Kwanini benki hutoza wateja ada kwa kutoa pesa zao wenyewe?

michibo

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
2,315
Reaction score
3,915
Habari za leo wakuu,

Leo tujadili hizi tozo za mabenki [withdrawal charges] kwa wateja ambao kimsingi ndio wamiliki wa fedha hizo.

Mteja anatunza pesa yake benki, na benki zinaifanyia biashara [kukopesha] kwa faida. Kisha mmiliki akihitaji kutoa kiasi chochote kwa matumizi yake hutozwa 'ada' kiasi fulani.

Hii imekaaje?

Ni afadhali wangeishia kuchaji zile ada za kuhifadhi tu, kama ni kwa mwezi au vyovyote.

Angalau tungejua ni gharama ya kutunza fedha, lakini hii ya kila unapotoa wanakata ni WIZI tu kama WIZI mwingine.

Kama kuna sababu zenye mashiko hebu tuzijadili hapa.

Nawasilisha.
 
Jana nimefanya utafit kila baada ya muda nachungulia salio kwa simu, mara 3 nimekuta lipo the same.weeee mara ya 4 nikakuta 1500 imepungua,wezi sn
 
Mada ya Mtoa hoja ni fikirishi na inahitaji exposure kidogo kwenye masuala ya monetary na banking system hasa katika nchi zilizopiga hatua kubwa kiuchumi.

Ukizitazama nchi zenye uchumi mzuri kifedha mathalani China kwa mfano, wao huamini benki ndizo zilipaswa kuwalipa wateja wao kwa kutunza fedha kwao (japo sina hakika kama linafanyika hilo) ila jambo nililolithibitisha ni kwamba HAKUNA CHARGES ZOZOTE ANAZOTOZWA MTEJA AFANYAPO MUAMALA WOWOTE WA KIFEDHA. Kwa maana nyingine ni kwamba kuna zero charges katika mifumo yao ya kawaida ya kibenki mathalani ATM n.k na kama ulikuwa na 100k kwenye akaunti yako haijalishi utatazama salio mara ngapi salio lako litabaki kuwa 100k na siku ukienda kutoa unaweza ukitoa 100k yote.

Jambo hilo linawezekana kufanyika hata hapa kwetu ikiwa serikali yetu kupitia kupitia Wizara ya fedha itaamua kuyaelekeza mabenki (kupitia BOT) kuondoa tozo za miamala yote ya kifedha katika benki zao.

Tatizo tulilo nalo sisi Tanzania ni kuwa serikali ndiyo inayoyahimiza mabenki kuweka tozo kama kodi ya serikali katika miamala inayofanyika. Kwa maana nyingine serikali ndiyo inayotubebesha mzigo huu.

AMANI IWE NANYI
 
Ndio mzunguko Wa pesa huo lazima uliwe kidogo .
 
Kuna haja ya kupewa risiti kila nitazamapo salio.
 
Vishingi vyako laki tano unavyoweka leo asubuhi na kuvichukuwa kwesho jioni ndiyo benki wafanyie biashara ya kukopesha watu? Hivi unadhani gharama za kuendesha benki 7/24, infrastructure zake zote siyo gharama? Anzisha yako au tafuta watu mfanye ushirika muanzishe ya kwenu na muwape wateja huduma kama unavyosema. Bila shaka wateja wengi watahamia kwenu kwani gharama zenu zitakuwa ndogo sana.
 

Jenga hoja mkuu, acha kushambulia mtu kwa mipasho.
 
We unadhan risk ya kutunza hela ya mtu ni ndg?

Tunza nyumbani kwako kwenye kibubu ndo utatatoa bure.
 
Mfanyakazi wa Benki ndio mshirika mkuu wa wizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…