KERO Kwanini Benki ya NMB Tawi la Chamwino wanatumia Mhudumu (TELLER) mmoja tu wakati madirisha yapo mawili?

KERO Kwanini Benki ya NMB Tawi la Chamwino wanatumia Mhudumu (TELLER) mmoja tu wakati madirisha yapo mawili?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa muda mrefu sasa benki ya NMB tawi la Chamwino dirisha linalotumika kutoa huduma ni moja tu wakati kuna madirisha mawili ila moja halina mhudumu kwa muda mrefu sasa.

Hali hii inasababisha usumbufu kwa wateja na kutumia muda mrefu kupata huduma muda ambao tunaweza kutumia kufanya shughuli zingine za kiuchumi.

Kama tatizo ni uhaba wa wafanyakazi ni vema benki ya NMB ikaongeza Teller katika tawi la Chamwino ili wananchi wapate huduma bora kwa wakati
 
Benki nyingi kotenchini zimekuwa na hii tabia ya kutumia madirisha machache ya kutolea huduma na hivyo kusababisha foleni isiyo na ulazima kwa wateja.

Ushauri kwao; Wabadilike na waheshimu muda kwa wateja wao.
 
Back
Top Bottom