Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mada ya Mtoa hoja ni fikirishi na inahitaji exposure kidogo kwenye masuala ya monetary na banking system hasa katika nchi zilizopiga hatua kubwa kiuchumi.
Ukizitazama nchi zenye uchumi mzuri kifedha mathalani China kwa mfano, wao huamini benki ndizo zilipaswa kuwalipa wateja wao kwa kutunza fedha kwao (japo sina hakika kama linafanyika hilo) ila jambo nililolithibitisha ni kwamba HAKUNA CHARGES ZOZOTE ANAZOTOZWA MTEJA AFANYAPO MUAMALA WOWOTE WA KIFEDHA. Kwa maana nyingine ni kwamba kuna zero charges katika mifumo yao ya kawaida ya kibenki mathalani ATM n.k na kama ulikuwa na 100k kwenye akaunti yako haijalishi utatazama salio mara ngapi salio lako litabaki kuwa 100k na siku ukienda kutoa unaweza ukitoa 100k yote.
Jambo hilo linawezekana kufanyika hata hapa kwetu ikiwa serikali yetu kupitia kupitia Wizara ya fedha itaamua kuyaelekeza mabenki (kupitia BOT) kuondoa tozo za miamala yote ya kifedha katika benki zao.
Tatizo tulilo nalo sisi Tanzania ni kuwa serikali ndiyo inayoyahimiza mabenki kuweka tozo kama kodi ya serikali katika miamala inayofanyika. Kwa maana nyingine serikali ndiyo inayotubebesha mzigo huu.
AMANI IWE NANYI
Benki siyo kama parishi ya kanisa inayofanya mambo kwa bila faida. Kwa mfano benki moja niliyokuwa na na account, hata kama hakuna fedha kama hujaifunga utachajiwa fee kila mwezi.
Ya kwetu. 🤣 . Asante kwa kuzidi kukazia kuwa hakuna cha bure kama mlalamikaji anavyotaka iwe.Parishi ya wapi inayofanya mambo yake bila faida?
Vishingi vyako laki tano unavyoweka leo asubuhi na kuvichukuwa kwesho jioni ndiyo benki wafanyie biashara ya kukopesha watu? Hivi unadhani gharama za kuendesha benki 7/24, infrastructure zake zote siyo gharama? Anzisha yako au tafuta watu mfanye ushirika muanzishe ya kwenu na muwape wateja huduma kama unavyosema. Bila shaka wateja wengi watahamia kwenu kwani gharama zenu zitakuwa ndogo sana.
Ni vema umekiri huna ufahamu, basi jifunze kusikiliza wakubwa wakiongea.
Mimi nimewaambia hawana hoja wakanishukia Kama mwewe.🤣 🤣 🤣 🤣 🤣Mtanzania kwa ''utaalam'' tu. Akisoma kidogo nadharia utadhani yeye ndiye mwanzilishi wake. Haya mnayolalamika hapa yote ni upuuzi wa hali ya juu, na yanatokana na kukosa exposure. Mtu kama wewe unaonekana umeenda hivi vyuo vya kata basi umekuwa kama yule kipofu aliyeona mwezi. Kukaa kwangu nje kumenifanya niwe na account kwenye benki mbalimbali. Hizi fees mnazolalamikia haziepukiki kwani ndiyo zinafanya benki ziwepo. Benki siyo kama parishi ya kanisa inayofanya mambo kwa bila faida. Kwa mfano benki moja niliyokuwa na na account, hata kama hakuna fedha kama hujaifunga utachajiwa fee kila mwezi. Vile vile mwenye fedha naye anachajiwa fee kila mwezi.
Point yangu ni mm bank inakupa namna mbali mbali za ww kuipata hela yako kwa urahis ndio maana kuna Atm, mawakala na njia nyengine so.hzo njia zitafanikiwaje.kama.hakuna pesa?Umesoma na ukaelewa mada?
Ya kwetu. [emoji1787] . Asante kwa kuzidi kukazia kuwa hakuna cha bure kama mlalamikaji anavyotaka iwe.
Una hoja nzuri sana. Zaidi naongezea gharama za kuangalia salio. Nataka kuangalia kujua kiasi gani cha pesa nilichonacho, sasa kwanini unitoze kuangalia pesa zangu mwenyewe? Huduma za kutuma pesa ni sawa kwasababu mnanisaidia kifikisha pesa kwa mwingine.
Habari za leo wakuu,
Leo tujadili hizi tozo za mabenki [withdrawal charges] kwa wateja ambao kimsingi ndio wamiliki wa fedha hizo.
Mteja anatunza pesa yake benki, na benki zinaifanyia biashara [kukopesha] kwa faida. Kisha mmiliki akihitaji kutoa kiasi chochote kwa matumizi yake hutozwa 'ada' kiasi fulani.
Hii imekaaje?
Ni afadhali wangeishia kuchaji zile ada za kuhifadhi tu, kama ni kwa mwezi au vyovyote.
Angalau tungejua ni gharama ya kutunza fedha, lakini hii ya kila unapotoa wanakata ni WIZI tu kama WIZI mwingine.
Kama kuna sababu zenye mashiko hebu tuzijadili hapa.
Nawasilisha.
Una hoja nzuri sana. Zaidi naongezea gharama za kuangalia salio. Nataka kuangalia kujua kiasi gani cha pesa nilichonacho, sasa kwanini unitoze kuangalia pesa zangu mwenyewe? Huduma za kutuma pesa ni sawa kwasababu mnanisaidia kifikisha pesa kwa mwingine.
baraa la europe,nchi niliyopo unakatwa pesa ya insuarance tu,na hapo mnalijadili wakati wa kufungua account ,hakuna makato mengine,hiyo insurance ni kwa manufaaa yako mfano ukifariki au kupata ajali kazini ikakufanya uwe kilema au usiweze kufanya kazi ,unapewa zaidi ya euro 60k zaidi ya milioni 160 za bongo,hapo mnajadili ukatwe kila mwisho
Kuangalia salio wapo right kukata. Kwa mfano una milioni ishirini na nne laki tatu na sabini na saba elfu na mia mbili hamsini, ukisema uhesabie mwenyewe utatumia muda gani? Sasa wewe unakuwa umeipa kazi mashine ikuhesabilie pesa yako kwa muda mfupi kwa TZS 350 TU.
Hoja hujaiona? Nimesema kuendesha benki ni gharama. Hata unapo-withdraw fedha unatumia resources za benki. Na gharama za kuhifadhi fedha zako.