawafikia kwa kasi kubwa
kwa mda mfupi nao watafungiwa rehema kisha Yesu ashuke.
Huenda ni wewe umeufahamu ukweli lkn hutaki kuufuata kwa sababu labda za maslahi, heshima au vinginevyo.
Angalia utafungiwa nje na usiokolewe Yesu akija,...udini wa mtawala kama Trump ni kengele kuelekea kutimia
yaliyotabiriwa, huenda asiwe yeye lkn ni lazima itatimia marekani hasa ukizingatia dalili zote zilishatangulia
kutimia, limebaki hilo tu la Marekani, nalo muda si mbali litatimia na Yesu arudi duniani mara ya pili.
Nakusihi mpendwa, kwa neema ya Bwana wetu Yesu, na kwa ushirika wa Roho Mtakatifu, amka!!!..inua kichwa
chako! Usijekufungiwa mlango wa rehema, na zaidi hujui hata lini mishale ya mauti itakuchoma! Utalala ukiwa
upande gani? Mfuate Yesu leo, na si kumfuata tu, bali mfuate ktk njia sahihi, njia nyembamba ambayo
waiendeayo ni wachache.
Yesu alikwisha tuonya akisema "Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu,
kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia" LUKA 21:28.
Mungu awabariki mnapotafakari ujumbe huu, amina