Kwanini Biashara ya Sukari inasimamiwa na Waziri wa Kilimo?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hivi Nchini Tanzania hakuna Wizara ya Viwanda na Biashara , ambayo ndio Mhusika halisi wa Biashara na Viwanda?

Naandika haya kwa Uzoefu, mimi ni Mfanyabiashara na namiliki Kiwanda (siyo cha sukari). Sijawahi kuelekezwa kusaini nyaraka yoyote kwenye Wizara ya kilimo angalau mara chache nimefika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje , hii ni kwa sababu biashara yangu kwa 95% inahusiana na Nchi za kigeni , USA , CANADA , na kwa kiasi England na S.Africa.

Swali langu ni hili. Kwanini Waziri wa kilimo ashughulikie masuala ya Biashara?
 
kwani waziri wa viwanda na biashara ndio analima miwa humu nchini πŸ’

na kwani tatizo ni biashara ya sukari au kuathirika kwa uzalishaji wa sukari πŸ’
Ni jukumu la waziri mwenye dhamana ya kilimo kuwajibika katika masuala yote ya uzalishaji wa mazao ya kilimo mathalani miwa, korosho, pamba, mahindi na mazao mengine yote unayoyafahamu nakuingilia kati endapo patatokea changamoto itakayo athiri walaji kwa namna yeyote ile πŸ’
 
Sababu ya kwanini sukari iko chini ya wizara ya kilimo ni kutokana na demand yake kwa taifa ndio mana hata taifa likitaka kujikabili kutokana na njaa linaanza kutunza mahindi na sio mchele ndio mana NFRA wapo nchi nzima wakikusanya na kutunza mahindi kwaajili ya akiba ya taifa kwa mantik ya kama njaa iktokea ni rahisi watu kupewa mahind wakapka hata uji na sukari na maisha yakaenda kulko serekali kugawa mchele na ngano. Najaribu kukuelezea ila sjui kama utanielewa sababu mimi ni moja ya watumishi wa wizara ya kilimo
 
Mpaka ni upi kati ya Waziri wa Kilimo na Waziri wa Viwanda katika mazao yanayochakatwa nchini?
 
Mpaka ni upi kati ya Waziri wa Kilimo na Waziri wa Viwanda katika mazao yanayochakatwa nchini?
mpaka ni majukumu tu ambayo yako bayana kwenye wizara husika, mathalani NRFA - wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula iko chini ya wizara ya kilimo na kwa taarifa tu hii sio Tanzania tu nadhani ni Africa nzima iko hivi πŸ’

Yale mazao mengineyo ya kilimo yasio ya Chakula ndipo sasa wizara ulizozitaja husimamia kwa pamoja kila wizara kwa sehemu yake kwa utaratibu mzuri uliowekwa kuepuka mgongano πŸ’

kwahiyo wizara ya kilimo inahusika na hili moja kwa moja bila mbambamba, Lakini pia kwakua sukari yetu hutosheleza zaidi soko la ndani hapajawahi kuwa na changamoto ya kibiashara katika huduma hii πŸ’
 
Mamafia yameshikilia rimoti ; yanaongoza serikali ya awamu hii.

Tusitegemee sa100 atatusaidia katka hili.

Hakuna kitakachofanyika.

Ni sisi wenyewe wananchi ndio tutakaoweza kulimaliza hili (endapo tukiamua kutoka nyuma ya keyboard zetu na kuingia mtaani nchi nzima).
 
Hata Waziri wa biashara hapaswi kuingia jikoni
 
Ni Katibu wa Wahuni!! Wahuni wamekamatwa usukani na Kila mmoja ana kipande chake Cha kupiga.
 
Kwahiyo hata bange anapambana nayo Waziri wa Kilimo Kwa sababu inalimwa?

Mlisomea ujinga?
 
Kweli kabisa bwashee
 
ndugu,sukari inasimamiwa kwa sheria na ndio maana kuna bodi ya sukari ambayo imeundwa kwa sheria ya bunge,hivyo ni lazima isimamiwe
 
Fanyeni utafiti utakunana na majibu haya,
1. Kila wizara au idara inayosimamiwa na jinsia Ile , anaye teuliwa ni mama anayeongoza ni baba ambaye hakuteuliwa

2. Kutoa maamuzi ni baba ambaye hakuteuliwa na mtekeza maamuzi ni mama aliyeteuliwa na ambaye ni magumu kuielewa au kutekeleza maamuzi Yale.

Tunakoelekea tutasimama siku Moja bila kufahami kwanini tumesimama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…