Kwanini benki hutoza wateja ada kwa kutoa pesa zao wenyewe?

Kwanini benki hutoza wateja ada kwa kutoa pesa zao wenyewe?

Wanatukata hata kuangalia salio kwenye ATM! Halafu mwisho wa mwaka wanatangaza faida ya mabilioni kumbe ni vibaka tu km wengine. Ni wizi mtupu - NMB Tanzania. Hivi nyie NMB Tanzania mngejisikiaje kama Vodacom, Tigo, Aritel, Halotel nk wangewakata muda wa maongezi kwenye simu zenu kila mnapoangalia salio?
Mkuu haya ni matatizo ya nchi zinazoendelea tu. USA na developed countries zingine kama unatoa hela kwenye ATM za benki husika ulipo na account yako ni bure. Kuangalia salio benki karibu zote zina apps unacheck tu kiganhani free.
 
Kwani Ulaya, Japan na US benki zao hazina gharama hizo? Mmezoea kupigwa tu. Mnaona kawaida.
Ogopa sana kuona Biashara ambayo wanakodi jengo kuubwa, wanaajiri watu na elimu zao za juu, wana ajiri kampuni za ulinzi, wanatoa tenda za internet, kuweka ATM mashine ili tu kukutunzia wewe elfu kumi (10,000) yako.
 
Kuangalia salio wapo right kukata. Kwa mfano una milioni ishirini na nne laki tatu na sabini na saba elfu na mia mbili hamsini, ukisema uhesabie mwenyewe utatumia muda gani? Sasa wewe unakuwa umeipa kazi mashine ikuhesabilie pesa yako kwa muda mfupi kwa TZS 350 TU.

Nimeandika nikafuta, ila nilimaanisha umeandika utumbo.
 
Tena kama safari hii mshahara ulichelewa kutoka wamevuna kweli za kuangalia salio.

Majizi wakubwa sana, wana-take advantage ya uelewa duni wa wateja kudhani pesa yao ni hisani.
 
Back
Top Bottom