Kwanini benki hutoza wateja ada kwa kutoa pesa zao wenyewe?

Ogopa sana kuona Biashara ambayo wanakodi jengo kuubwa, wanaajiri watu na elimu zao za juu, wana ajiri kampuni za ulinzi, wanatoa tenda za internet, kuweka ATM mashine ili tu kukutunzia wewe elfu kumi (10,000) yako.
 
Me huwa sielewagi hata kwanini kutoa hela yako mwenyewe kuwe na charges (simu na benki)

Hiyo sasa cha mtoto... kubwa kuliko ni hii ya kukatwa hela unapoangalia salio sijui hata ni nani alianzishaga huu wizi na upumbavu

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 

Kweli yako mkuu
Naona hili lipo Tz tu na huo ni wizi kama wizi mwingine tu
Mbona Ulaya hawana mambo haya
Naweka hela Bank zinaongezeka ingawa ni % ndogo ila makato hakuna ya kutolea wala ya kuangalia salio wala ya kuweka
Nashangaa sana kwa hili
 
Benki siyo kama parishi ya kanisa inayofanya mambo kwa bila faida. Kwa mfano benki moja niliyokuwa na na account, hata kama hakuna fedha kama hujaifunga utachajiwa fee kila mwezi.

Parishi ya wapi inayofanya mambo yake bila faida?
 

Duuh, jamaa umetoa makavuu! [emoji3525][emoji3525]
 
Zile karatasi na uchapishaji siyo bure...

Huduma za kutunza na kuendesha ATM siyo bure...
 
Ni vema umekiri huna ufahamu, basi jifunze kusikiliza wakubwa wakiongea.

Mimi nimewaambia hawana hoja wakanishukia Kama mwewe.

Wao wanadhan hizo ATM machine bank inapewa na serikali? Walinzi n.k
 
Bank haifanyii biashara pesa ya mtu bila mkataba unaweka leo keshokutwa umechukua hata usipochukua keshokutwa hawajui utaibeba lini so zile nigharama za kukuhifadhia cash yako hutaki nunua kibubu
 
Umesoma na ukaelewa mada?
Point yangu ni mm bank inakupa namna mbali mbali za ww kuipata hela yako kwa urahis ndio maana kuna Atm, mawakala na njia nyengine so.hzo njia zitafanikiwaje.kama.hakuna pesa?
 
Kuangalia salio wapo right kukata. Kwa mfano una milioni ishirini na nne laki tatu na sabini na saba elfu na mia mbili hamsini, ukisema uhesabie mwenyewe utatumia muda gani? Sasa wewe unakuwa umeipa kazi mashine ikuhesabilie pesa yako kwa muda mfupi kwa TZS 350 TU.
 

Naung mkono hoja,na serikali imefumbia macho swala hilo miaka yote,its doesn’t make sense,pesa ya mtu kaiweka na bank inanufaika nayo ila unakatwa makato ya kuangalia salio lako,,tozo za withdraw pesa,tozo za mwezi du,mabank ya kiafrica balaa sana,mi naishi baraa la europe,nchi niliyopo unakatwa pesa ya insuarance tu,na hapo mnalijadili wakati wa kufungua account ,hakuna makato mengine,hiyo insurance ni kwa manufaaa yako mfano ukifariki au kupata ajali kazini ikakufanya uwe kilema au usiweze kufanya kazi ,unapewa zaidi ya euro 60k zaidi ya milioni 160 za bongo,hapo mnajadili ukatwe kila mwisho
Wa mwezi au kila baada ya miezi 6 na ni hela mbuzi,wao wanathamini wewe kuweka pesa katika bank yao na wao wanaifanyia biashara sio kama bongo umeweka wanakata hadi kuangalia salio aisee
 
Ukitaka kujua ni wizi ambao Benki Kuu imeunyamazia, tembelea nchi nyingine. Nimekaa Ulaya, Asia na America. Na kote nilikuwa na akaunti. Sikuwahi kukatwa pesa kwa kutoa kwenye akaunti yangu! Huu ni wizi tu ila wezi wanatumia kalamu na wamekaa kwenye ofisi nzuri na AC juu.
 
Gharama ya kuangalia salio nao ni wizi mwingine. Hebu fikiria Vodacom, Airtel, Halotel, Tigo... nao wangemua kukata muda wa maongezi kila unapoangalia salio! Benki zenyewe zingelalamika. Na ukitaka kujua ni wizi, kwa nini Japan, Ulaya... hakuna makato ya kuangalia salio? Eti hata ukiangalia kwa ATM, wanakata pesa yako!!
 
Umeona eh? Huu wizi hauko nchi zilizoendelea. Ni wizi wa mchana kweupe na serikali imeufumbia macho.
 
Kwa nini Ulaya hawatukati kuangalia salio? Usitetee wizi. Nyie watu wa benki tafuteni njia nyingine ya kupata faidia siyo kuibia watu pesa zao. Acheni unyang'anyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…