Kwanini bei ya Volkswagen iwe juu wakati zinatengenezwa Rwanda?

Kwanini bei ya Volkswagen iwe juu wakati zinatengenezwa Rwanda?

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Tumeona baada ya ziara ya Mhe. Rais ktk nchi ya Rwanda ambao ni majirani zetu kila mmoja wetu ameshangaa na kuduwaa kuona magari Bomba aina ya volxwagon yanatengenezwa nchini Rwanda.

Nimejiuliza swali moja:
1. Kwanini bei ya magari hayo yanayotengenezwa Rwanda bado bei yake iko juu hapa Tanzania?! Je, magari hayo hayana soko hapa Tanzania?

Tunaomba Serikali yetu kupitia Wizara ya viwanda na biashara iruhusu wafanya biashara wa Tanzania waruhusiwe kuingiza magari hayo nchini ili watanzania wapate fursa ya kununua kwa bei nafuu.
 
Hiyo ni assembly plant, parts zote ni import, faida pekee ni kutoa ajira. Kushuka bei utasubiri sana. Tanzania ilikuwepo TAMCO pale kibaha, ikiunganisha magari ya scania, enzi za mwl, bado kipo?
nafahamu kuwa wanaunganisha, lkn naamini bei itakuwa nafuu tofauti na zile za kuagiza kutoka Japan n.k
 
Rwanda hawana uwezo wakutengeneza haya magari wa naunganisha vipuli toka ujeruman huko kama ILIVO kwenu tz matrekta ya suma jkt
sawa wanunganisha sisi je tunaweza kuunganisha hata pikipiki?

wenzetu Rwanda angalu wamepiga hatua ya kuunganisha hayo magari ya kifahari,

sisi tuna nyumbu lkn nyumbu yenyewe ni kama vile haipo.

Mawaziri wetu na watendaji wengine ktk idara mbalimbali za serikali badilikeni.....tunapaswa tukimbie.

wenzetu Rwanda wana kiwanda cha kutengeneza simu sisi bado tunaagiza kutoka china.

Tanzania kama ikiamua kutumia fursa ya kuwa kisiwa cha amani na utulivu tulipaswa sisi ndio tuwe vinara wa kusambaza bidhaa mbalimbali kwa nchi zinazo tuzunguka.
 
Ila Kagame huwa ana mambo ya mihemko & mkurukupo eti kuna kipindi alitaka kununua S-400 ya mrusi sijui alikuwa analenga nini
 
The One that got away
Screenshot_2021-08-03-20-30-52-1.png

Ngoja tujikumbushe nukuu ya Kitwanga
 
watanzania kazi yetu ni kuchonga maneno na kupiga fitina na majungu. tubadilike jamani, unakuta wasomi wazima walio elemika wamekabidhiwa dhamana hamna kitu!!

kwa sasa basi tuwe soko kwa ndugu zetu wa Rwanda, tuanze kuagiza Magari hayo ili angalau tyuwaunge mkono jirani zetu badala ya kuagiza magari kutoka Japani.
Subiri maneno mengi na ujuwaji mwingi watakavyo anza kuchonga!
 
Tumeona baada ya ziara ya Mhe. Rais ktk nchi ya Rwanda ambao ni majirani zetu kila mmoja wetu ameshangaa na kuduwaa kuona magari Bomba aina ya volxwagon yanatengenezwa nchini Rwanda.

Nimejiuliza swali moja:
1. Kwanini bei ya magari hayo yanayotengenezwa Rwanda bado bei yake iko juu hapa Tanzania?! Je, magari hayo hayana soko hapa Tanzania?

Tunaomba Serikali yetu kupitia Wizara ya viwanda na biashara iruhusu wafanya biashara wa Tanzania waruhusiwe kuingiza magari hayo nchini ili watanzania wapate fursa ya kununua kwa bei nafuu.
Yanakuwa assembled tu.
 
Hio ni garage iliochangamka. Not a serious assembly plant.
wewe hiyo garage yako iliyo changamka hata kuunganisha pikipiki iko wapi?
ndugu zangu watanzania badilikeni, punguzeni ujuwaji mwingi!
kuchonga maneno mengi hakuna vitendo.
tunacho jua sisi ni fitina na majungu basi.
tubadilike
ikiwezekana na sisi tuanze kuunganisha hata vitz tu.
 
Tunaomba Serikali yetu kupitia Wizara ya viwanda na biashara iruhusu wafanya biashara wa Tanzania waruhusiwe kuingiza magari hayo nchini ili watanzania wapate fursa ya kununua kwa bei nafuu.
Mimi nilifikiri kuwa utaishauri Serikali yetu nayo ianze kutengeneza magari hayo hapa nchini kwetu ili bei iwe chini zaidi lakini umeshauri kitu tofauti kabisa!

My take:
Mtu mweusi ni Kima aliechangamka.
 
hata kama wana unganisha naamini bei itakuwa chini haiwezi kuwa sawa na kuagiza Japani
Kumbe gari zenyewe pia huzijui ni za wapi VW sio mjapan ni mzungu na kitu cha mzungu ni imara hana longolongo.

Sio kisa wana assembly pale ndio bei iwe chini Hapana hata Pikipiki za Mchina zinakuja kwenye Mabox lkn bei yake imesimama
 
hatuna hata kiwanda cha kutengeneza simu.
wenzetu Rwanda Rwanda wanacho.
kwa kweli nyie mawaziri na watendaji mnao ambatana kwenye ziara za Mhe.Rais kama hmuwezi kujifunza na kubadilika mtakuwa watu wa ajabu sana.
tunataka kuona mabadiliko
 
wewe hiyo garage yako iliyo changamka hata kuunganisha pikipiki iko wapi?
ndugu zangu watanzania badilikeni, punguzeni ujuwaji mwingi!
kuchonga maneno mengi hakuna vitendo.
tunacho jua sisi ni fitina na majungu basi.
tubadilike
ikiwezekana na sisi tuanze kuunganisha hata vitz tu.
Punguza mihemko. Ulifikiri hilo ni bonge la kiwanda la magari. Pikipiki kibao zinaungwanishwa hapa hapa Tz. Itafika wakati hata magari yataunganishwa hapa. Omba picha au video ya hio assembly plant ya Rwanda tuone.
 
Back
Top Bottom